Goliath mfalamagoha
JF-Expert Member
- Aug 3, 2012
- 602
- 2,505
HUYU BADO NI MBUNGE HALALI
Ibara tajwa ya 71 (1) (a) inatamka, pamoja na mambo mengine, kuwa Ubunge hukoma pale ambapo Mbunge atatokewa na jambo lolote ambalo linampotezea sifa ya kuchaguliwa kuwa Mbunge. Jambo la kufungwa ni kati ya mambo yanayompotezea mtu sifa ya kuwa Mbunge. Ndilo lillilopo kwenye Ibara tajwa ya 67 (2) (c).
Kimsingi, katiba katika Ibara ya 67 (2) (c) inataja kifungo kinachozidi miezi sita jela. Soma na kusema tena: KIFUNGO KINACHOZIDI MIEZI SITA JELA. Kwakuwa kifungo cha Lijualikali, kama akikitumikia na kukimaliza, ni cha miezi sita, hapotezi sifa ya kuwa Mbunge. Ni kwakuwa hakikuzidi miezi sita.
Kile kifungu cha Kanuni za Kudumu za Bunge ibara yote ya143 (1) Kuhudhuria vikao vya Bunge na Kamati zake ni wajibu wa kwanza wa kila Mbunge.
(2) Mbunge yeyote atakayeshindwa kuhudhuria Mikutano ya Bunge mitatu mfululizo bila ruhusa ya Spika iliyotolewa kwa maandishi, atapoteza Ubunge wake kwa mujibu wa Ibara ya 71(1)(c) ya Katiba na Spika ataiarifu Tume ya Uchaguzi.
(3) Mbunge atakapokosa kuhudhuria nusu ya vikao vya Mkutano mmoja bila ya sababu ya msingi atapewa onyo.
(4) Mbunge yeyote atakayeshindwa kuhudhuria vikao vya Bunge na Kamati zake kwa sababu maalumu atatakiwa kupata kibali cha Spika.
(5) Kwa madhumuni ya fasili ya (4) ya Kanuni hii, kibali kitatolewa katika Ofisi za Bunge za Dodoma au Dar es Salaam au Zanzibar.