LILIKUWA NA UZURI GANI ?

Sharif

JF-Expert Member
Mar 13, 2011
2,471
2,000
Kwanza napenda kuwakumbuka wale wote ambao waliukaribisha mwaka 2015 kwa shauku kubwa bila kujua kwamba walikua wanajiandaa kufunga ukurasa wa mwisho wa historia ya maisha yao huku wakiacha ndoto zisizotimizika japo waliamini kwamba "kila mbwa ana siku yake" lakini ya kwao ikawa ni ile ya kuishia mita kadhaa ardhini katikati ya vilio.

Naamsha fikra na kulikumbuka JUMBA JEUPE
*Jumba jeupe lilizaa mbinu halali na haramu kuliishi
*Jumba jeupe liliweka damu rehani ili aliyemo asitoke na akitoka aingie wa mfano wake pekee

*Jumba jeupe liliwafanya chui kuvaa ngozi za kondoo
*Jumba jeupe liliwafanya wajenge kiburi na kujipa sifa ya uungu ya kutaka kutukuzwa na kupigiwa kila goti pasipo kupingwa

*Jumba jeupe liliufanya umma kusalitiwa kwa gharama ya jasho lake
*Jumba jeupe liliwafanya waliopendwa kupewa jina la mbwa mbaya

*Jumba jeupe liliwafanya waviache vitabu vinavyoaminika kua vitakatifu na hatimae kuwa washirikina wa matambiko...

JUMBA JEUPE LA MFALME POLYBUS
LILIKUA NA UZURI GANI ?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom