jingalao
JF-Expert Member
- Oct 12, 2011
- 36,155
- 29,677
Alichokifanya lipumba wakati wa uchaguzi kilikuwa ni kitu sahihi na kinachotakiwa kufanywa kwa wakati ule.
Lipumba aliamua kukataa kulamba matapishi yake...lakini pia aliipenda sana CUF kwa hiyo hakuamua kuiacha kwa maana ya kujitoa kuwa mwanachama.
Lipumba alitaka kuwaonesha CUF wenzake waliodanganyika kuwa maamuzi yao sio sahihi...lakini aliyaheshimu na akaamua asiwe kikwazo kwenye maamuzi hayo ya Chama.
Lipumba alitaka kuwaonesha CUF kuwa njia waliyopita haikuwa sahihi na haikuwa na tija kwa ustawi wa chama na hivyo kama mwenyekiti asingekubali kuona chama kinazama chini ya usimamizi wake.
Lipumba aliwaachia watoto wachezee wembe ...sasa umewakata na wamejifunza na ameamua kurudi na kuwaponya.
Lipumba na profesa na mstaarabu sana na anastahili nafasi nyingine.
Wasiostahili ni wale waliokubali kuukumbatia usanii na ufisadi uliokumbatiwa na UKAWA iliyoingia kwenye uchaguzi huku ikiwa imeachana na misingi ya ki-UKAWA.