MREKEBISHARIKA
Member
- Dec 4, 2006
- 18
- 33
Aliwahi kusema Mwalimu Nyerere kuwa ili maendeleo ya kweli yawezefikiwa moja ya vigezo vya kuzingatowa ni Siasa Safi na Uongozi bora.
Siasa safi niliyoielewa mimi ni pale panapokuwa na uhuru wa kufanya shughuli za kisiasa kwa maana ya kuwa wananchi wana uhuru wa kushiriki siasa kupitia vyama vyao na kwamba viongozi wa vyama hivyo wanasimamia maslahi mapana ya nchi ya vyama vyao na siasa kwa ujumla.
Hivi karibuni kuna vituko vimetokea na hivi ni vya kujiuliza wapi tunaelekea. Mwenyekiti wa CHADEMA alimpendekeza Aliyekuwa Fredrick Sumaye kuwa Mjumbe wa CC ya Chadema. Sio jambo baya lakini kwa sisi wana duru la siasa linatuachia Maswali mengi sana. Moja kubwa ni hili LINI SUMAYE AMEJIUNGA NA CHADEMA?
Katika mahojiano na Vyombo vya Habari mwezi wa 12 , 2015 Bwana Sumaye alikiri mwenyewe kuwa hajajiunga na Chama chochote cha siasa baada ya kutoka CCM. Isipokuwa moyoni mwake alieleza nia yake ya dhati ya kuona kuwa Ccm inasambaratika kwa kuwa sasa muda umefika.
Kwa fikira ndogo za mtu kama mimi nilidhani Chama kingejiridhisha kwamba juu ya Utayari wa mtu kama. Sumaye ambaye uenda anakwenda Chamani kutafuta ajira tu na sio kukisaidia chama. Ikumbukwe pia katika vikao vya uteuzi wa katibu mkuu wa Chama, mwenyekiti Mbowe aliwahi kutaka Sumaye awe katibu mkuu kabla jaribio lake hilo kushindikana na kuwa na jina la mtu ambaye hakuwa ameandaliwa na leo hii tunashuhudia chama kurudi ofisini tofauti na kilivyokuwa siku za nyuma.
Je hatujajifunza ya Mwalimu Juma Duni? Chadema kiliwahi kufanya jaribio katika kile kilitafsiriwa na wengi sisi kuwa jaribio la kuchukua nchi kwa hila. Walimchukia Lowasa toka CCM NA Duni toka CUF . Kilichoendelea kitoshe kuwa sehemu ya vituko. Babu Duni leo yuko CUF Karudi Chama chake na Lowasa anashinda barabarani tu akinunua mahindi na kuchekesha kuwa anakubalika wakati JPM anachanja mbuga na wananchi wanasoma Namba.
Turudi kwa Sumaye, Lini umejiunga na Chadema? Maana kwa umaarufu na umuhimu wako nilitaraji kusikia siku maalumu ya kupewa kadi ya Uanachama. Kwa maneno yako ulitwambia kuwa wewe hautojiunga na chama chochote. Au mwenyekiti Mbowe unaendelea na cinema zako zile.naomba kuwasilisha.