Lipumba: CHADEMA malizeni mgogoro

Eberhard

JF-Expert Member
Dec 20, 2010
1,070
2,000Dar es Salaam. Profesa Ibrahimu Lipumba amesema mgogoro uliopo ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ukiachwa uendelee unaweza kuathiri jitihada za vyama vya upinzani kutetea mchakato wa wazi wa Katiba Mpya.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam Profesa Lipumba ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF),alisema wameanza kufanya jitihada za kukutana na viongozi wa juu wa Chadema na kuzungumza nao ili waweze kutafutia mgogoro huo ufumbuzi wa haraka.

"Umoja wetu ni kutaka mchakato wa katiba uwe wa wazi, sasa huu mgogoro wa Chadema unaweza kutukwamisha, na kwa kutambua hilo tayari tumeanza kufanya mazungumzo na baadhi ya viongozi ingawa hayakuwa mazungumzo rasmi lakini tupo kwenye jitihada hizo," alisema Profesa Lipumba.

Aliyazungumza hayo baada ya kuulizwa na waandishi wa habari alipokuwa akitangaza maazimio ya kikao cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la CUF, ambapo alisisitiza kuwa hata hivyo wameshapanga kukutana ana kwa ana na viongozi wa Chadema kwa mazungumzo zaidi katika kuutatua mgogoro huo.

Alisema Baraza Kuu la CUF limetoa wito wa kuwepo kwa mkutano wa wadau hususan vyama vya siasa na asasi za kiraia kujadili rasmi ya mwisho ya katiba kwa lengo la kufikisha maridhiano ya mambo muhimu yaliyomo ndani ya katiba.

Profesa Lipumba alisema hatua hiyo inalenga katika kurahisisha kazi za Bunge la katiba kufikia mwafaka kuhusu vipengele muhimu vya Katiba Mpya.

Mgogoro wa Chadema unatokana na uamuzi wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kumvua madaraka aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo ya kusaliti chama.

Katika hatua nyingine Baraza Kuu la CUF limemtaka Waziri Mkuu Mizengo Pinda ajiuzulu au Rais amfukuze kazi, wakidai kuwa anahusika na matokeo ya vitendo vya ukatili vilivyotokea katika Operesheni Tokomeza Ujangili. "Baraza Kuu linamtaka Waziri Mkuu kuwajibika kutokana na matokeo ya operesheni hiyo."

Source: Gazeti la Mwananchi
 

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,491
2,000
Mnafiki mkubwa huyu.Anaongea bila hata kumbukumbu.Anamjua Hamad Rashid huyu??

Unafiki ni kitu kibaya sana!
 

Ulukolokwitanga

JF-Expert Member
Sep 18, 2010
8,403
2,000
Ametumwa na Kikwete kubembeleza CDM imsamehe Zitto ili aendelee kutumukia CCM akiwa ndani ya CDM. Kamati kuu ya CDM ikae haraka na kumvua uanachama huyu msaliti kabla hizi suluhu za kinafiki hazijaanza. Mbona wai hawajamalizana na Hamad Rashid kabakia mbunge WA mahakama, then wanataka kusuluhisha kwa jirani.

After all hatujasahau zile kura Lipumba ulizomgawia Kikwete 2010 kwa vile Ni muislam mwenzio kama ulivyonukuliwa ukisema
 

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,491
2,000
CUF walimfukuza Hamad Rashid kama Mbwa bila hata kumpa nafasi ya kujitetea.Kwao CUF wanadhani ndiyo wana Katiba na Chadema hawana Katiba ujinga mtupu!
 

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,491
2,000
Kwa mara ya kwanza nitatangaza mgogoro mkubwa na Viongozi wakuu wa Chadema endapo kama watasigina Katiba ya Chadema na kuruhusu kuongozwa na Akili ndogo ya watu mfano wa Lipumba.

Lipumba ambaye chama chake kimeungana na CCM kuunda serikali hana hadhi yoyote kusemea Chadema!
 

Yericko Nyerere

Verified Member
Dec 22, 2010
16,801
2,000
Lipumbu ni mzandiki, Chadema kutekeleza katiba yake ni mgogoro? Hamad Rashid alipofukuzwa CUF ulikuwa ni mgogoro?

Nani alikwenda kuwasuluhisha?

Huyu ccm ishamharibu
 

DianaY

Member
Sep 3, 2012
14
0
Mume akivurugwa mke hawezi kuwa na raha sasa ccm inaumizwa na uamuzi wa cdm mnategemea cuf wanaamani lazima atafute suluhisho amani irejee ndoa yao idumu
 

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,491
2,000
Lipumbu ni mzandiki, Chadema kutekeleza katiba yake ni mgogoro? Hamad Rashid alipofukuzwa CUF ulikuwa ni mgogoro?

Nani alikwenda kuwasuluhisha?

Huyu ccm ishamharibu

Isitoshe tumesikia CUF na CCM ndiyo walimuandalia mkutano kule Kigoma.Kwa hiyo wanajua wanachokifanya.

Eti amezungumza na viongozi wakuu Chadema.Anadhani Chadema ni kama Kokoro kwamba Mbowe au Slaa akishasema imetosha.Hajui Chadema inaongozwa na Katiba yake.Poor Him!
 

Bocho

JF-Expert Member
Jan 6, 2013
1,489
1,195
CUF walimfukuza Hamad Rashid kama Mbwa bila hata kumpa nafasi ya kujitetea.Kwao CUF wanadhani ndiyo wana Katiba na Chadema hawana Katiba ujinga mtupu!

