Lipumba na Mutungi waumbuka wizi wa fedha za ruzuku CUF washindwa kuwasilisha hesabu zaidi ya tshs1.6 bilioni kwa CAG

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
LIPUMBA NA JAJI MUTUNGI WAUMBUKA WIZI WA FEDHA ZA RUZUKU YA CUF, WASHINDWA KUWASILISHA HESABU ZA FEDHA ZAIDI YA TSHS.1.6 BILIONI KWA CAG:

Na. Mbarala Maharagande.

KWA MARA YA KWANZA, katika historia iliyotukuka ya CUF chini ya Uongozi wa Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad ambaye mara zote amekuwa akisimamia vyema utendaji wa shughuli za Chama na kuwasilisha Hesabu za Fedha za CUF mbele ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa wakati na mara zote kupatiwa Hati safi.

Lipumba na kundi lake wameshindwa kufanya hivyo kutokana na Ubadhilifu mkubwa unaoendelea kufanywa na Genge lake. Mpaka February 2018, inakadiriwa kuwa zaidi ya Tshs 1.6 bilioni zimetolewa na Jaji Mutungi kwa njia tofauti tofauti za PANYA na kinyume na Taratibu na Sheria za fedha. Mara ya kwanza ilikuwa January 6, 2017 jumla ya Tshs. 369,378,502.64/= milioni zilitolewa kwa njia ya wizi na kwa mazingira tatanishi kupitia akaunti Na.2072300456 ya benki ya NMB tawi la Temeke na baadae kuingizwa katika akaunti ya mtu binafsi Na.41401600207 ya NMB Handeni yenye jina la Mhina Masoud Omary.

Mbali na uwepo wa Zuio la kisheria lililotolewa na Mahakama Kuu mwaka Jana Tarehe 31/3/2017. Jaji Francis Mutungi, Msajili wa vyama vya siasa Nchini akishirikiana na Lipumba wakapanga njama za kutoa fedha hizo kupitia akaunti ya kificho ambayo baadae ilikuja kugundulika.

Awali Tarehe 10/10/2016 Mutungi alimuandikia Barua Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif na kumjulisha kuwa amesitisha kutoa fedha za Ruzuku kwa CUF kwa kile alichodai kuwa ni mgogoro wa uongozi uliopo ndani ya Chama. inaelezwa kuwa fedha hizo hutolewa kwa masharti maalumu ya Mgao kwenda kwa wale wote walioshiriki na kufanikisha kutolewa kwa fedha hizo na kila mmoja anapatiwa asilimia yake (Percent).
kama alivyokiri Msajiri wa Vyama vya Siasa Nchini katika Barua yake ya Kumb.Na.HA.322/362/14/17 ya tarehe 10/10/2016 ambayo nanukuu aya ya mwisho kama ifuatavyo;

"...Kwa kuwa fedha za ruzuku ni FEDHA ZA UMMA AMBAZO ZINAHITAJI USIMAMIZI MZURI KATIKA MATUMIZI YAKE, na kwa kuwa ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ina dhamana ya kugawa fedha za ruzuku kwa Vyama vya Siasa vinavyostahili na kusimamia uwajibikaji katika matumizi ya fedha hizo, hivyo baada ya tafakuri ya KINA NIMEONA NI BUSARA KWANZA KUSIMAMISHA KWA MUDA MGAO WA RUZUKU KWA CHAMA CHENU MPAKA HAPO CHAMA CHENU KITAKAPOREJEA KATIKA HALI SHWARI KIUTENDAJI INAYOWEZESHA VIONGOZI HUSIKA KUSIMAMIA MATUMIZI YA FEDHA HIZO IPASAVYO.”…mwisho wa kunukuu.

Katibu Mkuu, Maalim Seif akiwa ndiye Muwajibikaji Mkuu wa masuala yote ya fedha ndani ya CUF kwa mujibu wa KAtiba ya CUF hakuwahi tena kupokea barua nyingine kutoka kwa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini inayoelekeza kuanza kutolewa kwa fedha za Ruzuku ya Chama cha CUF.

