Ligwaride linapomchosha Mke........


Wewe ndio mbulula kabisa wa maandiko kwahiyo kabla ya Yesu ilikuwa giza bali sasa ndio kuna mwanga kiasi watu hawana tena mioyo migumu? hapo ulipo haikosi unajiona mtakatifu kuliko watu wa kizazi cha Mussa au Daud. Kwanini walipokuwa wanamletea hoja alikuwa anawajibu mnayo torati na manabii? ni wapi aliposema achaneni na torati na manabii mshike yakwangu ambayo ni mapya? Yesu hakuja kukomesha uovu juu ya nchi bali kuasili torati na manabii na kuhalalisha hayo ni neno lake pia. Halafu mimi naongelea suala la kuoa sio kuzini. Hakuna amri kumi alizokuja nazo Yesu na amri kumi alizopewa mussa wala hakuna mungu wa kizazi cha Daud na mungu wa kizazi cha Mussa au mungu wa kizazi cha baada ya Yesu. Mungu ni yuleyule na amri zake ni zilezile hakuna amri ya kumi na moja aliyoleta Yesu. Uzinzi ni dhambi na ni mojawapo ya amri kumi bali sijaona kutooa wake wengi ikiwa mojawapo ya amri hizo au Daud na Mussa walitii amri zipi? unabwabwaja eti mioyo ya watu ilikuwa migumu kwa hiyo mioyo ya kizazi hiki cha nyoka ndio laini?huna upeo usijihangaishe kuleta ngonjera binafsi hujibu hoja unaleta mawazo yako ya kuliona agano jipya ndio neno la mungu. Hiki ni kizazi wanaume kwa wanaume wanaoana tena kwa ndoa makanisani bila kuonyesha ushahidi wowote wa kiblia na unaona ndio kizazi chenye mioyo laini ya kuoa mke mmoja. Nayo amri kuu ni hii: mpende bwana mungu wako kwa moyo wako wote na mpende jirani yako. Kuoa kunavunjaje amri hii? kumzini mtu au mke wa mtu unamuumiza jirani, yeye mwenyewe kwa kuwa unamtumia kiubinafsi; lakini kuoa na kulea familia na kutendeana mazuri sioni inavyomuathiri jirani
 

hutakaa uibadilishe kweli... mbulula ni wewe unayelazimisha dhambi kuwa si dhambi kwa maandiko i believe in Jesus and what he tought . endelea na imani yako
 
hutakaa uibadilishe kweli... mbulula ni wewe unayelazimisha dhambi kuwa si dhambi kwa maandiko i believe in Jesus and what he tought . endelea na imani yako
Hivi nini maana ya kusema askofu au mzee wa kanisa anatakiwa kuwa na sifa ya kuwa mume wa mke mmoja? kama hiyo ni sifa adimu kiasi hicho je bado inamaanisha ndani ya kanisa hakuna waume za wake wengi? au tuseme mtu atazuiwa kuokoka au kumfata yesu kwa kuwa ana wake wengi? waweza kuniambia wanafunzi wa yesu walikuwa na wake wangapi? je kuoa na kuolewa kilikuwa kigezo katika huduma yao? mimi si mtu wa kuelewa ujinga na kufata kama kondoo mambo ambayo hayapo.
 

embu soma mathayo 19:1-9 na Marko 10:2-12 uone hata Yesu alivoikataa talaka ambayo imani zingine zinaruhu na alisisitiza "na hao wawili wtakua si wawili tena bali mwili mmoja" hakuna sehemu Yesu alisema na hao wengi watakuwa si wengi tena bali mwili moja wala na hao watano watakuwa si watano tena bali mwili mmoja. wawili alimaanisha mke na mume full stop. sio mume na wake.

ndo maana alisema alichokiunganisha Mungu mwanadamu asikitenganishe, lakini dunia ya leo tumekaidi na talaka zipo za kumwaga ndoa imekuwa km mchezo siku hizi hata watu wanaishi miezi wanaachana. Salim bwana wewe amini unachoamini ila ipo siku kila goti litapigwa na kila mtu atahukumiwa sawa sawa na matendo yake. acha tuishie hapa. good evening. amini unacho amini.
 
Hapa ni hoja tu hakuna cha imani na wengine wanataka kuelewa; jibu hoja je Mussa alikuwa mwongo? Daudi anakuwaje bado kipenzi cha mungu? wanafiki wanapenda sana kung'ang'ania dhambi moja wakati kupitia hiyo wanatenda zingine kumi na kuwakosesha watu. Kama una shida na ulimwengu usio na dhambi hata moja sio huu na ujue dhambi unazofanya zinawazidi wengi walioowa wake wengi. Unashikilia jambo na kujihukumu kuwa uko sawa wakati boriti limechuchumaa ndani ya jicho lako.
 

wapi salim nimekwambia sina dhambi au nataka ulimwengu usio na dhambi? maandiko yanasema watu wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu ndo maana wakristo tunaamini kuwa Yesu alikuja kuukomboa ulimwengu na alikufa kwa ajili yetu sisi wenye dhambi ili tuokolewe na alikufa na damu yake ilimwagika ili kuleta patanisho kati yetu na Mungu ndo mana kila siku tunatubu. na tumepewa nafsi inayotuukumu sisi wenyewe yani bila hata hujaambiwa hili ni kosa unakuta unahukumiwa moyoni kwamba hapa umekosa mtu unamwangukia Mungu kwa toba. na pia maandiko yanatuambia zamani zile za dhambi za ujinga Mungu alijifanya hazioni sasa akatuletea Yesu Kristo kama patanisho na yeye. nina kazi tu ila tungeanza kuchambua maandiko
 
na ujue mtu kuwa na dhambi haimaniishi Mungu hakupendi au wewe sio mpenzi wa Mungu Mungu anaichukia dhambi na sio mwanadamu ndo maana maandiko yanasema kwa jinsi hii Mungu "aliupenda Ulimwengu hata akamtoa mwanawe wa pekee ili kila amwaminie asipotee bali awe na uzima wa milele" kw maana hiyo ukitenda dhambi unapotea ndo maana akaja mkombozi so Mungu anatupenda hata kama tukitenda dhambi ndo maana ni vyema kutubu ukijua umetenda dhambi na maandiko yanasema hakuna aliye mwema ila mmoja tu, ambaye ndiye Mungu. so we are all sinners sema tunaishi kwa neema ya Mungu.
 
na sijang'angania dhambi moja ila ni issue iliojitokeza hapa tukaidiscuss hiyo moja iliokuja lakini dhambi ni nyingi na hata ukiziorodhesha haziwezi kuisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…