Wewe ni mtu mzima uongo hautakusaidia bhana! Hamada Rashid alipelekewa barua kabla hata ya kikao kilichomvua uanachama. Hata hivyo hatua ya kumvua uanachama ni baada hata ya mbinu nyingine za kumsihi arudi kwenye mstari kushindikana. Au umeshasau kuwa alisema hakitambui kika kilichomuita akajielezee?

Kinyume na Zitto, mlishtukiza ajieleze hapo hapo na uamuzi ukatolewa papo hapo. Issue ya Hamad na Zitto ni tofauti.
 

AdvocateFi

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
11,511
2,000
Hakika nasema endapo CHADEMA mtamsamehe huyu mnafiki zitto kwa sikiliza kauli za wachumia tumbo kama lipumba basi itabidi tugawane mbao za mtumbwi tunaosafiria, Duniani kote inajulikana kwamba "HAKUNA MJADALA NA WANAFIKI NA WAHAINI" hata kama ni Mbowe au Dr.Slaa ndio mnaomlinda Zitto basi hakika hii dhambi itawatafuna milele.
 

Matola

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
41,198
2,000
Hivi Chadema wanasubili nini kumfukuza huyu jinga Zitto ili abakie kuwa mbunge wa mahakama tu?
 

Kajunjumele BA

JF-Expert Member
Jan 3, 2012
673
195
Ametumwa na Kikwete kubembeleza CDM imsamehe Zitto ili aendelee kutumukia CCM akiwa ndani ya CDM. Kamati kuu ya CDM ikae haraka na kumvua uanachama huyu msaliti kabla hizi suluhu za kinafiki hazijaanza. Mbona wai hawajamalizana na Hamad Rashid kabakia mbunge WA mahakama, then wanataka kusuluhisha kwa jirani.

After all hatujasahau zile kura Lipumba ulizomgawia Kikwete 2010 kwa vile Ni muislam mwenzio kama ulivyonukuliwa ukisema

Mkuu Ulokolokwitanga; Miminadhani kuumaliza Mgogoro hakuna maana ya kuridhiana na msaliti kauli waliyotumia ni ya jumla tu hivyo tumpe benefit of doubt Profesa Lipumba.Mimi ninachosema ni kweli Kamti kuu ichukue hatua za haraka kwasababu huyu msaliti badala ya kutulia na kutumia muda huu katika kuboresha uhusiano na viongozi wake anaendelea kutumia jukwaa la chama kuwa nanga viongozi na kuvuruga umoja kwa wanachama ,awajibishwe haraka hakuna haja ya kusubiri muda huyu ni Kansa na anatakiwa akatwe mara moja toka kwenye mwili wa chama.
 

Kilaga

JF-Expert Member
Feb 23, 2013
2,148
2,000
Watu mna hasira kweli!!!

Kesho watakuwa wasaliti wao, kila mtu ni msaliti kwa wakati wake. Haohao walisaliti NCCR, na baadae TLP, leo wanajiona waungwana. Aliyezoea kula nyama ya mtu haachi, na siasa za Tanzania ni za usaliti na kusalitiana,. Hao wapigao kelele wote siyo wanasiasa bali wapiga debe wa wanasiasa..
 

casampeda

JF-Expert Member
Jul 28, 2012
2,800
1,500
Wewe ni mtu mzima uongo hautakusaidia bhana! Hamada Rashid alipelekewa barua kabla hata ya kikao kilichomvua uanachama. Hata hivyo hatua ya kumvua uanachama ni baada hata ya mbinu nyingine za kumsihi arudi kwenye mstari kushindikana. Au umeshasau kuwa alisema hakitambui kika kilichomuita akajielezee?

Kinyume na Zitto, mlishtukiza ajieleze hapo hapo na uamuzi ukatolewa papo hapo. Issue ya Hamad na Zitto ni tofauti.

Si wamfukuze wanasubiri nini??? Wachagga ban!!,hamuwezi kuchukuwa Dola kutegemea kanda moja.Mboe kajitahidi sasa akae pembeni,Zitto akunaga!!mtabana mtaachia.Chupi kimewabana,mumelikoroga wenyewe na lazima mulinywe wenyewe kudadadeki!!!! sisi kazi yetu kuchochea kuni kavu kwenye mafiga,Lisu anazidi kuwa mfupi tu,anakula pesa za kesi na aziishi Mahakamani,Ruzuku inaraha yake bana!!! wanajua watu 3 tu,na wapo tayari kuukosa Urais lkn sio uongozi wa chama,ila wanauwakika kuongeza Wabunge na ruzuku.
 

Kudadeki

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
859
0
CUF walimfukuza Hamad Rashid kama Mbwa bila hata kumpa nafasi ya kujitetea.Kwao CUF wanadhani ndiyo wana Katiba na Chadema hawana Katiba ujinga mtupu!

Nafikiri wewe ndiyo mnafiki na muongo wa kiwango cha juu. Hamad Rashid hakutaka hata kuhudhuria mikutano aliyokuwa anaitwa badala yake alikimbilia mahakamani kutaka mahakama ibatilishe hiyo mikutano. Nenda kasome vizuri kabla ya kukurupuka kuandika mapupu yako.
 

jogi

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
25,615
2,000
Lip lip,
le profeseri, hivi yeye hafugi ng'ombe wa kisasa!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom