Lini Tundu Lissu ataacha kutafuta sifa na kuwa Mzalendo wa kweli?

idawa

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
25,282
38,359
Ni baada ya kuomba Mwongozo kuhusu swala lililoleta utata kwa siku kadha kuhusu uhalali wa serikali kuwasilisha mpango wa mwaka mmoja badala ya miaka mitano.

Awali akiomba Mwongozo mh.Lissu alisema serikali imekiuka kuleta mpango wa mwaka mmoja badala ya miaka mitano ambayo ndio desturi ya mabunge yote yaliyopita na kumtaka Spika kutokubali kuruhusu bunge lake tukufu kukiuka kanuni zake kwa faida ya serikali. Huku akiendelea na kibwagizo cha hapa kazi tu hapa kazi tu.

Kwa kukazia ndipo akasimama Mh.Zitto na kuikumbusha serikali kuwa serikali ilikuwa na uwezo kuwasilisha hoja ili kanuni zitenguliwe na mpango wa mwaka moja ujadiliwe na kanuni zinaruhusu utenguaji huo.

Ndipo aliposimama Waziri na kusema kuhusu suala la utenguaji wa kanuni serikali ilishakaa na kamati ya kanuni ambapo kiongozi wa KUB alishiriki kwa kutuma mwakilishi, na Mwakilishi mwenyewe alikuwa Lissu.

Waziri akasema anamshangaa Lissu kwa kuomba mwongozo jambo ambalo alishiriki kutoa maamuzi na akasema anaweza kutaja hata majina ya wajumbe wote walioshiriki huo uamuzi.

NB. Wabunge waache unafiki na kuwa vigeugeu kwa kutafuta umaarufu usio na tija.
 
Mbona spika alikataa kumpa Lissu nafasi pale pale ya kujibu hoja hiyo ya waziri?Alihofia nini?
 
Kaumbuliwaje?

Spika mwenyewe ni M/Kiti wa kamati ya Uongozi kwahiyo kama ni kweli kuwa kikao kiliketi na Lissu alikuwepo sidhani kama angeruhusu mjadala!

Na kama ni kweli walikaa na alikuwepo kwenye kikao si lazima akubaliane na maamuzi ya kikao!

Kwahiyo acha kushabikia mambo uliyoyasikia toka kwa third part, utaonekana kilaza!
 
dah unafiki m baya sa hapo ni wapi kaumbuka ... mbona unaandika ka mwanamke Wa uswahilini kupenda kusutana
 
Mkuu mbona sioni sehemu aliyoumbuliwa? Zaidi ya kutaka taratibu zifuatwe?

Mkuu hujagundua kuwa serikali ilishafuata taratibu kwa kukaa na kamati ya kanuni za bunge ambapo kimantiki Kiongozi wa Upinzani bungeni hushiriki, lakini kiongozi wa KUB akatuma mwakilishi ambaye ni Lissu na walishakubaliana kuhusu utenguaji wa kanuni ili mpango wa mwaka mmoja uweze kujadiliwa.

Kwa nini Lisu aliomba Mwongozo kwa jambo ambalo kimantiki alishiriki maamuzi yake, inamaana hakuwaambia ukweli wabunge wa upinzani kuhusu makubaliano yaliyofikiwa kwa pamoja na serikali kuhusu utata huo.

Ndio maana Waziri alimshangaa Lissu kwa kuomba Mwongozo jambo ambalo walishakubaliana ambapo ilibidi Waziri atolee ufafanuzi tu



Hapo ameumbuliwa wapi???
 
Kaumbuliwaje?

Spika mwenyewe ni M/Kiti wa kamati ya Uongozi kwahiyo kama ni kweli kuwa kikao kiliketi na Lissu alikuwepo sidhani kama angeruhusu mjadala!

Na kama ni kweli walikaa na alikuwepo kwenye kikao si lazima akubaliane na maamuzi ya kikao!

Kwahiyo acha kushabikia mambo uliyoyasikia toka kwa third part, utaonekana kilaza!

Sasa mbona hakukanusha kwamba hakukubaliana na maamuzi ya kikao pale Waziri alipotolea ufafanuzi kuhusu ushiriki wake na maamuzi ya pamoja.
 
Back
Top Bottom