Lijue bara la Afrika kwa undani

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,156
13,249
route_map.gif

Hapana shaka Bara la Afrika limekua kivutio kwa watu wa kaliba na kadhia zote ulimwenguni wakiwemo viongozi, wafanyabiashara, wawekezaji, watafiti, watalii na wengine wengi
Tukiwa na ugeni wa ya waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu. wiki hii Barani Afrika, ni vyema tukaendelea kukumbushana machache kati ya mengi kuhusu AFRIKA


1. 1. Bara la Afrika ni la pili kwa ukubwa miongoni mwa mabara saba ya Ulimwengu. Lina kilomita za mraba 30 million, ASIA ndilo bara linaloongoza kwa ukubwa kwani lina kilomita za mraba 44 million.

1.jpg


2, Mto Nile Ndio Mto mrefu duniani ambao una urefu wa kilomita 6,650. Pia mto Congo, ambao una urefu wa kilomita 4,700 unashika nafasi ya nane miongoni mwa mito mirefu duniani-mto Nile ndio taswira ya ustaarabu wa mwanadamu duniani (civilization) kwani unaunganisha mataifa 11 YA AFRIKA (Tanzania, Uganda, Rwanda, Burundi, Congo-Kinshasa, Kenya, Ethiopia, Eritrea, South Sudan, Sudan na Misri).


5.jpg


3, 30% ya madini yote duniani yanapatikana Afrika huku (asilimia 40 ikiwa ni dhahabu) Nusu ya almasi yote duniani, ikitoka kusini na Afrika ya kati


upload_2016-7-5_18-19-9.jpeg


3. Chura mkubwa zaidi duniani Chura mkubwa zaidi Duniani anapatikana barani Africa na amepatikana katika msitu wa nchi za Cameroon na Equatorial Guinea. Anaitwa Goliath, anaweza kukua na kufikia uregu wa mita moja na uzito wa kilo 3.
8.jpg

4 Jangwa kubwa Jangwa la Sahara ndilo jangwa kubwa duniani. likiwa limeenea katika nchi zipatazo 12, Jangwa la Sahara ni kubwa kuliko bara lote la Amerika ya Kaskazini (ikiwemo Marekani Yote).
upload_2016-7-5_18-21-18.jpeg


5 Jiji linaloongoza kwa idadi kubwa ya watu barani Afrika ni Lagos ambalo liko nchini Nigeria, lina jumla ya watu 21 million (zaidi ya mara nne ya DSM na takirbani nusu ya watanzania wote). Jiji la Cairo lililopo nchini Misri ni la pili likiwa na jumla ya watu 13 million, wakati jiji la Kinshasa linalopatikana nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo linashika namba tatu kwa kuwa na jumla ya watu 12 millioni, Afrika ni ya pili duniani ambayo ni sawa na 15% ya watu wote duniani.
Nchi ya Nigeria ina zaidi ya makabila yanayotambulika 370 na kutengana huku kukiwa na lugha hai 510. Kulinganisha, na bara la Ulaya likiwa pungufu kwa lugha 150 na nchi ya India ina lugha 400.
c5c23-07104c.jpg


6. Asili ya Mwanadamu
.
12.jpg


7. Kila mmoja ni Mwafrika kwa asili. Vipimo vya kisaba vya DNA vilivyofanywa vimethibitisha kuwa, binadamu wote ulimwenguni wanahusiana na watu wa kale ambao walihama barani Africa kiasi miaka 125,000 iliyopita. Watu wameanza kuzaliana zaidi katika mabara yote miaka 80,000 baada ya hapo.


