Likizo ya Serikali imekaribia kuisha? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Likizo ya Serikali imekaribia kuisha?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by GHOST RYDER, Jul 13, 2011.

 1. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #1
  Jul 13, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Nnamaliza Likizo yenu lini?

  Sina mashaka wala hofu juu ya Likizo hii ndefu ya serikali ambayo inadhihirishwa na uwajibikaji hewa na mipango muflisi inayokinzana na utashi wa wananchi walio wengi.

  Katika hali ya kusikitisha kabisa Nchi imerudi katika hali ya ujima huku kasi ya uzalishaji ikiporomoka kwa kasi ya ajabu na kupoteza kabiasa ndoto za kumjengea mtanzania maisha bora kama wimbo wa serikali ya CCM ambao sasa hata katika hali ya kawaida ukiuingiza katika top 40 za radio one utaishia kushika nambari 30.

  Huduma na pampu za maji mijini zinawezeshwa na upatikanaji wa nishati ya uhakika ya umeme, hakuna umeme hakuna maji katika maeneo mengi pia ambapo pump zinategemea nguvu ya umeme kusukuma maji.

  Ni kero kwa kiwango kikubwa huku adha hii ikiwatatiza kwa kasi wakazi wa maeneo mengi ya mijini na kibaya zaidi kwa ndugu zangu wenye vyoo vya maji, hii kadhia inapoteza heshima katika familia.

  Inashangaza kuona ni siku moja baada ya Mkullo kusoma bajeti na ongezeko la faini kwa wakiukaji wa kanuni na sheria za usalama barabarani, askari walafi na wenye uchu wa senti walianza kutekeleza azimio hilo asubuhi na mapema ya siku iliyofuata huku madereva hoe hae wakionja joto ya Jiwe.

  Kwa kasi hiyo ya ulafi mbona mmeshindwa kupunguza bei ya mafuta mpaka leo, vituo vingi vya mafuta tofauti na BP ambao wanayauza kwa sh. 2367 lita moja ya petrol kwingineko pia bei bado imeng’ang’ania Tshs. 2570 sasa hapa kama si kwenda likizo kwa serikali ni nini?

  Haya ya umeme, bei za mafuta na maengine mengi mliyoahidi kuyashusha mara moja kupunguza ukali wa maisha mbona yameshindikana huku ongezeko la kodi linatekelezwa kwa kasi ya ajabu na wanaokiuka huko wanakiona cha moto.

  Mipakani yanakopitishwa magari kutoka nchini Kenya kule Namanga na Sirari, waagiza magari na vifaa vingine kutoka nje ya nchi kupitia maeneo hayo wanakiona cha moto. Sitaki kusema lolote kuhusu Bandari ya salama maana unyang’anyaji wa kodi hapo ndio sera tofauti na kanuni za utozaji kodi.

  Kwa mantiki hii tuambieni viongozi wakuu wa serikali hii legelege lini mtatoka likizo mje kushughulikia hizi kero za wananchi?

  Porojo na sifa mnazopeana Bungeni za umakini na uadilifu zinalenga zaidi katika shukrani binafsim kwa kupeana ulaji na si katika uadilifu na umakini wa kushughulikia kero na mipango ya kumtanzua mtanzania katika Lindi la Umaskini.

  Tukilalamika mnasema hizi ni kelele za wapinzani, sijui kama ndugu zenu ambao pia wanaathirika na mfumko huu wa bei ya soko na wao pia ni wapinzani au pengine wao wana soko lao la siri ambapo wananunua bidhaa kwa unafuu.

  Haitashangaza kuona wanasiasa kama Kafulila wanawatukana matusi ya dhahiri kwa uzembe na uwajibikaji mfu ambao unadhihirisha wazi likizo mliyokwenda ni ndefu na sijui itamalizika lini?

  Huku ni kuiweka Nchi rehani, madhara na majibu yake kutoka kwa watanzania yanaweza yakawa kinyume kabisa na matazamio ya wengi, chonde chonde tokeni katika likizo hiyo mliyojipa kinyemela nje mtanzue kero za watanzania.

  ADIOS

  G.R
   
 2. s

  smz JF-Expert Member

  #2
  Jul 13, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 251
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu,

  Wakigoma kurudi, waache mpaka 2015, huo ndo mwisho wa likizo yao, wapende wasipende.
   
 3. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #3
  Jul 13, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Inavyoelekea hii Likizo endapo watajiongezea mpaka 2015 itakuwa na Tija sana sana
   
 4. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #4
  Jul 14, 2011
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Indeed serikali wako likizo! Miaka ya 2006 tuliambiwa wako 'honeymoon' na nchi ikaingia gizani kwa shida ya umeme, leo hii miaka 5 baadaye hawana jibu walikuwa wanafanya nini kushindwa kumaliza tatizo hili.

  Na hizi ahadi bandia tunazoambiwa eti serikali imejipanga kutatua tatizo hili, ni juhudi za wapiganaji wa cdm ambao wanawaamsha usingizini watawala wetu kila wanapojifanya kutusahaulisha.
   
 5. MANI

  MANI Platinum Member

  #5
  Jul 14, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  "Mipakani yanakopitishwa magari kutoka nchini Kenya kule Namanga na Sirari, waagiza magari na vifaa vingine kutoka nje ya nchi kupitia maeneo hayo wanakiona cha moto. Sitaki kusema lolote kuhusu Bandari ya salama maana unyang'anyaji wa kodi hapo ndio sera tofauti na kanuni za utozaji kodi."

  GR hapo umenena mfumo wa kutoza ushuru tunakoelekea gharama za vitu zitakuwa kubwa!
   
Loading...