Limbwata - Tujihadahari

Bahati furaha

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2012
Posts
3,077
Reaction score
1,439

Kuna aina nyingi za limbwata, kuna kaligoligo, shuntama (Maana kwa kiswahili inama) ya Kanda ya Ziwa ambayo akipewa mume, kila atakachoambiwa na mke atafanya. Lakini kuna limbwata ya kisaikolojia ambayo ni huduma bora na maalumu kwa mume, hii mara nyingi hupatikana maeneo ya mwambao.

Vibao vya matangazo vilivyozagaa nchini vikitangaza huduma kutoka kwa waganga mbalimbali wa kienyeji, havidanganyi. Vinadhihirisha ukweli kuwa wapo wateja wanaohitaji huduma hiyo kwa wingi.
Aina za dawa
Mfano dawa za kumlinda mume ziko za aina mbili, zinazofanya kazi ya kumkosesha nguvu ya kufanya tendo la kujamiiana anapokwenda kwa hawara na zile ambazo humfanya moyo uwe mzito kusaliti ndoa.
Uchunguzi wa gazeti hili katika viunga vya Jiji la Dar es Salaam ulibaini kuwa katika kila vibao kumi vya matangazo, vinane vilitaja huduma ya kumtuliza mpenzi, mume au mke.
Ilibainika kuwa waganga wengi wa kienyeji, wanatoa dawa za mapenzi kuliko hata zile za kupandisha cheo, kutoa mikosi au za bahati.
Mganga mmoja, kwa jina la Bibi Maajabu, alisema wateja wake wengi ni wanawake ambao hufika kumwona kwa ajili ya kupata dawa za kumdhibiti mume.
"Wengi wanafika hapa wanaomba dawa za kumdhibiti mume, wanaume wanaokuja kwa ajili ya kuwadhibiti wake zao si wengi kama walivyo wanawake," alisema Bibi Maajabu ambaye anapatikana maeneo ya Njia Panda ya Kigogo.
Alisema yeye anatoa dawa kwa wanawake hao, dawa ambazo hata hivyo anadai ni siri yake na wateja wake tu.
Bibi huyo alisema dawa zake zinafanya kazi kweli na wala hakuna utapeli kama wafanyavyo waganga wengine.


Mganga mwingine, mkazi wa Tandale maarufu kwa jina la K, yeye hakutofautiana na Bibi Maajabu. Alisema wateja wake wakubwa ni wanawake hasa wenye matatizo ya ndoa na hufika kwake kutaka kupata ‘mwarobaini' wa kumdhibiti mume.

"Katika wanawake sita wanaofika hapa kwa siku basi wanne watakuwa wanataka dawa za kumdhibiti mume, au kumrudisha mume aliyekimbilia kwa mke mdogo," alisema K.
Alisema wanawake wengine huwa na mahitaji ya matibabu, kuondoa mikosi lakini nao pia wanaweza wakahitaji dawa za kuwadhibiti wenza wao.
"Wengine wanataka ndoa, na mimi ninayo dawa ambayo nikikupa, mpenzi wako anatangaza ndoa ndani ya siku 14 tu," alisema.
K, hakutofautiana na Bibi Maajabu, naye alisema hawezi kutaja mchanganyiko wa dawa ambazo wanawapa wanawake wawachanganye waume au wenza wao.


Wanatoa juju la Kufuli na Kalamu.

Mzee Kingomba Moto Motowaka, (75) mkazi wa Chanika alisema yeye ni bingwa wa kutoa dawa za kumtuliza mume au mke.
Alisema kwa kawaida anatoa dawa kwa wanawake na wanaume ya kuzuia mwenza asitoke nje ya ndoa, ambayo ipo mfano wa kufuli.
Motowaka alitoa mfano wa juju la kalamu, kuwa kalamu zote zina kifuniko, kama mwanamke anataka kumfunga mume wake, anaenda kwa mganga wa kienyeji na dawa hupakwa katika uke. Mwanamke hupewa kalamu mpya yenye kifuniko kisha atafute mbinu ya kumwambia mume wake afunike kalamu kwa kifuniko bila kufahamu madhumuni ya kuifunga.