Mara kadhaa Katibu Mkuu, Maalim Seif amekuwa akimuandikia Jaji Mutungi na kumuonya juu ya utoaji wa fedha hizo kwa bahati mbaya kwa hila na Ufisadi aliokwisha uonja ameziba masikio na kuendelea na hujuma hizo dhidi ya CUF na hapa nanukuu maelezo ya Maalim Seif;

“Kwamba kwa uelewa wetu amri ya mahakama ya kuzuia ruzuku kutolewa ilikusudia kuzilinda fedha za umma zisifanyiwe ubadhilifu wakati ufumbuzi wa kisheria suala hilo unashughulikiwa na mahakama. Zuio hilo mpaka sasa ni HAI. Tunataraji ulinzi huo wa fedha za umma utafanywa na taasisi zenu pia hadi hapo mashauri yaliyopo mahakamani yatakapopatiwa ufumbuzi. Mahakama ndiyo yenye dhamana, mamlaka na kauli ya mwisho ya utoaji haki Tanzania kwa mujibu wa Ibara ya 107A(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Ni matarajio yangu na Chama Chetu kuwa mtazingatia taarifa hii, na maombi yetu mtayapa uzito unaostahiki.”

Aidha, Tarehe 29 January, 2017 BODI YA WADHAMINI YA THE CIVIC UNITED FRONT (CUF – CHAMA CHA WANANCHI) KUFUATIA KIKAO CHAKE KILICHOFANYIKA siku hiyo kilitoa tamko na kumuandikia Msajili na mamlaka zingine za kiserikali akiwemo Gavana wa Benki Kuu, Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha-Hazina, Mkurugenzi mtendaji, National Microfinance Bank (NMB), Makao Makuu, Dar es salaam. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG), nk kuwajulisha ukiukwaji huu wa sheria na taratibu za fedha za umma.

Kutokana na hali hiyo ya mkanganyiko wa hesabu za fedha, Lipumba ameshindwa kuandaa hata taarifa ya Kufoji na kuiwasilisha kwa Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG), Prof. Mussa Assad amesema aliyasema hayo hivi karibuni wakati anakabidhi ripoti ya Ukaguzi wa hesabu za Serikali kwa kukitaja Chama Cha CUF kuwa kimeshindwa kuwasilisha taarifa ya Hesabu za Fedha wanazopatiwa na Serikali kutokana na Ruzuku.

Hivi karibuni bila aibu imebainika kuwa Jaji Mutungi na Lipumba wameshirikiana KUGHUSHI NYARAKA MBALIMBALI ILI KUHALALISHA UTOAJI WA FEDHA HIZO LAKINI WAMESHINDWA KUTOA HESABU ZA MATUMIZI YAKE.

Jumanne Tarehe 10/4/2018 Naibu Katibu Mkuu Joran Bashange amepokea majibu ya kisheria (Counter Affidavit) katika shauri jipya la RITA lililofunguliwa na Mhe Shaweji Mketo na Juma Nkumbi na kugundulika kuwa Saini zote za Wajumbe wanaoitwa wa Bodi ya Wadhamini ya Lipumba zikiwa zimefojiwa –KUGHUSHI, zikionekana zimesainiwa na mtu mmoja kupitia Wakili wao Mashaka Ngole. Huu ndio uadilifu wa Lipumba na Genge lake.
MSIMAMO WA KISHERIA JUU YA SUALA HILI:

kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa, Sura 258 ya Sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Political Parties Act, Cap 258) na Katiba ya CUF ya 1992 (Toleo la 2014). Inaeleza wazi kuwa, kila chama cha siasa chenye usajili wa kudumu kinapaswa kuunda Bodi ya Wadhamini ambayo ndiyo inayokuwa mmiliki na msimamizi wa mali zote za chama cha siasa husika. Kifungu cha 21 cha Sheria ya Vyama vya Siasa kinalieleza hilo kama ifuatavyo:

“21. —(1) Every political party which has obtained a certificate of full registration shall appoint a board of trustees to manage the properties and any business or investment of the party.”

CUF-Chama cha Wananchi kilitimiza masharti hayo ya kisheria kwa kuunda Bodi ya Wadhamini, na Katiba ya Chama ya 1992 (Toleo la 2014), Ibara ya 98 ikafafanua zaidi namna inavyopatikana, pamoja na nguvu na uwezo wake kichama, kama ifuatavyo:

“98(3) Bodi ya Wadhamini itakuwa ndiyo mdhamini pekee wa fedha na mali za Chama pamoja na madeni na itafanya shughuli zake kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa na sheria ya nchi inayohusu Wadhamini.

