Mkoa wa Manyara ulioanzishwa mwaka 2002 makao yake makuu yapo mjini Babati. Mkoa huu una umri wa miaka takribani 14 sasa kuanzishwa kwake. Serikali imejitahidi kuunganisha mkoa huu na mikoa ya Arusha na Singida kwa barabara ya lami. Pia ujenzi wa barabara ya Babati - Kondoa - Dodoma unaendelea. Bado mkoa hauna uwanja wa ndege. Ni lini mkoa huu utajengewa uwanja wa ndege? au hakuna umuhimu wa uwanja wa ndege?