Lijue bati la msouth kisha linunue kwa bei ya kiwanda

Ahsante kwa ushauri...
 

Vipimo vya Meter(m) na futi(ft)

Hivi ni vipimo ambavyo wengi tunavisikia sana kwenye habari za ujenzi ,pia vipo vingine kama sentimeter(sm) ,inchi nk.

Ila vyote ni vipimo vya kimahesabu ambavyo vinaamanisha kitu kimoja ila kwa namba tofauti,mfano 100cm ni 1000mm,au 3meter ni sawa na 10ft.

Hivi vipimo hutumika sansana wakati wa kupima urefu na upana na ni vigezo vikubwa sana vya tofauti ya bei ata kitu cha sehemu moja ,mfano mbao au bati au waya ya kampuni moja inaeza kuwa tofauti kutokana na vipimo hivyo vinapoongezeka.

Pia tujifunze tu jinsi ya kuvitumia pale mafundi wetu wanapotumia vimipo kwa units fulani na tukiingia sokobi tukute vinauzwa kwa unit nyingine iwe rahisi kwetu kufahamu haraka na kuzungumza lugha moja
Mfano fundi akikupimia kitu katika units ya meter na ukakuta sokoni ni kinauzwa kwa futi usichangnywe na mahesabu.3meter ni 10futi 10

Kifaaa kirahisi kupimia hivi vipimo kinaitwa measuring tape,tape measure au futi,au tape wote tunakijua kina number zinazonesha meter,futi,cm na inch kwa wakati mmoja
Zipo za 3m,5m, 8m na zinginezo

Hii ukiifungua tu unakutana na kitu kimeandikwa 3m=10ft kwa upande wa chini itapima meter na cm kwa tofuti za ukubwa wa no (fontsize),juu itaandika ft

Tutumie mda kujifunza na kuelimika kwa faida yetu wenyewe tusiibiwe kwa kuchanganywa na vipimo
 

SOMO LA UPANA WA BATI/UPANA UNAVYO ATHIRI BEI ZA BATI/KILA UULIZIAPO BEI YA BATI ULIZA LA UPANA GANI.

Hili ni somo kubwa sana katika ununuzi wa bati,kea kuwa unauhusiano mkubwa sana na bei ya bati ukiachilia sababu nyingine,ni kitu kikubwa sana kuzingati hasa kwa bati la aina moja na gauge moja.

Upana huwa katika vipimo vya centimeter(cm),meter(m) au milimeter(mm) n.k.

Upana hupimwa kwa kutumia measuring tape/tape/futi.itaonesha vipimo

Upana unauhusiano wa karibu pia na idadi za bati zitakazo kaa juu ya bati,ndio unatakiwa ujue unataka bati za upana upi?ili ufanye maamuzi sahihi wakati wa kununua bati na usichanganywe bei kwa kuwa ukatajiwa bei pungufu akafu ukapewa bati za upana mdogo amabo hauendani na bei halisi pia ukakubali bei ndogo wakijua watakupa bati hilo hilo ila upana pungufu,

Mfano bati la it5 la sunshare la upana wa 107cm=1075mm la gauge28 linauzwa 12,500/meter na bati hilo hilo la upana wa 87cm=870mm linauzwa 9436/meter 28gauge

Mfano bati la corrugated la gauge 28 upana wa 90cm=900mm linauzwa 9436/meter na bati hilo hilo la upana wa 86cm=86cm linauzwa 8720/meter la gauge 28.
Utaoana tofauti ya upana kidogo inavyoleta utafoauti wa mkubwa wa bei.

Mwisho ukishajua upana utakahitaji kea bati zako na mahesabu wa fundi ambao utakuonesha ni wapi unapunguza gharama,ujue pia upana halisi(overall width) na upana wa kuezekea(effective cover)
Kadri unavyonunua upana mdogi ndio unaongeza idadi ya piece za bati.

NB.Ukishanunua kagua bati zako kama ndio upana ukiochagua kwa kutumia futi yako.

Call/whatsapp 0656-816616 0766-004940
 
Mkuu naomba ujibu hili ni wengi tunatamani majibu ya haya maswali.
 
Walituaminisha bati hizi kwa elfu 50 unapata moja tu!
Ilikuwa nikipita kwenye nyumba zilizoezekwa na hizi bati nazihesaaabu afu nazidisha mara 50 elfu kwa kila bati...najikuta sitamani hata kununua kiwanja....
Shubaaamit!
Hahaha kiukweli elimu haikutolewa ipasavyo na watu walikuwa wapigaji Sana
 
Mkuuu maswali yote ulouliza yapo hapo juu toka page ya kwanza ,tuwe na utamaduni tu wa kusoma btn lines,nasi yunafurah ila ukiona mtu anauliza kitu ulichoaandika unjua watu hawasomi inavunja moyo,ndo maana ata no za simu zipo anayekuwa serious atakutafuta tu in any way ulizoweka
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…