98(4) Bodi inaweza kushitaki au kushitakiwa kwa niaba ya Chama”.

kifungu cha 15(1) na 15(2) cha sheria ya Vyama vya Siasa
sura 258 (Political Parties Act, Cap 258) imeweka sharti kwa kila chama cha siasa kupitia kwa Bodi yake ya Wadhamini kufungua akaunti ya benki ambapo fedha zote zinazopokelewa na chama hicho kwa mujibu wa kifungu cha 13 cha sheria hiyo zitawekwa humo na chama kisicho na akaunti iliyofunguliwa na Bodi ya Wadhamini hakitapewa fedha za ruzuku. Kifungu hicho kinaeleza ifuatavyo:

“15-(1) Every political party which has been fully registered shall, through its trustees, maintain a bank account of the party in which all the money received by the party in accordance with section 13, shall be deposited.
(2) Any subvention from the government which is payable to any political party under this Act shall not be paid to any political party which does not maintain a bank account in accordance with this section.”

Ni wazi akaunti za benki (Na.2072300456 ya NMB tawi la Temeke na Na.41401600207 ya NMB tawi la Handeni) inayotumika kutekeleza wizi wa fedha za Ruzuku ya CUF haikidhi vifungu vya 13 na 15 vya sheria ya Vyama vya Siasa sura 258 na vinaondoa dhana ya uwepo wa mamlaka zinazoshughulikia masuala ya fedha ndani ya Chama kwa mujibu wa Katiba ya 1992 (Toleo la 2014) ambazo ni Bodi ya Wadhamini, Katibu Mkuu, Kamati ya Utendaji ya Taifa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa.

Inashangaza sana kuona mtu mwenye hadhi na sifa ya kuwa Jaji wa MAHAKAMA KUU ambae ni Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi; akiwa mtumishi wa umma, kukiuka maadili ya kazi yake, na kushiriki wizi wa wazi wa fedha za umma huku akifahamu kuwa alimwandikia Katibu Mkuu wa CUF-Chama cha Wananchi; ambaye, kwa mujibu wa Katiba ya CUF ya mwaka 1992 (Toleo la 2014) kifungu cha 93(i) ndiye mwajibikaji mkuu wa mambo yote ya fedha na mali za Chama katika ngazi ya Taifa (Chief Accounting Officer).

Maharagande,
April 14, 2018

maharagande@gmail.com
Tigo-0715 062 577, Voda -0767 062 577
 
Mungu hajaribiwa walianza kwa mbwembwe nyingi kuivuruga caf sasa hawana milango yakupenyezea aibu zimewajaa
 
Katika tasnia ya siasa awamu ya tano imefeli kabisa

Hakuna uwajibikaji ila ubabaishaji

Hakuna utawala wa sheria

Hakuna utawala bora wala haki

Niuhuni kuanzia juu kupitia kila mhimili

Tunadharaulika sana kwasasa watanzania

Heshima yetu imetoweka duniani kote.....uoza wa awamu ya tano.
 
Nawahakikishieni 100%
JIWE akitoka Ikulu, kuna Watumishi wa Umma wenye dhamana kwa sasa, wataozea jela.

Ni vyema Mtumishi wa Umma akazingatia Sheria, Taratibu na Kanuni husika.

Wakati huo, JIWE atakuwa Chattle akilindwa na katiba hii yenye viraka vingi.
Wakati huo nchi inaongozwa na chadema au?!
 
Mbona Huongelei Ripoti ya CAG na Chadema?
Unaogopa Maboss wako..
Mnapotosha ripoti ya CAG kuhusu Chadema kwa malengo ya kishamba sana , Chadema imepeleka kila kitu kwa uwazi kabisa kwa CAG , Ndio maana ameandika aliyoandika kwa tafsiri yake , HAWA AKINA MUTUNGI NA LIPUMBA BAADA YA KUGAWANA HELA YA CUF hawakuandika popote , Maana wameiba hela isiyo yao , Zipo taarifa kwamba Mutungi anashirikiana na Lipumba na Malima kuiba hela ya cuf na anapewa mgao wake , baada ya uchunguzi wetu kukamilika tutaweka namba ya A/C inayowekwa mgao wa Mutungi
 
Taarifa ya ukaguzi ya CAG inahusu mwaka wa fedha wa July 2016 to June 2017. Kipindi hicho afisa mhasibu wa CUF alikuwa maalim Seif. Hizo fedha za ruzuku zilizopokelewa na CUF- Lipumba taarifa ya ukaguzi wa CAG itatolewa bungeni April 2019 ikihusu mahesabu ya mwaka wa fedha wa kianzia July 2017 hadi June 2018. Hivyo msitake kudanganya wananchi. Hesabu za CUF-Lipumba bado hazijakaguliwa na CAG kwani hata mwaka haujaisha hivyo bado hesabu za mwaka hazijafungwa. Hesabu hufungwa tarehe 30 June na ndipo huwa tayari kwa ukaguzi wa CAG.
 
Back
Top Bottom