Lindi: Watu 34 mbaroni kwa kufanya fujo kabla na baada ya Uchaguzi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Polisi mkoani Lindi imewakamata watu zaidi ya 34 wanaodaiwa kuwa ni wanachama na wafuasi wa vyama vya upinzani kwa tuhuma za kuchoma nyumba, ofisi za serikali, magari na zahanati kabla ya Oktoba 28, mwaka huu na baada ya kutangazwa matokeo ya Uchaguzi Mkuu.

Mkuu wa Mkoa Lindi, Godfrey Zambi alisema kwa simu kuwa miongoni mwa magari yaliyochomwa ni ya mgombea udiwani Kata ya Liwale. Pia alisema watuhumiwa walichoma moto jengo la kata na jengo la Katibu wa CCM wa kata.

Zambi alisema uharibifu uliotokea katika mkoa huo ni mkubwa, na kwamba watuhumiwa wengi walikimbia. Alisema uhalifu ilitokea katika wilaya za Liwale, Nachingwea, Lindi na Kilwa.

Alisema tukio hilo lilitokea kati ya Oktoba 28 na 29, mwaka huu, na kwamba magari yalichomwa, mengine kupigwa mawe, nyumba zilichomwa ikiwemo ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Nachingwea.

Zambi alisema Liwale, watuhumiwa walichoma moto magari zaidi ya saba yakiwemo ya aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, Zuberi Kuchauka na gari la aliyegombea udiwani katika kata hiyo.

Aidha, alisema jengo la zahanati lilinusurika kubomolewa kwa kuwa askari waliwadhibiti watuhumiwa. Alisema Nachingwea watuhumiwa pia walichoma ofisi mbili za serikali za kata, wakichoma gari la Mwenyekiti wa halmashauri, nyumba, wakatishia kuchoma jengo la Mahakama, lakini walishindwa.

Alisema pia Nachingwea mmoja wa mgombea kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akiwa na watu 12 walikutwa wakiwa na vitambulisho 60 vya kupigia kura.

Alisema katika vurugu hizo, katika kata mbili yalitangazwa matokeo tofauti, huku akitangazwa mshindi kutoka upinzani wakati waliotoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) ndio walioshinda, na hiyo ilitokana na msimamizi wa uchaguzi kushikiwa visu wakati akitangaza matokeo.

Alisema gari la Katibu wa CCM wa Wilaya lilipigiwa mawe, watu wakiumizwa wakati Lindi Vijijini, jengo la maendeleo ya jamii lilichomwa moto, kuchoma jengo la kata na jengo la Katibu Kata wa CCM vikichomwa.

Kwa upande wa Kilwa Kivinje, alisema lipo eneo wahalifu walimwaga petroli wakitaka kuwasha jengo la kata lakini wananchi walimwaga mchanga kwa wingi kuzuia uharibifu huo. Awali, Zambi aliwaeleza waandishi wa habari mjini Lindi kuwa vurugu zilianza wakati wa kuhesabu kura na matokeo yalipotangazwa hali ilikuwa mbaya zaidi.

Alisema Jeshi la Polisi liliwakamata wafuasi wa CHADEMA nyumbani kwa mgombea wa chama hicho wakiwa na galoni za mafuta ya petroli, maski na zana zenye ncha kali wakijiandaa kufanya fujo wilayani Nachingwea.

Zambi alisema ukiondoa kasoro hizo hali kwa sasa ni shwari. Alisema katika Uchaguzi Mkuu, CCM mkoani humo imepata madiwani 137 kati ya kata 152. Alisema pia CCM imepata ushindi kwenye majimbo yote manane.

Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga kwa niaba ya wakuu wa wilaya alisema serikali ipo macho kukabili uvunjaji wa amani katika wilaya za mkoa huo.

Alisema kuna taarifa za kuwepo njama na vikao katika moja ya kata kupanga kufanya maandamano mjini Lindi. Alisema taarifa hizo zinafanyiwa kazi na amewaonya watakaoandamana.

HabariLeo
 
tunakuomba mkuu wa mkoa wa Lindi watuhumiwa hao washughurikiwe vilivyo bila huruma. Na magari yaliyo chomwa moto yarudishwe nikiwa na maana kwamba wayanunue kwa pesa yao wenyewe. Na ofisi zilizo bomolewa zijengwe kwa pesa zao wenyewe. Kama ni chama fulani kiliwatuma kiwajibishwe kwa kuharibu mali za serikali. Nyongeza naomba hao jamaa wapigwe virungu vya uhakika ili wawataje wenzao walio kimbia na mtu aliye watuma.
Ni hayo tu ndugu mkuu wa mkoa.
 
Watanzania wengi wanaandamana mioyoni daima dhuluma na haki hudaiwa japo kimya kimya.
 
tunakuomba mkuu wa mkoa wa Lindi watuhumiwa hao washughurikiwe vilivyo bila huruma. Na magari yaliyo chomwa moto yarudishwe nikiwa na maana kwamba wayanunue kwa pesa yao wenyewe. Na ofisi zilizo bomolewa zijengwe kwa pesa zao wenyewe. Kama ni chama fulani kiliwatuma kiwajibishwe kwa kuharibu mali za serikali. Nyongeza naomba hao jamaa wapigwe virungu vya uhakika ili wawataje wenzao walio kimbia na mtu aliye watuma.
Ni hayo tu ndugu mkuu wa mkoa.
Wameomba poo kwa mkuu wa wilaya..walidhani hizi ni zama za jk.
 
Back
Top Bottom