'Like' hii kama vipi 'potezea'

'Like' hii kama vipi 'potezea'

Head prefect

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2013
Posts
225
Reaction score
108
***nimeipenda hii***

Habari wana MMU:
Utafiti unaonesha kuwa kuna baadhi ya vitu vilivyofanya ndoa za babu zetu zidumu tofauti na hizi za zama hizi. Mojawapo ya vitu hivyo ni aina ya malazi waliyolalia ikiwa ni ngozi za wanyama,mikeka na vitanda vya samadari vilivyokuwa na ukubwa usiozidi futi 2.5.
Udogo huo wa vitanda uliwafanya wanandoa kuwa karibu mno na kugusana usiku kucha. Hii iliwalazimisha kuongea hata kama wamegombana maana bila kusema "sogea huko" huwezi kupata nafasi ya kulala vizuri.
Baridi ilivyokuwa inaongezeka kunapokaribia kucha iliwalazimu wasameheane hata bila kuombana msamaha maana kugusana kule kuliwapa joto lililogusa mioyo yao na kufuta makosa yote na kuanza upya siku iliyofuata.
Sasa vitanda vyetu vya 5*6 na 6*6 havitoi nafasi ya kufuta makosa ya wanandoa kwani wakikoseana kila mtu anakuwa kwenye kona yake ya 6*6 na kusikia aibu ya kumgusa mwenziwe kutokana na makosa waliyofanyiana,nani aanze kumgusa mwenziwe? Nani aanze kupandisha mguu kwenye paja la mwenziwe wakati kulikuwa na ugomvi? Ngoma inakuwa droo mpaka asubuhi na ugomvi unakuwa palepale kila mmoja akijifanya nunda kwa kutompapasa mwenziwe.
Sasa je turudishe vitanda vyetu kwa fundi seremala virekebishwe viwe 3*6 ili viweze kusuluhisha wanandoa? Au tulalie mikeka kama ileeee ya babu na bibi ili tuondoe foleni ya kwenda kwa washenga,wazazi,mashoga na baba Paroko kusuluhisha majambo yetu????

~~~KARIBUNI~~~
 
...hakika kuna point ya msingi hapa
 
Hivi hao mababu zenu wangelikuwa ni watu wa mapenzi ya dhati....kwa nini walikuwa na ndoa za mitala??
 
Yaani unataka kutuambia current matatizo ya mapenzi kama ku cheat,watoto kubambikiwa,watoto wa nje ya ndoa,wanaume kugegeda ma housegirl na mama kugegeduliwa na ma house boy hiyo ndo SOLUTION(2x6)?come on...man be serious

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Hivi hao mababu zenu wangelikuwa ni watu wa mapenzi ya dhati....kwa nini walikuwa na ndoa za mitala??

ni msukumo wa mila na desturi za makabila mengi ya Kiafrika ambazo kwa sasa zimemezwa na utamaduni wa kimagharibi wa mke mmoja kwa mume mmoja
 
Yaani unataka kutuambia current matatizo ya mapenzi kama ku cheat,watoto kubambikiwa,watoto wa nje ya ndoa,wanaume kugegeda ma housegirl na mama kugegeduliwa na ma house boy hiyo ndo SOLUTION(2x6)?come on...man be serious

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

wengi wanakuwa wamekosa pumbao kwa wenza wao na wachache wanatoka nje ya ndoa zao kwa tabia zao za ufuska na tamaa
 
kwani mitala inaondoa mapenzi ya dhati?

Je unadhani unaweza kuwapenda watu wawili, watatu kwa kipimo kilekile?

Kama mwanamke mmoja tu aitwaye Hawa(mkewe Adam) alitokea ubavuni mwa Adam, je huyo mkeo wa pili, wa tatu n.k katokea upande gani wa mwili wako?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom