Lipumba: Umechelewa japo sio sana (someone has written it somewhere)

Aloyce mk

Member
Joined
Nov 10, 2014
Posts
76
Reaction score
33
Jumapili iliyopita katika kipindi cha watoto ITV Shangazi alikuwa anawasimulia watoto kisa cha wanyama kumtafuta mfalme. Ili kutochosha namalizia mwishoni wakati simba anachaguliwa kuwa mfalme. Kamati ya uteuzi ilimchagua simba atawale baada ya ‘kuomba’ ateuliwe yeye, kwa sababu tu wanyama wengine wangemkataliaje simba ambaye licha ya kutoogopa lakini mnyama yeyote yuko hatarini wakati wa shida na wakati wa raha?

Mimi nilikuwa nayashangaa mambo yanayoendelea ndani ya UKAWA na sababu ya UKAWA ‘kuitaka’ CHADEMA imtoe mgombea urais. Lakini CHADEMA ‘inayoombwa’ kutoa mgombea urais ‘haina’ mtu anayeweza kuwa rais. Inamendea atakayetemwa na CCM. Ona sasa. CHADEMA inaye kijana machachali ambaye angeweza kuwa mgombea mwenza. Mr. Mwalimu. Badala yake inamchukua mtu muhimu na anayependwa sana CUF anakuwa mgombea mwenza. ‘Huyu mfalme’ anayeazima wa kukikalia kiti cha ufalme kwa nini asiwaachie wenye uwezo wakawa wafalme?

Nalisema sasa ili wasipochukua tahadhali likitokea watakaokumbuka wajifunze. CHADEMA yaweza kuwa na siri ya kuivunja CUF. CHADEMA haikubaliki Zanzibar. Kijana wake machachali Mwalimu anaandaliwa kuwa kiongozi kwa upande wa Zanzibar siku zijazo. Kama CUF itaendelea kuwa na nguvu bado huyu kijana hawezi kukubalika Zanzibar. Umachachali wake si kukubalika kwake hasa kama bado CUF ina nguvu. Njia pekee ni kuivunja uti wa mgongo CUF.

Akichukuliwa Duni akawa mwanachama wa CHADEMA atawavuta wengi kuikubali CHADEMA. Ikitokea CHADEMA ikashinda makubaliano yao waliyokubaliana bedirumu huwezi kuyaleta sebureni. Rais ataunda serikali CHADEMA inavyotaka na UKAWA itabaki historia. Uwezekano wa Duni kujiondoa na kuuacha uhondo wa umakamu wa Rais ni mdogo sana. Ikiwa hivyo basi wafuasi wa CUF watajipanga nyuma ya Duni na hivyo nyuma ya CHADEMA. Hapo CUF itabaki kwenye kumbukumbu za msajili wa vyama vya siasa.

Inahitaji kuwa na miwani mikali kuliona hilo. Na Lipumba ameliona. Ni msataarabu wa kutosha kutofanya vurugu. Tunaomkumbuka Thomas Sankara tunakumbuka. Alipogundua mkuu wa majeshi anataka kumpingua alimwita akamwambia: ‘Najua unachotaka kufanya. Nikikuua sasa wataniita muuaji. Sitaki. Endelea kukifanya sina la kufanya’. Baada ua wiki moja hivi Sankara alipinduliwa na kuuawa. Mpaka leo sijawahi kumtambua Kompaure japo sina serikali ya kumuumiza kwa kutomtambua.

Nasikia Ibrahimu Haruna Lipumba anataka kuachana na siasa. Lazima akifanya hivyo atatwambia sababu. Kwa ustaarabu wake hawezi kuitaja hii. Baada ya muda tutagundua kuwa hii ninayoiandika humu leo ndiyo iliyomfanya aachane na siasa. Mnajua Lipumba ni msataarabu sana? UKAWA hoyeeee!

Nasikia mtu wa kwanza kusema dunia ni mviringo aliuawa kwa amri ya uongozi fulani. naomba nisiuawe kwanza.
 
