Line za TTCL

Line za TTCL

Nazungumzia kibiashara, feature phones hazitumiki siku jizi? Ktk biashara ya mawasiliano asilimia kubwa ya subscribers wanatumia feature phones.
Jamaa wamefocus kwny data mkuu...features phone unaweka tigo mambo yanakwenda..
 
Hivi hizi simcards (chips) zinapatikanaje?
Zinatumika kwenye simu za kawaida au kuna simu maalum?
Naomba kujuzwa kwa mwenye ufahamu wa jambo hili
Mi nilienda mwanza nikanunua line yao. Sasa pale mjini ilikua inakamata fresh tu. Ila nikatoka mpaka nafika kona bwiru network hakuna kabisa. Ni km kama nne hivi kutoka town. Ile kurudi kwao, wakanambia mtandao upo hapo hapo mjini basi
 
Watawanyike kwa haraka mikoani,toka tumeanza kiwasikia na 4G,mikoani bado kabisa
 
mm nimenunua line ya 4g lkn ukiiweka kwenye simu ambayo haina internet(kama nokia ya tochi) haisomi kabisa.....inatumika kwenye smartphones tu
But its "4G" simcard right??? so unakwenda kuweka kwa simu ya tochi haki ya nani umevurugwa
 
mkuu
But its "4G" simcard right??? so unakwenda kuweka kwa simu ya tochi haki ya nani umevurugwa
mkuu mbona line za 3g mitandao mingine ukiweka kwenye nokia ya tochi inasoma?? naweka kwenye nokia ya tochi ili nitumie dakika na sms
 
TTCL ukitaka special namba ni bure , hakuna gharama yeyote ile. kuhusu huduma zao bado wanaendelea na ujenzi wa mawasiliano kwa kasi,Na lengo lao ni kuwafikia watanzania popote walipo nchini na wamesha tandaza Dar, Pwani,
Morogoro, Dodoma, Mbeya, Mwanza,Tanga na Zanzibar N.K jana na leo walikuwa na uzinduzi kule Tanga kunani, pamoja na Arusha ni kesho nasika wanazindua, kwa ujumla hawa jamaa wako vizuri.
- Simu yeyote yenye 3G au 4G unaweza kuweka line ya TTCL na inafanya kazi, tena wana ofa kibao ukiacha kupiga simu bure TTCL-TTCL mara uongezapo salio, si hivyo tu utapiga mitandao kwa bei ya 1.17 kwa sekunde.
- Kwa sasa wanajitahidi sana wana mawakala,na kwa yule wa mabibo hostel jitahidi utoke maeneo yako hapo barabarani au rahisi kwako ni ubungo plaza wana shop yao hapo,contact yao ni namba 100 huduma kwa wateja ni bure, ukiwa na simu ya TTCL na namba 0222100100 kwenye simu yeyote ile ila utachajiwa
- kujiunga kwenye vifurushi vya TTCL piga Code *148*30# au ingia kwy www.ttcl.co.tz na kwa maoni zaidi wana customercare@ttcl.co.tz
Mkuu hv ni kwanin kwenye simu nikichagua option ya lte/3g/2g line inasoma 4g lakini siezi piga wala pokea simu. Sms zinaingia na kutoka.. internet iko poa sana.
Nikichagua 3g/2g ndo kabisaa "no service". Na pia kwene modem ya 3g inasema "No service" but kwa miezi ilopita 3g ilikuwa inasoma.
Wamezengua baada ya "marekebisho" yao jpili ilopita. Niko maeneo ya SAUT mwanza
 
Mimi nipo morogoro naitaji chip ya ttcl nataka nitumie mkongo wa taifa
 
Back
Top Bottom