Lipumba: Umechelewa japo sio sana (someone has written it somewhere)

Lipumba: Umechelewa japo sio sana (someone has written it somewhere)

Mimi niko neutral sijajua kura yangu niipe chama gani na najua watu wenye msimamo kama wangu tuko wengi.

Nadhani Ukawa wanapaswa watuambie watafanya nini badala ya kutuambia tu tunataka tuwaondoe CCM.

Tumeona katika nchi nyingine baadhibjirani zetu hakukuwa na mabadiliko yaliyowasaidia wananchi maskini katika nchi hizo baada ya kuondoa vyama tawala zaidi ya kujinufaisha kwa walioshika hatamu.

bila ya ccm kurudi kama upinzani hawataacha:-
1. kulala bungeni
2. kuitikia ndiyooooooo kwa vitu ambavyo hata hawajaviskia vizuri bungeni
3. kutetea maslahi ya chama badala ya taifa kisa tu wazo au mchango limetoka kwa wapinzani.
 
Lipumba kala ile mil 200 mliyompa sasa hatatimiza lemgo la kuvuruga ukawa basi ni full kuruka ruka na kukanyagana
 
Mimi niko neutral sijajua kura yangu niipe chama gani na...
kitakacho hajui akitakacho! Miezi miwili kabla ya uchaguzi hujajua nani umpe kura...hii ni sifa au ujinga?
...najua watu wenye msimamo kama wangu tuko wengi.
Mlikutania wapi na hao watu? Yaani ujue watu wenye msimamo kama wako lakini usijue upigeje kura, kweli hujui utakacho!
Nadhani Ukawa wanapaswa watuambie watafanya nini badala ya kutuambia tu tunataka tuwaondoe CCM.
Mbona tayari umeambiwa watakachofanya cha kwanza ni kuiondoa CCM. Baada ya hapo vuta subira kampeni karibu inaanza...
Tumeona katika nchi nyingine baadhibjirani zetu hakukuwa na mabadiliko yaliyowasaidia wananchi maskini katika nchi hizo baada ya kuondoa vyama tawala zaidi ya kujinufaisha kwa walioshika hatamu.
Hatuna hata nchi moja duniani au jirani ambayo imevumilia uozo wa miaka zaidi ya 50 wa chama kile kile bila mabadiliko...huu wa kwetu ni kushupaa!
 
Last edited by a moderator:
Jason baurne alishatutaadhaliksha ,wamechemka kwa CHADEMA sasa wameamia CUF.

Mwaka wa kufa Nyani huu, miti yote inateleza.
 
Tanzania kwanza vyama baadaye,vision ya ukawa ni kuunda chama kimoja kikubwa cha upinzani ili kuwa na uwezo wa kupambana na ccm,CHADEMA au CUF peke yake haviwezi kupambana na ccm,acha propaganda hatupo kwa ajili ya kugawana vyeo.
 
mbona CUF na CCM waliunda serikali ya mseto je CUF imebaki kwenye daftari la msajili?
 
Ccm ni waoga sana.... Hapa wanachokiogopa ni upinzani kuungana nakuwa chama kimoja chenye nguvu... Na inshaallah mnayoyataka yawe hayatakuwa.... Na kuhusu zanzibar, hata kama chadema haina strong base mjue wazanzibar hawaipendi na wala hawaihitaji ccm.. Mark my words, ccm zanzibar hawana chao mwaka huu... Kama kuna ambao wamekaa zenji watakuja hapa wakuambie

kweli jamaa wamekimbiwa kabisa hawana watu,wataabika mbona kwenye kampen
 
CCM haiwezi kuogopa muungano wa upinzani ambao Cement yake ni fedha chafu za Lowassa.
Ila hakika, upinzani Tanzania ndio kwaheri, Pengine labda mwaka 2099 ndio tutakuwa na upinzani
 
Jumapili iliyopita katika kipindi cha watoto ITV Shangazi alikuwa anawasimulia watoto kisa cha wanyama kumtafuta mfalme. Ili kutochosha namalizia mwishoni wakati simba anachaguliwa kuwa mfalme. Kamati ya uteuzi ilimchagua simba atawale baada ya ‘kuomba’ ateuliwe yeye, kwa sababu tu wanyama wengine wangemkataliaje simba ambaye licha ya kutoogopa lakini mnyama yeyote yuko hatarini wakati wa shida na wakati wa raha?

