Lini Frederick Sumaye amejiunga na CHADEMA?

Huyo mwanajeshi ni muhimu sana atujuze namna ya kuikabili green coler
 
Wewe unaishi dunia gani? Mbona alishapewa kadi kwenye mkutano Wa hadhara Arusha? Fanya research kabla ya kutokwa mapovu hapa
 
ondoa neno chetu wewe ni wa lumumba,
 
Hoja yako ni nzuri maana yawezekana hukuwahi kusikia kuwa sumaye amejiunga na chama cha siasa baada ya kutoka ccm ila ulichokosea kabisa umeambatanisha na Mipasho kwenye hoja au swali lako hili...ila nashukuru watu wamekujibu lini sumaye amekabidhiwa kadi ya chadema...
 
aziri mkuu wa awamu ya tatu Mh.Fredirick
Sumaye amtangaza rasmi kujiunga na chama
cha Demokrasia na maendeleo Chadema na
amekabidhiwa kadi na Mwenyekiti wa chama
hicho Mh.Freeman Mbowe.
Sumaye ambaye wakati wa uchaguzi alitangaza
kujiondoa CCM na kudai kuwa anaunga mkono
mageuzi yanayofanywa na vyama vinavyounda
katiba ya wananchi (UKAWA) bila kuweka
wazi kuwa yuko kwenye chama kipi kati ya
hivyo amesema asa ameamua kujiunga na
CHADEMA.
Akizungumza katika mkutano wa kufunga
kampeni za ubunge wa jimbo la Arusha kwa
chama cha CHADEMA uliofanyika kata ya baraa
Sumaye amesema anataka kuungana na
wanamageuzi wenzake katika kuendeleza
harakati za mabadiliko hapa nchini ambazo bado
zinaendelea.
Akizungumza baada ya kumkabidhi kadi
Mwenyekiti wa chama hicho Mh.Freeman
Mbowe amesema chadema na vyama washirika
wa UKAWA bado viko imara na vimeendelea
kuimarika na kwamba licha ya kudhulumiwa
ushindi azma yaoya kuleta ukombozi nchini iko
pale pale.
Awali aliyekluwa mgombea uras wa CHADEMA
akiwakilisha vyama vya umoja wa katiba ya
wananchi ukawa Mh.Edward Lowassa
ameendelea kuwataka watanzania wanaounga
mkono mabadiliko kuwa watulivu na kwamba kwa
vile wana dhamira ya dhati ya kuyaona
mabadiliko hakuna kukata tamaa kwani bado
kuna fursa yakufikiwa kwa malengo yao .
� Sumaye atangaza rasmi kuwa
mwanachama wa Chadema.
4
 
Ulikuwa unaelekea kuwa na swali zuri japo swali lenyewe umeleta kwa sababu tu hufuatilii vyombo vya habari. Sumaye ni mwanachama wa Chadema. Umeharibu ulipoanza kuingiza mambo ya akina Haji Duni. Kama hadi leo hujui hata utaratibu uliotumika kwa Babu Duni kujiunga Chadema sidhani hata kama una deserve kuwa kwenye jukwaa hili!
 
Sumaye hivi sasa ameshakuwa mzoefu huko CDM, kadi alichukua muda mrefu tu baada ya uchaguzi mkuu.
 
Kwanza mlitupumbaza, kutulisha na kutukaririsha maneno wakati wa uchaguzi mwaka jana.watu tukahadaika mara tukakubali kubadili gia angani(zidumu fikra za mwenyekiti),mara mkatulisha maneno wamba dr slaa kahongwa an ccm,mara kaponzwa na mshumbushi n.k.na sasa mmemteua sumaye kuwa mjumbe wa halmshauri kuu.sasa nauliza hivi,ni kigezo gani kimetumika kumpa huo ujumbe??maana sumaye hana kadi ya chama chochote cha upinzani zaidi tu alisema amekuja kuongeza nguvu kwa lowasa,acheni kutufanya sisi mazezeta kiasi hicho,hizo habari za zidumu fikra za mwenyekiti na ufia chama inabidi zife
 
Kwanza mlitupumbaza, kutulisha na kutukaririsha maneno wakati wa uchaguzi mwaka jana watu tukahadaika mara tukakubali kubadili gia angani (zidumu fikra za mwenyekiti),mara mkatulisha maneno wamba Dr Slaa kahongwa na CCM,mara kaponzwa na mshumbushi n.k.na sasa mmemteua Sumaye kuwa mjumbe wa halmshauri kuu.

Sasa nauliza hivi, ni kigezo gani kimetumika kumpa huo ujumbe?Maana Sumaye hana kadi ya chama chochote cha upinzani zaidi tu alisema amekuja kuongeza nguvu kwa Lowassa, acheni kutufanya sisi mazezeta kiasi hicho,hizo habari za zidumu fikra za mwenyekiti na ufia chama inabidi zife.
 
Umedumaa akili hadi umesahau kuwa sumaye ni mwanachama wa CHADEMA, siyo (chadema)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…