8.Bara la Afrika ndilo lenye nchi nyingi zaidi duniani likiwa na jumla ya nchi 54 (Sahara Magharibi Ndiyo Nchi Pekee ndani ya AFRIKA ILIYOJITENGA); Bara la Asia ni la pili likiwa na nchi 49

upload_2016-7-5_18-24-44.jpeg


8. Bara la Afrika ni bara ambalo linapatikana wanyama wa aina zote yaani wenye kasi zaidi na wanyama wakubwa zaidi. Asilimia 85 ya Tembo wote Duniani wanapatikana Afrika huku ikiwa na asilimia 99 ya Simba wote waliosalia duniani kwa sasa huku 25% ya ndege wote duniani wakiwa wanapatiakana kwenye Bara hili huku Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa likiitaja Hifadhi ya Serengeti Kama eneo pekee la URITHI WA DUNIA kwa sasa (world heritage site) kwani ndiyo pekee iliyosalia kuwa na hayawani na ndege adimu duniani

Duma, ambaye anaweza kukimbia kwa umbali wa hadi kilomita 120 kwa saa, ni mnyama mwenye kasi zaidi duniani, wakati hakuna Tembo yeyote mkubwa zaidi ulimwenguni kuliko Tembo wa Africa.

upload_2016-7-5_18-26-25.jpeg
images

9. Ziwa Tanganyika lipatikanalo barani Africa, ni ziwa la pili kwa kuwa na kina kirefu ulimwenguni. Ziwa hili limekwenda chini kwa urefu wa zaidi ya kilomita 1.7. Hii ni pungufu ya mita 200 nyuma ya ziwa linaloongoza kwa kina kirefu ambalo linapatikana nchini Russia.

upload_2016-7-5_18-28-6.jpeg
images

10. ZIWA VICTORIA
Ziwa Victoria ni ziwa la pili kwa ukubwa ulimwenguni. Pia ni chanzo cha mto Nile. Ziwa Nyasa/Malawi ndilo lenye aina nyingi/species za samaki wa maji baridi kuliko ziwa lolote duniani

11. Nchi zote za Afrika kasoro Ethiopia na Liberia zimepita katika Kongwa la Ukoloni kwa miongo kadhaa huku Ghana ikiwa ya kwanza ilihali Zimbabwe ikiwa ya mwisho kujinasua kutoka kwenye kongwa la mkoloni
12. Tafiti zinaonesha kwamba 40% ya watu wazima hapa Afrika wako kwenye lindi la UJINGA wa kwa maana ya kutojua kusoma wala kuandika (Illiteracy) huku theluthi mbili kati yako wakiwa ni wanawake
HATA HIVYO RIPOTI YA BENKI YA DUNIA YA MWAKA 2013 INAIWEKA AFRIKA KAMA BARA MASIKINI ZAIDI KULIKO MABARA YOTE ULIMWENGUNI (AFRIKA NZIMA INACHANGIA 2.4% TU YA UTAJIRI/PATO LOTE DUNIANI/GDP)
www.google.co.tz/#q=poorest+continent+in+the+world


www.google.co.tz/#q=poorest+continent+in+the+world
 
African

In March 2013, Africa was identified as the world's poorest inhabited continent; however, the World Bank expects that most African countries will reach "middle income" status (defined as at least US$1,000 per person a year) by 2025 if current growth rates continue.
 
Ni bara masikini mno bali viongozi wao wana utajiri mkubwa ambao umepetikana kwa rushwa na kuwapa natumaini wananchi wao kwamba ipo siku na wao watakuja kuwa matajiri ila wawe na subir hadi Yesu arudi
 
Give thanks mama Africa. Africa is moving next level....oh wait.....kumbe bado tuko na viongozi uchwara.....rasilimali kibao wananchi wasikini kwelikweli, watawala wanaficha chapaa hadi vitandani mwao
 
African

In March 2013, Africa was identified as the world's poorest inhabited continent; however, the World Bank expects that most African countries will reach "middle income" status (defined as at least US$1,000 per person a year) by 2025 if current growth rates continue.
Amavubi, hizi predictions do not hold water in Africa! Waafrika ni shida, laana!
 
  • China is Africa’s top trade partner with Sino-African trade volumes now nearing $200 billion per year.
  • China’s direct investment in Africa exceeds $50 billion. Just look at the “Forum on China Africa Cooperation”.
  • Neocolonialism is a real threat with over 1 million Chinese citizens on the African continent. Angola alone has a population of over 350,000 Chinese.
 
  • Africa has approximately 30% of the earth’s remaining mineral resources.
 
  • Africa is the world’s hottest continent with deserts and drylands covering 60% of land surface area (e.g. Kalahari, Sahara and Namib).
  • Africa is the world’s second driest continent (after Australia).
 
Back
Top Bottom