Line moja unayoona inafaa ni ya mtandao gani ?

Line moja unayoona inafaa ni ya mtandao gani ?

Kuna kutupa line zako zote ubaki na moja tu kwa ajili ya internet (Data ) , Message na mawasiliano mengine.
Utabaki na line gani ? Itakutoa ?
Mm nabaki na Airtel, mtandao wa kijanja sana.
Vifurushi safi kabisa muda wote na iko safi sana!
Ulianzishwa utaratibu ambao unatuwezesha line ya mtandao wowote kuibadili iwe ya mtandao mwingine unaoupenda, TCRA inatakiwa itoe ufafanuzi hasa baada ya usajiri mpya.
 
binafsi natumia haloteli na enjoy sana tu bila tatizo, kwaiyo kura yangu kwa halotel japo marafiki zangu na ndugu zangu wengi wana namba ya tigo
 
Mi naeza nkabaki na Tigo ila voda sitoitupa siku wakizinguwa narejea halotel wakitafuna mb zangu narejea home kisiwani zanzibar zantel nkiona mishe hazisomeki napanda boti narudi bara nachukua airtel si unajuwa mi Baharia
 
Kwa sasa hamna Kampuni/laini bora katika data kwa sababu zifuatazo
1.Vifurushi vinabadilika badilika hovyo
2.Uwezo wa kampuni kutoa masafa ya H+,3G na 4G ni wa kubahatisha na inategemea na mahali pia 'coverage' ni ndogo mfano; simu ina uwezo 4G ipo Dar,Dodoma nk ila muda mwingi simu inasoma 3G au H+ pia hayo masafa hayafiki kiwango cha juu cha utumaji na upakuaji wa mawimbi ya masafa(Uplink/Downlink) kwenye zile MBPS, wataalam wa IT/Computer Sc. nadhani watasaidia pale uwezo wangu ulipoishia..
 
Halotel ndio mtandao wa intaneti ninaouamini nimejaribu yote isipokuwa ttcl na zantel
 
Kuna kutupa line zako zote ubaki na moja tu kwa ajili ya internet (Data ) , Message na mawasiliano mengine.

Utabaki na line gani ? Itakutoa ?

Mm nabaki na Airtel, mtandao wa kijanja sana.

Vifurushi safi kabisa muda wote na iko safi sana!
Kiukweli artel hawajawahi ni angusha na huduma yao ya uni number 4
 
Back
Top Bottom