Uchaguzi 2020 Lindi: Majengo ya Serikali yachomwa, magari yaharibiwa kisa Uchaguzi

Usemayo ni kweli kwa 100%!

Kuna mshikaji wangu mmoja kule, siku ya uchaguzi nilim-text, lakini HAKUJIBU!!

Jana akanitafuta mwenyewe, na kuniomba radhi kwa kushindwa kujibu message yangu, na akaeleza ni namna gani alikuwa kwenye wakati mgumu kupita maelezo kutokana na vurugu za uchaguzi huko Lindi!

NIKASHANGAA, na kujiuliza ni kwa namna gani yote hayo unayosema watu tulikuwa hatufahamu!!! Kwahiyo, again you're 100% RIGHT, media ziliogopa kuripoti!

Hata hivyo, jamaa alinieleza yote hayo kutoka eneo lake la kazi, yaani Mtama... Mtama kule kule ambako Tume wametuambia Nape alipita bila kupingwa!!

Sasa kwa habari hii, inaonesha kumbe Lindi yote ilichafuka kwa vurugu wakati mwanzoni nilidhani ni Mtama pekee!!

Jamaa ni mtumishi wa serikali, na akanitajia maeneo mbalimbali ambako ziliibuka vurugu baada ya kura kubadilishwa na kupewa wagombea udiwani wa CCM!!

Akanieleza hata jimbo la Mchinga ambako Mama Salma amepita ubunge, kata kubwa mbili zenye population kubwa zaidi kwenye jimbo la Mchinga, kata zote zimeenda kwa upinzani, manake uhaini wa CCM ulishindwa kufua dafu huko!!!

Wazoefu wa huko wanasema hizo kata ndizo huamua mshindi wa uchaguzi wa ubunge, na kwahiyo unaweza kufanya hesabu ya 1+1 kupata hali halisi ya ushindi wa Mama Salma wakati kata kubwa zimeikataa CCM!!

Aidha, kata ambayo mshikaji mke wake alikuwa ni msimamizi wa uchaguzi, unaambiwa matokeo ya haki yalitangazwa kwa nguvu za wananchi kwa sababu hadi saa 7 usiku, raia waligoma kuondoka, na ndipo akatangazwa diwani wa ACT!

Kwahiyo kauli yako kwamba CCM ipo ICU huko Lindi, ni ya kweli manake hata kijiji anakotoka Shemeji yangu, na kwenyewe kata imeenda upinzani lakini na kwenyewe kulikuwa na vurugu kweli kweli!
Watu wakusini ndivyo walivyo hata ukiwa mfanyakazi kule uwe makin na matendo yako
 
Back
Top Bottom