Mimi nilikuwa nayashangaa mambo yanayoendelea ndani ya UKAWA na sababu ya UKAWA ‘kuitaka’ CHADEMA imtoe mgombea urais. Lakini CHADEMA ‘inayoombwa’ kutoa mgombea urais ‘haina’ mtu anayeweza kuwa rais. Inamendea atakayetemwa na CCM. Ona sasa. CHADEMA inaye kijana machachali ambaye angeweza kuwa mgombea mwenza. Mr. Mwalimu. Badala yake inamchukua mtu muhimu na anayependwa sana CUF anakuwa mgombea mwenza. ‘Huyu mfalme’ anayeazima wa kukikalia kiti cha ufalme kwa nini asiwaachie wenye uwezo wakawa wafalme?

Nalisema sasa ili wasipochukua tahadhali likitokea watakaokumbuka wajifunze. CHADEMA yaweza kuwa na siri ya kuivunja CUF. CHADEMA haikubaliki Zanzibar. Kijana wake machachali Mwalimu anaandaliwa kuwa kiongozi kwa upande wa Zanzibar siku zijazo. Kama CUF itaendelea kuwa na nguvu bado huyu kijana hawezi kukubalika Zanzibar. Umachachali wake si kukubalika kwake hasa kama bado CUF ina nguvu. Njia pekee ni kuivunja uti wa mgongo CUF.

Akichukuliwa Duni akawa mwanachama wa CHADEMA atawavuta wengi kuikubali CHADEMA. Ikitokea CHADEMA ikashinda makubaliano yao waliyokubaliana bedirumu huwezi kuyaleta sebureni. Rais ataunda serikali CHADEMA inavyotaka na UKAWA itabaki historia. Uwezekano wa Duni kujiondoa na kuuacha uhondo wa umakamu wa Rais ni mdogo sana. Ikiwa hivyo basi wafuasi wa CUF watajipanga nyuma ya Duni na hivyo nyuma ya CHADEMA. Hapo CUF itabaki kwenye kumbukumbu za msajili wa vyama vya siasa.

Inahitaji kuwa na miwani mikali kuliona hilo. Na Lipumba ameliona. Ni msataarabu wa kutosha kutofanya vurugu. Tunaomkumbuka Thomas Sankara tunakumbuka. Alipogundua mkuu wa majeshi anataka kumpingua alimwita akamwambia: ‘Najua unachotaka kufanya. Nikikuua sasa wataniita muuaji. Sitaki. Endelea kukifanya sina la kufanya’. Baada ua wiki moja hivi Sankara alipinduliwa na kuuawa. Mpaka leo sijawahi kumtambua Kompaure japo sina serikali ya kumuumiza kwa kutomtambua.

Nasikia Ibrahimu Haruna Lipumba anataka kuachana na siasa. Lazima akifanya hivyo atatwambia sababu. Kwa ustaarabu wake hawezi kuitaja hii. Baada ya muda tutagundua kuwa hii ninayoiandika humu leo ndiyo iliyomfanya aachane na siasa. Mnajua Lipumba ni msataarabu sana? UKAWA hoyeeee!

Nasikia mtu wa kwanza kusema dunia ni mviringo aliuawa kwa amri ya uongozi fulani. naomba nisiuawe kwanza.

Swali dogo na la msingi ,hivi inawezekana umoja wa vyama tofauti kama UKAWA viongozi wake wote watokane na chama kimoja?.
 
CCM haiwezi kuogopa muungano wa upinzani ambao Cement yake ni fedha chafu za Lowassa.
Ila hakika, upinzani Tanzania ndio kwaheri, Pengine labda mwaka 2099 ndio tutakuwa na upinzani

Nikukumbushe tu hata makaburu wa South Afrika walikuwa na mawazo kama haya haya ya kwako na kikubwa kabisa wao raslimali zao Makaburu zilishatumika kuijenga hiyo South Afrika lakini kilichotea sote tumeona.

Nnawashukuru wananchi kwa sasa baadhi yao kwa wingi wao wanajitambua ,wataambizana na kupeana taarifa.Hii ni vita dhudi ya mkoloni mweusi ,ataondoka na mfumo wake mmbovu ulioshindwa kutoa matokeo yaliyotarajiwa.
 
Back
Top Bottom