Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,278
- 25,846
Imekuwa ikisemwa sana kuwa wapo askari polisi wasio waaminifu wanaowabambikia wananchi kesi kwa lengo la kuwaomba rushwa au kuwakandamiza. Ndiyo maana,sisi Mawakili hujitokeza kuwatetea watuhumiwa kwakuwa si wote waliotenda kweli
Huko mkoani Arusha,askari polisi mmoja amekamatwa kwa kuwabambikia wananchi madawa ya kulevya kama bangi kwa lengo la kuomba rushwa. Askari huyo aliyekamatwa,kwa mujibu wa ITV Habari,ni kielelezo na uthibitisho kuwa kubambika kesi kupo
Kimsingi,kutaja au kuhoji au hata kushtaki mwananchi kwa tuhuma fulani si mwisho wa mambo. Ni mwanzo tu unaoficha mambo mbalimbali yakiwemo ya watu kusingiziwa kesi au vizibiti. Ndiyo maana, ipo haja ya kuwa makini na kesi za wananchi na kuacha mapambano ya kimahakama yaseme na kutenda haki.