Linex ana kipaji, mbona hang'ai kama wengine?

mbotoki

JF-Expert Member
Jan 27, 2015
265
250
Wanajamvi, tumeweza kushuhudia hivi sasa ushindani mkali katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya, wasanii wengi wakijitahidi kufanya kila liwezekanalo, ili mradi aweze kusikika au kukubalika, wapo wengine wanafanya mpaka mambo yasiyofaa ili mradi tu tumsikie sikie.

Sasa ba ndugu kuna huyu kijana anaitwa Linex Sunday Mjeda.
ki ukweli kabisa jamaa anajua kuimba, nyimbo zake zote alizopata kutoa nadhani mtakubaliana na mimi kuwa ni vinanda. jamaa ana sauti nzuri sana kwa hakika. Style yake ya kuweka kilugha chao kidogo kwenye kila nyimbo nayo inanifanya nimuone mzalendo Zaidi.

kinachonishangaza mbali na sifa zoote hizi, jamaa sioni akipaa juu kama hawa wawili (Mnawajua) hapo ndio najiuliza haswa, tatizo la jamaa huyu liko wapi aisee?

Sioni jamaa akipata Show za maana, sioni akipata show za nje, sioni akivuma kwenye media mbali mbali, hata kwenye tuzo jamaa hatokei.
 

pwilo

JF-Expert Member
May 27, 2015
3,786
2,000
Amesema Hana mpango wa kwenda kimataifa na video kwa mwanachi kamaliza au aj
 

Mrs Van

JF-Expert Member
Mar 9, 2016
5,375
2,000
Anaimba saNa nyimbo za masikitiko. Hazinogi sana kny show coz soko la mziki limechange
 

Denis denny

JF-Expert Member
Oct 7, 2012
5,785
2,000
Huyu dawa yake hajaikoleza kama wenzie naona Waha wenzie hawajamshauri vizuri au yawezekana ni mbishi hataki kupuliza
 

Mlatinoh king

JF-Expert Member
Oct 14, 2015
5,568
2,000
bado ajaamua kujitanua kimawazo na kupata ushauri nin afanye ili aweze kutusua, tena ukifatilia vizur jamaa anaweza fanya mziki kama wa tekno wa nigeria, saut zao zinaendana kiaina.
 

Karne

JF-Expert Member
Jun 13, 2016
5,023
2,000
Binafsi nawasikitia wasanii walioficha "maziwa" yao kwa kisingizio kwamba Ruge atawanyonya matokeo yake maziwa yao yanawachachia maghettoni ilhali wanaonyonywa wanatusua daily.

Linex hana vision kama 20% tu sidhani hata kama wana managements za kueleweka maanake mziki wa leo ni connections na promo.

Belle 9 pia ni mkali lakini sijua hata kama ana passport.
 

Rutagwerera Sr

JF-Expert Member
Dec 21, 2011
2,467
2,000
Mtoto wa kishua yule hana njaa ya kumfanya aongeze juhudi plus ana toto ya kitasha ndo basi ashakunja nne. Afu mabange mengi pia upande mwngine.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom