likikugusa ---- LIMEKUHUSU | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

likikugusa ---- LIMEKUHUSU

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by under_age, Oct 14, 2007.

 1. u

  under_age JF-Expert Member

  #1
  Oct 14, 2007
  Joined: Apr 17, 2007
  Messages: 317
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  thamani yetu iwapi?,wanyonge wa duniani.
  wanaotujali wangapi?,mbona hawaonekani?
  haki zetu ni zipi?,mbona hazijulikani?
  makosa yetu ni yepi?, hata tuwe adhabuni?

  masuali yamenijaa , kichwani najiuliza
  kitembea hujikwaa , nasubiri mliwaza.
  nishaikata tamaaa , nasubiri miujiza
  wanasiasa hadaa , wamo watuangamiza.

  ni wengi watesekao , ni malaki kwa lukuki.
  wamekimbia makwao , kuitafuta riziki.
  mataifa watokayo , yamekana zao haki.
  wakubwa ndio walao , wanyonge tunahiliki.

  wengi barabarani ,usiku hujilalia
  vyakula vya majalalani, ndio wao hujilia.
  ya kinamama sisemi , heshima nawatunzia
  watawala ni nani? , wasiotufikiriaa.

  wanatunyima elimu , wanasema hatusomi
  matibabu yalazimu , pesa iwe mfukoni.
  maji nayo ni adimu , umeme hatuuoni.
  tumemkosa hakimu ,twamuachia manani

  kuna wanaojinyonga ,kwa kuchoshwa na dhuluma.
  kuna tunaojitenga , na siasa za hujuma
  msitufanye wajinga ,kutunyanyasa daima.
  mwatudharau mwaringa ,mwatuchimbia nakama.

  duniani tunaishi ,mithili ya nusu wafu.
  matatizo hayaishi , si sasa wala halafu.
  wakubwa haziwatoshi , wazitafuna sarafu.
  wajifanya ni wacheshi , wakitubana mapafu.

  watawala fikirini , nasi pia binadamu.
  kile mnachotamani , nasi pia tuna hamu.
  mwatibiwa ugenini , sie twafa majumbani.
  haki yetu ni nini? , mbona mnatudhulumu?

  roho zetu mwaziona , ni kama roho za mende.
  miili yatuzizima , hatujui wapi twende.
  twamuomba karima , atujalie tushinde.
  atuepushe daima , na madhara atulinde.

  hatujali utajiri , twaomba uadilifu.
  muwajali mafakiri ,msiwe wabadhirifu.
  hapo sisi tutakiri , serikali ni tukufu.
  rushwa nayo ni hatari ,wekeni uaminifu.

  maisha yenu ni mema , hayafanani na yetu.
  daima mko salama , sie "hofu" jina letu.
  kutwa kucha twalalama,hamjali vilio vyetu.
  na tukiamua kusema , mwaziba midomo yetu.

  "Taifa ni maskini" ,mwashindwa kuthibitisha.
  nyuso zetu ziko duni , zenu nyie zang'arisha.
  twawaona majiani , magari mwabadilisha.
  wale tulo maskini , kijio chatuhangaisha.

  kukumbushana wajibu , nami leo nakumbusha.
  si lazima mnijibu , mkifahamu yatosha.
  maisha ni majaribu , iko siku yatakwisha.
  kwa mola kuna adhabu , kaburini kunatisha.

  shairi nahitimisha , kwa mnasaba wa dua.
  yarabbi tasahilisha , na kheri kutuletea.
  dhuluma ataondosha ,atujaaliye sawiya .
  zisitupate presha , atulinde na ghasiya.

  tunamuomba muumba , atujaalie subira.
  atulinde na kasumba ,za wanasiasa na sera.
  awafedhehi watimba ,wanaodanganya kwa kura.
  atubariki wa shamba , tusiamue kugura.

  amiin.
  ni mdogo wenu underage
   
 2. N

  Nurujamii JF-Expert Member

  #2
  Oct 15, 2007
  Joined: Jun 14, 2007
  Messages: 414
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  very thoughtful of you underage! keep it up. Litawagusa tu, hata kama wakijifanya haliwahusu
   
 3. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #3
  Oct 15, 2007
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ..asalaam aleykhum!

  ..ulipotea kidogo,au ulikuwa hausikiki!

  ..shairi zuri hili,kwa kila tafsiri ya neno zuri!
   
