Lipyoto

Lipyoto

amulson

Member
Joined
Nov 18, 2010
Posts
54
Reaction score
12
Katika mikoa ya kusini mwa Tanzania, Lindi au Mtwara, kulikuwa na vijiji jirani viwili ambavyo watu wake walikuwa wanashirikiana kutumia maji ya mto mmoja unaopita baina ya vijiji hivyo. Mto ulikuwa na desturi ya kujaa maji msimu wa masika mvua zinapokuwa zinanyesha na kupungua sana maji wakati wa msimu wa kiangazi jua linapokuwa kali sana. Miaka nenda miaka rudi, wanakijiji waliendelea kuyatumia maji ya mto ule wakishirikiana kwa furaha na amani, mpaka walipokuja vurugwa na LIPYOTO.


Ilikuwa wakati wa msimu kiangazi. Maji yamekauka mtoni. Kupata maji ya matumizi ilibidi wanakijiji wa pande zote mbili wawahi asubuhi na mapema angalau wachote maji yaliyojikusanya kwenye vijisima vifupi walivyovichimba mtoni. Asubuhi moja wanakijiji ,kutoka upande mmoja wa mto,waliowahi kufika mtoni walistaajabu kukuta maji machache yaliyopo yamechafuliwa,hayafai kwa matumizi ya binadamu. Wakarudi kijijini kwao huku lawama zote za uchafuzi wa maji wakizielekeza kwa kijiji cha upande wa pili.


Wanakijiji wa upande wa pili nao walipofika mtoni wamechelewa wakakuta maji hayafai kwa matumizi. Wakawalaumu wale wa kijiji kingine kuwa wamewahi asubuhi wamechota maji kisha wakayachafua. Hasira za wanakijiji hawa ziliongezeka maradufu siku iliyofuata walipodamka kwenda mtoni asubuhi na mapema na kakuta maji yameshachafuliwa tena.


Minong'ono ikaenea vijiji vyote kila upande ukikishutumu kijiji jirani kuwa ndicho kinachohusika na uchafuzi wa maji. Uhasama ukaanza baina ya wakazi wa vijiji hivi jirani. Vita ya maneno ikakolea mpaka watu kutaka kushikana mashati. Kuona unga unataka kuzidi maji wazee wa pande zote mbili wakaingilia kati kutatua tatizo lililojitokeza.


Wazee kwa hekima zao wakaamua pawekwe ulinzi usiku kucha pale mtoni. Watu kutoka vijiji vyote viwili wakaweka kambi, wakakesha. Majira ya saa kumi alfajiri ndege mmoja mkubwa mkubwa,mbishi mbishi anatua kwenye vijisima vya wanakijiji. Anakunywa maji yaliyojikusanya kwenye vijisima,anaoga,mwisho anatimua timua maji yote. Watu waliokuwa wameweka ulinzi pale mtoni kuangalia,wakachoka kwa mshangao,Daaah!njomba umeona,kumbe LIPYOTO bwana wewe ndiye anataka tugombane


Lipyoto anatufundisha mambo mengi watanzania katika hii hali tuliyonayo sasa. huenda kuna Lipyoto hapa kati
 
Back
Top Bottom