Linipate la kunipata!

Linipate la kunipata!

Hello! Ushawahi sikia mtu anaenda makuburini anaomba akiwa na imani kuwa atafanikiwa? Kwa upande wangu kipindi nipo darasa la nne kuna kaburi lilisadikika kuwa ni la mtakatifu watu wengi walikuwa wanaenda kusali pale kwaajili ya kutatuliwa matatizo yao,ukiomba unafanikiwa malengo yako kupitia ilo kaburi .kama ni mwanafunzi na upo kwenye kipindi cha mitihani basi unaweza kwenda kwenye kaburi ilo unasali,unachukua udongo unamimina kwenye pen zilikuwa zinaitwa cello,ivyo unaandika huku udongo upo ndani ya pen.siku moja tukashauriana na rafiki angu kwenda kwenye kaburi Ilo tujionee miujiza iyo sio kusikia tu kwa jirani ilikuwa miaka ya 2000, Basi tukaenda tulipofika pale tukasari tukaweka karanga mifuko miwili juu ya kaburi maana ndo kitu ambacho tulikuwanacho mkononi.
Lakini hata sisi kabla hatujasali nakuweka zile Karanga tulikuta ela juu ya lile kaburi, kwakweli hatukuziacha. Inaonekana kuna mtu alifanya dua zake akaweka ela. Kwakweli kaburi hilo liliheshimika sana japo sijaendelea kulifatilia sana kwa siku za karibuni.

Sasa mdogo wangu yupo darasa la saba anamaliza mwaka huu analala na udongo ndani, mwingi tu katia kwenye kopo alichukua kwenye ilo kaburi na mwingine uwa analamba! Nikamshirikisha mama nikamwambia dogo analala na udongo ndani wa makaburini na mwingine analamba, mama akawa mkali akaniambia muache kila mtu na imani yake!

Basi mimi ule udongo nikaendelea kuuacha kwenye chumba chake lakini mimi bwana msomi siwezi endelea kuona icho kitu kikiwepo ndani,Mimi niliutumia lakini dogo anapitiliza hadi analamba jamani!!!! Mimi na rafiki angu tulifaulu vizuri tu though hatujui kama sababu ni kusali kwenye lile kaburi.... Kwakweli nimemwaga kimya kimya, nimeegesha kifaa alichokuwa akiwekea udongo huo wa makaburini. Nasemaje "liwalo na liwe, la kunipata linipate Mungu anisamehe kama nimekosea".
Mkataze aisee asije maliza huo udongo
 

au ni Sexless ?
Hapana.
 
kwa kweli mimi huwa nakwenda kusali na kuomba kwenye makaburi ya wazazi wangu naweza kukaa hata nusu saa hapo
makaburi mengine nikipitaga kama mkristu nawasalia tu ile roho za marehemu ziendelee kupumzika kwa amani nafanya na ishara ya msalaba basi napita zangu.
Ila binafsi sipendelei kabisa kupita au kwenda makaburini labda iwe kwa minajili ya kuzika
 
kwa kweli mimi huwa nakwenda kusali na kuomba kwenye makaburi ya wazazi wangu naweza kukaa hata nusu saa hapo
makaburi mengine nikipitaga kama mkristu nawasalia tu ile roho za marehemu ziendelee kupumzika kwa amani nafanya na ishara ya msalaba basi napita zangu.
Ila binafsi sipendelei kabisa kupita au kwenda makaburini labda iwe kwa minajili ya kuzika
Anaye ombwa ni Mungu sio makaburi mtu akifa ndio ameshakufa hawezi kukusaidia

Siku nyingine usirudie kufanya hayo
 
Back
Top Bottom