Kufuniko cha kalamu

"Mwanaume akishafunika kifuniko katika kalamu, moja kwa moja atakuwa amejifunga na hatoweza kutoka nje ya ndoa yake hata siku moja," alisema. Kalamu hizo huwekwa sehemu salama na mwanamke na hiyo inatakiwa kutunzwa ili mtu asije akafungua hicho kifuniko cha kalamu kwani kikifunguliwa, basi mwanaume naye atapata nguvu ya kutoka nje ya ndoa.
Mbinu nyingine anayoitaja mganga huyu haitumii kifaa chochote kile bali mganga hutakiwa kutemea dawa katika uume au uke wa mwanamke hivyo hakuna mtu mwingine atakayeweza kufanya tendo la ndoa na mume/mke huyo.



Mganga mwingine maarufu mwenye vibao vingi vya matangazo ya kazi zake kila kona ya jijini ambaye hakupenda jina lake litajwe alisema, dawa za kumdhibiti mume au mke zipo nyingi na nyingine zinahusisha wadudu kama nzi au funza.
"Kuna dawa ambayo mwanamke anaambiwa amwekee mume kwenye chakula. Anachukua nzi watatu anawaweka katika mboga, mume akishakula tu, hawezi kutoka nje ya ndoa hata siku moja," alisema.


Wanawake wanasemaje?

Wanawake wengi waliohojiwa kuhusu tuhuma za wao kwenda zaidi kwa waganga wa kienyeji kusaka dawa za mapenzi, walitoa ya moyoni lakini kwa kutopenda kutaja majina yao gazetini.
Mwanamke mmoja mkazi wa Buguruni Mnyamani, alisema wanawake wengi hupenda kwenda kutafuta dawa za kuwadhibiti waume kwa sababu wamekosa uaminifu.
"Unajua inauma sana unapojua mume wako anakusaliti au ameoa mke mdogo, kwa sababu huwezi kumfungia ndani asitoke au kushtaki polisi, basi waganga wa kienyeji ndiyo wanakuwa kimbilio letu," alisema.
Alisema waganga hao wanawapa dawa ambazo si za kudhuru kwa ajili ya kuwadhibiti waume au wenzi wao kwa minajili ya kutunza ndoa zao na si vinginevyo.
Mwanamke mwingine, Anastazia Aron, mkazi wa Arusha anakiri kuwa wanawake wengi wanakwenda kwa waganga wa kienyeji lakini anawalaumu kwa kukosa kujiamini na kujiharibia utu wao.
"Mimi ninafahamu kuwa wanawake wanakwenda sana kwa watu hawa, lakini nawalaumu kwa sababu hawajiamini. Zipo njia mbadala za kumfanya mume wako asitoke nje lakini waganga ni matapeli," alisema Anastazia.
Mwanasaikolojia na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Modesta Kimonga alisema kinachosababisha wanawake wengi kutafuta dawa za mapenzi ni kutokujiamini.
Alisema kisaikolojia, wanawake wengine wanakosa kujiamini katika uamuzi, hivyo mara nyingi utakuta wanaegemea ushauri wa marafiki.
"Mapenzi siyo dawa, dawa ni wewe mwenyewe, wanakurupuka wanatafuta njia za mkato," alisema Kimonga.
Baadhi ya waganga wa kienyeji, wanahama mkoa mmoja hadi mwingine kutafuta wateja na wakati mwingine hupanga katika nyumba za wageni kwa kipindi kirefu.
Imamu wa Msikiti wa Shababi, Kimanga, Salimu Kihiki alisema wanawake wanafanya hivyo kwenda kwa waganga wa kienyeji kwa sababu za kutokujiamini na kutokuwa na hofu ya Mungu.
Mchungaji wa Kanisa Assemblies of God (TAG), Kihesa Morogoro, Innocent Mfyatulila alisema, tatizo ni kweli kuwa wanawake wengi wanakwenda zaidi kwa waganga wa kienyeji kuliko wanaume na hili linasababishwa na mambo mawili makuu ambayo ni saikolojia na historia.
"Wanawake wengi kisaikolojia hawajiamini, wanahisi kwamba ili mume awe wa kwake peke yake ni lazima aende kwa mganga na kihistoria imetokana tangu zama za Adamu na Eva," alisema Mfyatulila.
 
