Ligi Kuu Soka Tanzania Bara 28 Dec 2016: Yanga Sc 4 Ndanda FC 0

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
51,986
114,301

=> Dk 1, mechi inaanza kwa kasi kubwa ikionekana Yanga wamepania kupata bao la mapema.

=> GOOOOOO Dk 4, Ngoma anaiandikia Yanga bao saafi kwa kichwa baada ya kuunganisha mpira wa kona

=> Dk 5, Juma Abdul anaachia mkwaju mkali kabisa hapa, goal kick

=> Dk 8, Martin anawachambua mabeki wawili wa Yanga, anapiga krosi safi kabisa. Kidogooo, Tambwe anachelewa

=> Dk 9 sasa, kwa hali ilivyo, Ndanda wanalazimika kubadilika, la sivyo watafungwa tena, maana wanaachia upenyo kwa Yanga kupenya mara nyingi kwenye lango lao huku wao wakishindwa kabisa kumiliki mpira muda mrefu

=> Dk 13, Kiggi Makasi anapiga mpira wa faulo, shuti kali kabisa hapa lakini Dida anadaka vizuri

=> Dk 13, martin wa Yanga anaingia vizuri, anajaribu kupiga shuti lakini kipa wa Ndanda anaonyesha umahiri hapa
=> Dk 15, Ndanda wanapata kona yao ya kwanza, inachongwa na Ngalema, hatari hapa lakini Yanga wanaokoa

=> Dk 19 sasa, Yanga inaendelea kupambana vizuri na mambo yanaonekana si mazuri kwa Ndanda

=> GOOOOOOOOO Dk 21, Ngoma anaandika bao la 37 kwa Yanga msimu, la pili kwake leo baada ya kuunganisha krosi safi kabisa kutoka kwa Juma Abdul ambayo ilimparaza beki wa Ndanda na kumfikia yeye aliyeupiga mpira na kutinga wavuni
=> Dk 24, Yanga wanagngena vizuri, Niyonzima anawachambua mabeki wa Ndanda na kuachia shuti kali, lakini kipa anadaka kama nyani
=> GOOOOOOOO Dk 25, pasi safi, Tambwe anatulia na kuandika bao safi kabisa

=> KADI Dk 26, Tambwe analambwa kadi kwa ushangiliaji wake usiokuwa wa kiungwana, aliruka na kukanyaga kibendera kikavunjika

=> Dk 30 sasa, kipa wa Ndanda alikuwa anatibiwa kwa dakika mbili. Ameamka pale, mpira unarejea mchezoni

=> Dk 32, Yanga wanagongeana vizuri tena, Mwinyi anampa Martin pembeni, anapiga krosi lakini mabeki Ndanda wanaokoa.

=> Dk 34, shuti kali la mpira wa adhabu la Kiggi, linadakwa kwa ulaiiniiii na Dida

=> Dk 39, Kipa Ndanda Jeremiah anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira wa krosi kichwani mwa Tambwe

=> SUB Dk 40 Ndanda wanamtoa Salvatory Ntebe na kumuingiza Ayoub Shabaan

=> Dk 44, Yanga wanafanya shambulizi kali, Msuva anaingia vziuri lakini Ndanda wanaokoa

=> Dk 45, Yanga wanafanya shambulizi jingine, safari hii Ngoma anapiga shuti, wanaokoa. Mwamuzi anasema ni offsise

MAPUMZIKO DAKIKA 3 ZA NYONGEZA

=> Dk 46, mpira unaana na Yanga wanaonekana bado kuwa na uchu...

=> Dk 47, krosi safi ya Juma, Tambwe anaunganisha kichwa, Ndanda wanaokoa, mpira unakuta Martin anaachia shuti kali kabisa hapa, goal kick

=> Dk 49, Yanga wanapata kona, inachongwa vizuri kabisa hapa. Ngoma akiwa katika nafasi nzuri anapiga kichwa juuu

=> Dk 51, krosi safi ya Niyonzima, anapiga krosi safi, Tambwe anapiga lakini mpira unatoka nje

=> SUB Dk 53, Abuu Ubwa anakwenda nje na nafasi yake inachukuliwa na Salum MineliDk 52, krosi nyingine safi ya Msuva, lakini Tambwe anajichanganya mwenyewe mpira ukiwa mguuni

=> Dk 55 sasa, inavyoonekana, Ndanda hawana shambulizi lolote kali langoni mwa Yanga.

=> SUB Dk 60 Yanga wanamtoa Said Juma 'Makapu' na nafasi yake inachukuliwa na Justice Zulu maarufu kama Mkata Umeme

=> Dk 62, Yondani anaondoa mpira ndani ya eneo la 12 la lango lake lakini yeye na Rifat Hamisi wanaanguka. Wote wawili wanatibiwa hapa

=>Dk 68, Yanga inaendelea kutawala mpira kwa asilimia kubwa

=> SUB Dk 70, Thabani Kamusoko anaingia kuchukua nafasi ya Haruna Niyonzima

=> Dk 73, Omary Mponda anaachia mkwaju mkali kabisa hapa wa adhabu lakini Dida anadaka vizuri kabisa

=> SUB Dk 78, Yanga wanamtoa Emmanuel Martin na nafasi yake inachukuliwa na Deus Kaseke

=> Dk 80, Ndanda wanaingia vizuri, Kiggi anapiga krosi safi, kona. Hii ni kona ya pili ya Ndanda katika mechi hii, inachongwa na Mtama hapa, hakuna kitu

=> Dk 83, Jeremiah, kipa wa Ndanda FC anaonyesha umahiri mkubwa kuokoa mpira wa kichwa wa Msuva akiunganisha krosi

=> Dk 86, Yanga wanaendelea kutawala huku Ndanda wakiwa hawana matumaini hata ya kupata bao moja tu

=> Dk 87, Yanga wanapata koa yao ya sita leo baada ya NGalema kuiwahi krosi ya MSuva. Ila Ngalema yuko chini pale

=> Aliungainisha mpira wa kona

=> GOOOOOOO Dk 88, Bossou anaiandikia Yanga bao la nne, likiwa ni bao la 39 la Yanga msimu huu katika Ligi Kuu Bara na la pili kwake msimu huu.

=> Dk 90, Ndanda wanafanya shambulizi kali hapa, Dida anaokoa

DAKIKA 3 ZA NYONGEZA

MPIRA UMEKWISHA

Yanga Sc 4 Ndanda FC 0
 
Dah.. Hizi habari hua zinavuruga kabisa siku yangu.. Ila still bado na imani kubwa na wanakuchere.
 
45'

Sasa ina maana hela za mikia zimeenda bure?au hawa Ndanda watarudisha?Mikia wameliwa hapa. . Haya Yondani anampasia Niyo anauruka kwake Abdul anaachia mkwaju mkali sana Njeeeeee.

Yanga 3 - Ndanda 0
 
Back
Top Bottom