Umemsikia vizuri Mbowe jana kwa kumpongeza na kumshukuru Mwenyekiti Lipumba kumruhusu duni atoke CUF!! Kama hivyo ndio kwa nn ajitoe leo!! Acheni uzandiki nyie watu wa MAKUMBUSHO na LUMUMBA
 
Lipumba shemeji yake mbowe, kaowa kule kule, hana ujanja wakutoka kwenye saccos, sema amuuze maalim seif tu
 
Duh napita tu 🏃🏻🏃🏻🏃🏻🏃🏻🏃🏻🏃🏻🏃🏻
 
siasa ya mwaka huu ni ya kipekee sana na sizani kama itakuja kujirudia. Namshukuru Mungu kwa kushuhudia uhondo huu
 
Ccm ni waoga sana.... Hapa wanachokiogopa ni upinzani kuungana nakuwa chama kimoja chenye nguvu... Na inshaallah mnayoyataka yawe hayatakuwa.... Na kuhusu zanzibar, hata kama chadema haina strong base mjue wazanzibar hawaipendi na wala hawaihitaji ccm.. Mark my words, ccm zanzibar hawana chao mwaka huu... Kama kuna ambao wamekaa zenji watakuja hapa wakuambie
 
Lipumba shemeji yake mbowe, kaowa kule kule, hana ujanja wakutoka kwenye saccos, sema amuuze maalim seif tu

Mfano maridhawa wa mtu aliyefilisika hoja,pole sana.
 
Umeandika vizuri, lakini mjue maana ya chama au vyama vya siasa ni muungano wa watu wenye mtazamo sawa na wenye lengo la kuchukua Madaraka ya nchi. Lengo sio kuwa na vyama vingi visivyo na tija. Prof. Lipumba amekuwa CUF tangu 1990s amefanya nini la maana? Amegombea urais mara nne bila mafanikio bila shaka mwaka huu ilikuwa agombee tena bila mafanikio. Kwa nini wasiunganishe nguvu ili kuiondoa CCM madarakani?
Kama Lipumba anaondoka kwa sababu hiyo aende tupate sura mpya ya upinzani
 
mawazo negative.Watu wa hivi hata maendeleo ni shida kuyapata.Na walivyofanya ukawa ni jambo jema na wachache sana wataelewa sasa
 
Ccm ni waoga sana.... Hapa wanachokiogopa ni upinzani kuungana nakuwa chama kimoja chenye nguvu... Na inshaallah mnayoyataka yawe hayatakuwa.... Na kuhusu zanzibar, hata kama chadema haina strong base mjue wazanzibar hawaipendi na wala hawaihitaji ccm.. Mark my words, ccm zanzibar hawana chao mwaka huu... Kama kuna ambao wamekaa zenji watakuja hapa wakuambie
wazanzibari hawajawahi kuipenda ccm. ni jeshi la polisi ndilo huiweka madarakani CCM zanzibar.

Mkuu ccm hawajahi kuwa na chao zanzibar bali hunyang'anya tu kwa nguvu. Tofauti na miaka yote mwaka huu nguvu za ccm za kunyanganya zimekuwa diluted sana.
 
mkuu nakusoma sana...
 
Ukawa fans your leaders might be wrong learn to think for yourself
 
ni ndoto za mchana kufikiria CUF itakufa. hivi unawajua wapemba wewe? au unawasikia tu kwenye redio.

Jumapili iliyopita katika kipindi cha watoto ITV Shangazi alikuwa anawasimulia watoto kisa cha wanyama kumtafuta mfalme. Ili kutochosha namalizia mwaishoni wakati simba anachaguliwa kuwa mfalme. Kamati ya uteuzi ilimchagua simba atawale baada ya ‘kuomba’ ateuliwe yeye, kwa sababu tu wanyama wengine wangemkataliaje simba ambaye licha ya kutoogopa lakini mnyama yeyote yuko hatarini wakati wa shida na wakati wa raha?

