Lion King

Kabinti ka ludilo

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2014
Posts
409
Reaction score
468
Basi aliondokea Mfalme Simba mtawala wa tano Umofia aliekuwa Hodari kweli kweli.

Basi katika mkoa wa kijani aliweka fedha nyingi akajenga meli kubwa, nayo ilikuwa kwa Lengo la kuabili abilia na mizigo

Basi fundi wa meli hiyo ya mabilioni alitengeneza meli kwa ustadi kweli kweli maana mfalme simba wakati huo alipenda uchapakazi. Basi Bwana fundi yule aliitwa na "wenye nchi" siku moja, nao wakamwambia awe makini katika kazi hiyo kwani wao ndio "wenye nchi" na mfalme simba hana chochote. Wakamwambia meli hiyo itaathiri sana mzunguko wa magari yao kwani itaondoa uhitaji wa magari mengi kwenda msumbiji na Malawi. Aliambiwa asitishe utengenezaji wa meli. Basi bwana fundi akasema yeye anamuogopa mfalme simba hivyo atatengeneza ila anajua cha kufanya ili asiwaangushe "wenye nchi".

Basi Bwanafundi alitengeneza Meli na kwenye injini akaweka "lipalata"

Basi Meli ikawaka ikawa furaha kwa mfalme simba akaanza kuwaza kuweka bandari kavu katika mji wa Pwani mkoa wa kijani. Meli ikaabili siku tatu ikazima majini ikiwa na watu 300. Basi ikawa hofu kwa watendaji wa mfalme simba Bahati nzuri nahodha hodari aliikomboa meli hiyo.

Basi akaja yule waziri wa kutoka kanda maalumu, aliyehama upinzani kwenda Tawala. Naye akakuta Meli imezima. Akamtisha Bwanafundi kuwa atoe siri ya Meli hiyo. Akatoa maneno ya ukali sana. Basi bwanafundi alihofu kuzungumzia habari ya "lipalata" akaanguka kitandani akafa usiku wa manane.

Basi hazikupita siku nyingi yule mfalme simba alianguka kwenye kiti cha utawala na mamlaka yake walichukua "wenye nchi". Basi yule Bwana waziri wa kanda maalumu ilikuwa ni taget namba moja aliondolewa ofisini na mamlaka yake kutupiwa mbali.

Hadithi ya Mameli haya makubwa iliishia hapo. Hatimaye meli hii iliungana na meli nyingine mbili kubwa nazo zimetia nanga zinaendelea na uzalishaji wa samaki.

Nao wenye nchi wakakipiga chapa kitabu cha masimulizi ya Meli hiyo kuwa ole wake atakaethubutu kuwasha meli hizo na kufungua kitabu hicho chanye siri ya "lipalata"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…