Likizo bila malipo kwa watumishi wa umma

rosita

JF-Expert Member
Oct 18, 2013
509
468
Nawasalim ndugu zangu

Naomba msaada kwa yeyote anayefahamu utaratibu wa kuomba likizo bila malipo serikalini ili nikafanye kazi katika shirika lingine la kimataifa...Nimefanikiwa kupata kazi katika shirika hilo na nipo kwenye hatua za awali za kuajiriwa..nimejaribu kuongea na afisa utumishi wangu lakin hakunionesha ushirikiano wa kutosha zaidi ya kunikatisha tamaa na wamekuwa waoga sana kutokana na matamko yanayotolewa kila siku na viongozi wetu...

Ningependa kujua pia inaweza kuchukua muda gani baada ya barua kupitishwa na mwajiri ili kupata hiyo ruhusa?

Na wizarani ni idara gani au utaratibu upi unatumika kupokea maombi husika ?

Naamini JF ni jukwaa linalokutanisha watu wengi naomba kama kuna watu wanaofahamu hilo mnielimishe tafadhali na kama wapo watumishi ambao wanafanya kazi wizarani hususani katika hicho kitengo au unafaham utaratibu wa hicho kitengo ninaomba kupata msaada wenu tafadhali.

Ahsante kwa ushirikiano

Mungu awabariki
 
Naona unawaamusha waliolala, hujui kama wote wana ID fake humu.

Ungeomba tu utaratibu ila sio kusema umepata kazi.

Siku si nyingi utasikia linazungumziwa hili.
 
Sasa kama umepata shavu kwingine si uache kazi kabisa nafasi yako ibaki wazi na wengine wapate hiyo riziki?
 
Naona unawaamusha waliolala, hujui kama wote wana ID fake humu.

Ungeomba tu utaratibu ila sio kusema umepata kazi.

Siku si nyingi utasikia linazungumziwa hili.
We jamaa unajizibia riziki mzee!!!!!!
 
Naona unawaamusha waliolala, hujui kama wote wana ID fake humu.

Ungeomba tu utaratibu ila sio kusema umepata kazi.

Siku si nyingi utasikia linazungumziwa hili.


Niko tayari kwa yote. Katika haya maisha hatupaswi kuishi kwa woga ..Ahsante kwa ushauri Mkuu
 
One mistake.....goal!!!;.....utakuta unamuulizia mtu ambaye anakukatisha tamaa ofisini, unakuwa umehamisha maimbi akusaidie kupitia JF.....hahahah. Mwaka 2013 nikiwa Dom kuna kazi nilikuwa namfanyia muhadhiri mmoja wa UDOM, sasa nikawa nmechoka kumfanyia kazi nikawa nataka nipate kazi nyingine na mkoa mwingine sio Dodoma...aisee nikaja hapa nikatiririka mambo kwa uwazi hadi mahali nolipokuwa nafanyia kazi, kumbe yule bosi yumo humu na aliiona ile post, kwakuwa sikuweka lugha kali na za kuudhi...kesho take nmeingia job kumbe kaacha maagizo kwa mkewe kwamba nikija nimuachie CV yangu ili bosi akipata njia basi aniunganishe na kazi nyingine....na bahati mbaya namba ya bosi nilikuwa sina mara baada ya wiki nikapigiwa simu ngeni alafu sikupokea...nikakimbilia mpesa kuangalia jina...jina kamili la bosi nikawa silijui...nikampigia nikamtaja kwa jina lake kwamba nmeona missed call...jamani!!!! Kuna mfanyakazi wa ndani mmoja nikamwita kumuuliza bosi wake anaitwa nani....nikatajiwa jina lile ambalo ndio nilimpigia simu kwa mbwembwe namba ileile akaniambia ni ya baba...basi nikachoka nikaja JF kubadilisha ID name na nikakaa wiki mbili nikafungua ofisi yangu....alinisihi nisiondoke hadi nipate kazi nyingine lakini niligoma.....na yangu hapo nilijifunza kitu...usiweke uwazi hadi ukapitiliza!!!!ni hatari sana
 
Back
Top Bottom