Mimi nilikuwa nayashangaa mambo yanayoendelea ndani ya UKAWA na sababu ya UKAWA ‘kuitaka’ CHADEMA imtoe mgombea urais. Lakini CHADEMA ‘inayoombwa’ kutoa mgombea urais ‘haina’ mtu anayeweza kuwa rais. Inamendea atakayetemwa na CCM. Ona sasa. CHADEMA inaye kijana machachali ambaye angeweza kuwa mgombea mwenza. Mr. Mwalimu. Badala yake inamchukua mtu muhimu na anayependwa sana CUF anakuwa mgombea mwenza. ‘Huyu mfalme’ anayeazima wa kukikalia kiti cha ufalme kwa nini asiwaachie wenye uwezo wakawa wafalme?

Nalisema sasa ili wasipochukua tahadhali likitokea watakaokumbuka wajifunze. CHADEMA yaweza kuwa na siri ya kuivunja CUF. CHADEMA haikubaliki Zanzibar. Kijana wake machachali Mwalimu anaandaliwa kuwa kiongozi kwa upande wa Zanzibar siku zijazo. Kama CUF itaendelea kuwa na nguvu bado huyu kijana hawezi kukubalika Zanzibar. Umachachali wake si kukubalika kwake hasa kama bado CUF ina nguvu. Njia pekee ni kuivunja uti wa mgongo CUF.

Akichukuliwa Duni akawa mwanachama wa CHADEMA atawavuta wengi kuikubali CHADEMA. Ikitokea CHADEMA ikashinda makubaliano yao waliyokubaliana bedirumu huwezi kuyaleta sebureni. Rais ataunda serikali CHADEMA inavyotaka na UKAWA itabaki historia. Uwezekano wa Duni kujiondoa na kuuacha uhondo wa umakamu wa Rais ni mdogo sana. Ikiwa hivyo basi wafuasi wa CUF watajipanga nyuma ya Duni na hivyo nyuma ya CHADEMA. Hapo CUF itabaki kwenye kumbukumbu za msajili wa vyama vya siasa.

Inahitaji kuwa na miwani mikali kuliona hilo. Na Lipumba ameliona. Ni msataarabu wa kutosha kutofanya vurugu. Tunaomkumbuka Thomas Sankara tunakumbuka. Alipogundua mkuu wa majeshi anataka kumpingua alimwita akamwambia: ‘Najua unachotaka kufanya. Nikikuua sasa wataniita muuaji. Sitaki. Endelea kukifanya sina la kufanya’. Baada ua wiki moja hivi Sankara alipinduliwa na kuuawa. Mpaka leo sijawahi kumtambua Kompaure japo sina serikali ya kumuumiza kwa kutomtambua.

Nasikia Ibrahimu Haruna Lipumba anataka kuachana na siasa. Lazima akifanya hivyo atatwambia sababu. Kwa ustaarabu wake hawezi kuitaja hii. Baada ya muda tutagundua kuwa hii ninayoiandika humu leo ndiyo iliyomfanya aachane na siasa. Mnajua Lipumba ni msataarabu sana? UKAWA hoyeeee!

Nasikia mtu wa kwanza kusema dunia ni mviringo aliuawa kwa amri ya uongozi fulani. naomba nisiuawe kwanza
 
Umeandika vizuri, lakini mjue maana ya chama au vyama vya siasa ni muungano wa watu wenye mtazamo sawa na wenye lengo la kuchukua Madaraka ya nchi. Lengo sio kuwa na vyama vingi visivyo na tija. Prof. Lipumba amekuwa CUF tangu 1990s amefanya nini la maana? Amegombea urais mara nne bila mafanikio bila shaka mwaka huu ilikuwa agombee tena bila mafanikio. Kwa nini wasiunganishe nguvu ili kuiondoa CCM madarakani?
Kama Lipumba anaondoka kwa sababu hiyo aende tupate sura mpya ya upinzani

Mimi niko neutral sijajua kura yangu niipe chama gani na najua watu wenye msimamo kama wangu tuko wengi.

Nadhani Ukawa wanapaswa watuambie watafanya nini badala ya kutuambia tu tunataka tuwaondoe CCM.

Tumeona katika nchi nyingine baadhibjirani zetu hakukuwa na mabadiliko yaliyowasaidia wananchi maskini katika nchi hizo baada ya kuondoa vyama tawala zaidi ya kujinufaisha kwa walioshika hatamu.
 
Back
Top Bottom