 4. u

  under_age JF-Expert Member

  #4
  Oct 15, 2007
  Joined: Apr 17, 2007
  Messages: 317
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  waaleykum salam .
  nilikuwa napiga mpunga wa iddi el fitri yakhee.
   
 5. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #5
  Oct 15, 2007
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ..halafu ukala mwenyewe sio?

  ..yakhee!uungwana kukaribishana ati!japo kidogo tu!

  ..sasa,pilau aliloleta invisible si ushalila?maana haya mashairi nadhani yametokana pia na kushiba hilo,pilau!

  ..ushanifahamu nadhani!
   
 6. N

  Ngao Member

  #6
  Oct 15, 2007
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kimuachia manani, kusema tena ya nini?
  Kilileta barazani, nasi tutalitamani,
  Tuweke wetu uneni, tujiulize kwanini,
  Tafauti halifani, lisipofika bungeni!

  Ya Mola msikitini, kisujudu mswalani,
  Ni kimya kimya rohoni, tuwapo majaribuni,
  Hatumulizi kwanini, kwani ye ndio Manani,
  Sudi yetu mikononi, kashiklilia Manani!

  Ya hawa wanasiasa, dawa yao kuwaasa,
  Au la ni kuwatosa, kura siwape kabisa,
  Kwani ni yetu makosa, kuwaweka maafisa,
  Kumbe wote matutusa, tena ni wezi kabisa!

  Andaeji nakuasa, ya hawa wanasiasa,
  Hawapigiki msasa, wameoza kwa mikasa,
  Na lifaalo kwa sasa, tuwanyime uafisa,
  Taifa kulitakasa, TUTAKUPA UAFISA!!!!
   
 7. u

  under_age JF-Expert Member

  #7
  Oct 16, 2007
  Joined: Apr 17, 2007
  Messages: 317
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  ha ha ha

  yakhee mie mwenyewe nilialikwa naweye wataka nkualike, si tutafurushwa sote unkoseshe namie,mbona nyie hilo ubwabwa la invisibo hamjanialika?
   
 8. u

  under_age JF-Expert Member

  #8
  Oct 16, 2007
  Joined: Apr 17, 2007
  Messages: 317
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  nimefurahi rijali , kupata lako shairi.
  limenifunza kwakweli, waziwazi ninakiri.
  tujikaze kwelikweli ,kuwaasa wajeuri.
  wapunguze utapeli , na pia chao kiburi.

  "kumuachia manani" , sikusudii tulale.
  ila kumbuka yakini ,yeye ndie apangae.
  tuingiapo vitani , yeye atusaidiee.
  na pia huko bungeni , shujaa amnyanyue.

  nakushukuru kwa tena ,kutoa yako mawazo.
  nataraji wataona ,watalipata funzo.
  maneno uliyonena , si ya kufanyiwa bezo.
  uafisa ulonipa , nakupa wewe tunzo.

  NGAO usiwaogope ,wakikosa waambie.
  watawala walo kupe , damu wasituibie.
  watudanganya kwa kope, mazuri tuwadhanie.
  walichoiba walipe , wanyonge tushuhudie.

  beti zangu namaliza , muda umeniishiaa.
  JF tunawezaa, , ikiwa tutapaniaa
  kuwafichua twaweza , wanasiasa bandia.
  wanaotukandamizaa ,wanyonge tuso hatia.

  tukionesha mfano , wengine watafatiaa.
  tuanzishe mpambano, walafi kuwang'atua
  mpemba kwa mzaramo, tuikabili kadhiaa
  sote tuwe msimamo ,wanyonge kuwakomboa.

  tuwe kamba madhubuti ,haki zetu kutetea.
  tuwe makini kwa dhati ,adui kumtambuaa.
  tusimpe tena kiti ,akija tena gombea.
  tumuite msaliti , machoni akitujia.


  tanabahi:neno vita katika shairi limekusudiwa vita vya maneno na fikira sio vya upanga. tunaijali amani na tutaithamini milele.

  ni mdogo wenu underage
   
 9. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #9
  Oct 16, 2007
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ..basi harufu ya ubwabwa pekee inatosha,huitaji mwaliko!

  ..hasa ukiwa mchele wa morogoro,kama wa jana!

  ..mtamu kama vipeto!
   
 10. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #10
  Jun 14, 2017
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,427
  Likes Received: 22,347
  Trophy Points: 280
  Moja ya tenzi bora kabisa
   
Loading...