Limbwata ni imani iliyoegemea zaidi kwenye imani za kishirikina. Haifanyi kazi kama zisivyofanya kazi imani zingine.

Anayebisha na anijaribu tuone.
 
Hiyo ya kizibo cha kalamu ndo poa!! ila ingependeza sana kama akinituliza kisha na yeye anatulia mwisho wa siku wote tunakuwa salama.
Kwa bahati mbaya uzoefu unaonyesha wengi waliowaroga wenzi wao,huwa wanakuwa mapepe sanaView attachment 99152
 
kunb mmoja alimroga kibosile ili afaidi mali tena alimtia kwenye kichupa akaenda kukifukia makaburi ya kinondoni.
Sasa kibosile hela ikakata na anamganda bibie kinoma na bibie alitaka mpunga tu.
Hela imekata hamtaki na dawa ndo kwanza zimeanza kufanya kazi.
Utamu upo hapo hapa sasa kaburi alilofukia kichupa hakumbuki yaani full matataizo
 
Good God Amu do you believe this!!!
 
Naona JF limekuwa jukwaa la kufundishana mambo ya Ulozi...kuna jukwaa jingine huko jamaa kaweka habari za majini
 
Haya makubwa sana yaani inzi na funza
acha nipite bila breki naona mko mbali
wakati wenzetu wanakwenda Mars,sisi
bado tuko kwenye mambo ya Ugoro kula.
 
Hayo mambo ndio maana kuna kwaya moja ikaja na wimbo wa KEKUNDU. mtaua waume zenu kwa kuendekeza mambo ya ulozi. kama unampenda na unamtimizia haja yake, unamheshimu na unajitambua, unajua wajibu wako na unawajibika ndio limbwata tosha.
 
hivi hawa waganga mbona hawapatikani Masaki, Mikocheni, Mbezi beach sijawaona pia Upanga? Y tu kigogo, buguruni Mnyamani, chanika ehe ehe.
 
Haya makubwa sana yaani inzi na funza
acha nipite bila breki naona mko mbali
wakati wenzetu wanakwenda Mars,sisi
bado tuko kwenye mambo ya Ugoro kula.

Halafu mtu akiumwa tumbo mwenzie anasema "mapenzi ya Mungu"!
 
Hiyo ya kizibo cha kalamu ndo poa!! ila ingependeza sana kama akinituliza kisha na yeye anatulia mwisho wa siku wote tunakuwa salama.
Kwa bahati mbaya uzoefu unaonyesha wengi waliowaroga wenzi wao,huwa wanakuwa mapepe sanaView attachment 99152

Mkuu, huwezi kuhisi umelogwa/unalogwa kama wewe huna 'chembechembe' hizo ndani mwako.
 
hivi hawa waganga mbona hawapatikani Masaki, Mikocheni, Mbezi beach sijawaona pia Upanga? Y tu kigogo, buguruni Mnyamani, chanika ehe ehe.

Maeneo kama Mikocheni, Mbezi beach,Upanga,makazi ni ghari,Ila watu wanaokaa maeneo hayo nao ni wateja wazuri tu,kila leo utawakuta Kigogo,Buguruni,Chanika nk..
 
Mtaliwa sana na waganga. Mwanamke una gubu, matusi, kero mchafu akutake mwanaume gani?
Lazima atatoka nje
 
Naona JF limekuwa jukwaa la kufundishana mambo ya Ulozi...kuna jukwaa jingine huko jamaa kaweka habari za majini
Mkuu watu8 Kwani Majini hawapo? Wewe unawaogopa Majini nini? Basi watakufuata hapo ulipo wewe unasemaje?
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…