Mhere Mwita
JF-Expert Member
- Jan 24, 2012
- 235
- 1,275
Yahya Jammeh hana jeshi la kumtisha mtu, ana kajeshi ambako hakawezi kupambana na "Jeshi". Jeshi la Gambia linao wanajeshi wapatao 1000 tu ambao wanaweza kusaidiwa na kikosi cha askari 1200 wa jeshi la akiba. Katika jeshi ambalo liko tayari kwa vita lenye askari 1000, Kikosi cha Majini kina askari 125, cha anga kina askari 100 na Kikosi cha Ardhini askari takribani 700 huku kile cha kumlinda Yahya Jammeh kikiwa an askari 75 - 100. Jeshi la Gambia lina magari ya kivita pamoja na deraya takribani 12 na nyingi kati ya hizo ziko chini ya kikosi cha ulinzi wa Rais,".
Wana ndege sita za kivita zikiwemo Su-25 Frogfoot kutoka Georgia, Ndege mbili aina ya AT- 802A za kusafirisha vifaa vya kijeshi, ndege moja ya kivita aina ya Il-62M Classic, ndege moja ya kivita aina ya Skyban 3M na ndege moja ya kivita mahsusi kwa shughuli za ulinzi wa anga. Kwa upande wa jeshi la majini, wana boti 3 za kivita, ya kwanza ni Peterson kwa ajili ya kukagua malindo, pamoja na boti mbili ziendazo kasi ambazo zimetengenezwa nchini Hispania.
Bajeti ya jeshi la Gambia kwa mwaka mmoja ni dola za Marekani Milioni 1, hii ni moja ya bajeti ndogo kabisa za jeshi duniani. Kwenye viwango vya kimataifa vya kijeshi, jeshi la Gambia linashikilia nafasi ya tisa kutokea mkiani, yaani kama dunia inapambanisha majeshi kutoka nchi 200 duniani, Gambia inashika nafasi ya 191 ikishindana na vijeshi vidogo kama Bahamas n.k.
[HASHTAG]#Unadhani[/HASHTAG] kajeshi haka katamlinda Jammeh dhidi ya "mijeshi" yenye bajeti za dola Milioni 300 hadi Dola Bilioni 3? Ukitaka kujua zaidi soma uchambuzi wangu katika Gazeti la Mwananchi kesho.