Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,397
Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura amesema kuwa mfumo wa Ligi Kuu ya soka nchini kujumuisha timu 20 utatumika kwa msimu wa 2019/20 pekee
Kwa msimu wa 2020/21 timu zitapungua na kubaki 18
Msimu wa 2021/22 timu zitapungua na kubaki 16
Wambura amesema kwa msimu huu zitashuka timu nne moja kwa moja daraja la kwanza, zitakazo kuwa nafasi ya 17, 18, 19 na 20 huku timu zilizoshika nafasi ya 15 na 16 zikicheza mchujo na mbili za daraja la kwanza
Aidha, utaratibu wa kupanda Ligi Kuu kwa timu za daraja la kwanza utakuwa vile vile kwa vinara wa makundi yao mawili kupanda moja kwa moja huku watakaomaliza nafasi ya pili kwenye kila kundi wakicheza mchujo
Je, ni uthibitisho wa kuwa tumefulia?