Mkuu,Spain kuna Barca na Real, German kuna Bayern na Borussia wakati England kuna Liverpool,Arsenal,Chelsea Man u,Man city na Italy Kuna Juve,Milan,Inter na Roma.Timu zote hizo nilizotaja ni dominant kwenye ligi zao na zinaweza kukutana zenyewe na ukapata matokeo yoyote. Sasa hapo unaweza ukajua ni ligi gani ngumu kwa kuangalia ni timu ngapi kutoka kila nchi zenye ubavu wa kucheza na yeyote kati yao
Usidanganyike bado ligi bora duniani ni EPL kwa kila kitu
Hah hah hah hah mkuu hiyo ni moja tu ya kufahamu ubora wa ligi ya nchi.Naona umeshaanza kuwa kigeugeu baada ya timu za Spain kupewa kipigo cha aibu
Mkuu The Boss hata hivyo mada inahoji ipi ligi bora kwa msimu huu.?
na kama kigezo cha ligi bora ni kutoa mchezaji bora wa dunia, iweje hapo kwenye orodha yako utangulize b.liga wakati la liga ndio imetoa mchezaji bora.?
Na kama unasema serie a ndio ligi bora, unaongelea ubora upi ikiwa zaidi ya miaka 15 inapitwa na na la liga kutoa mchezaji bora wa dunia.?
mkuu nahitaji ufafanuzi wako wako wa ziada.!!
Soma vizuri nilivyosema na kuelewa nilichosema. Sijataja ligi gani bora katika sentesi yangu. Nilichokuwa nataka kusema ni simply kuwabeza wale waliokuwa wanadai La Liga ni ligi bora kuliko EPL kwa vile waliingiza timu 3 katika robo fainali ya UCL mwaka huu wakati EPL haikuwa na hata timu moja. Na kukurahisishia maoni yangu ligi bora ni ile yenye ushindani mkubwa, ligi ambayo matokeo ya mechi hayatabiriki timu ndogo (toka daraja la chini) inaweza kuipa kipigo timu kongwe, ligi ambayo toka mwanzoni mwa msimu huwezi kutabiri timu gani ( zaidi ya mbili) itabeba kombe. Katika ligi ya Spain tunajua bingwa atakuwa either Barca au Real Madrid. EPL inapoanza huwezi kutabiri nani atabeba kati ya Manchester utd,Chelsea au Manchester city (kwa sasa) na bado kuna kina Arsenal, Tottenham, Liverpool,Everton ambao wanatoa ushindani kwa hizo timu tatu kugombea nafasi za UCL au hata kunyemelea kuchukuwa kombe kwa miujiza ( keyword Miujiza). kwa kifupi EPL kwangu ni ligi bora kiushindani, ila kitechnical naweza kusema La liga ipo juu.Mkuu rubaman, Kwa kigezo chako ulichotumia wala hakina maana yoyote na inaonyesha kabisa wewe sio moenzi wa Soka la ukweli bali ni ushabiki tu, kwa vigezo vyako basi EPL ndio ligi bora, maana ilishazipeleka fainal Chelsea na Man U, na kisha Chelsea alizifunga Barca nusu fainal na kisha Bayern Fainal
mi nadhani unachanganya timu bora na ligi bora, Think think
Soma vizuri nilivyosema na kuelewa nilichosema. Sijataja ligi gani bora katika sentesi yangu. Nilichokuwa nataka kusema ni simply kuwabeza wale waliokuwa wanadai La Liga ni ligi bora kuliko EPL kwa vile waliingiza timu 3 katika robo fainali ya UCL mwaka huu wakati EPL haikuwa na hata timu moja. Na kukurahisishia maoni yangu ligi bora ni ile yenye ushindani mkubwa, ligi ambayo matokeo ya mechi hayatabiriki timu ndogo (toka daraja la chini) inaweza kuipa kipigo timu kongwe, ligi ambayo toka mwanzoni mwa msimu huwezi kutabiri timu gani ( zaidi ya mbili) itabeba kombe. Katika ligi ya Spain tunajua bingwa atakuwa either Barca au Real Madrid. EPL inapoanza huwezi kutabiri nani atabeba kati ya Manchester utd,Chelsea au Manchester city (kwa sasa) na bado kuna kina Arsenal, Tottenham, Liverpool,Everton ambao wanatoa ushindani kwa hizo timu tatu kugombea nafasi za UCL au hata kunyemelea kuchukuwa kombe kwa miujiza ( keyword Miujiza). kwa kifupi EPL kwangu ni ligi bora kiushindani, ila kitechnical naweza kusema La liga ipo juu.
Kwa hiyo Mkuu unataka kusema Barcelona na Madrid huwa hawafungwi na team za chini yao? Ukisema Spain washindi ni predictable (RM au Barca) halafu ukasema EPL huwezi kujua nani atachukua kati ya Man Utd, Man Cty au Chelsea, huoni kama unaongea kitu kilekile ila tu kwa EPL kuna team 3 na La Liga 2?
Nadhani kati ya timu 3 ni vigumu ku predict ipi itachukuwa kombe kuliko kati ya timu 2. Odds za atakayechukuwa Kombe Spain ni 50/50 kati ya Wababe wawili, wakati EPL odds ni less ya hizo za la liga. Ndio hata Spain Barca na Real wanafungwa na timu ndogo lakini ni mara chache sana kutokea ukilinganisha na England.
Still ni kitu kilekile, kujua kwamba kati ya hizi tatu au hzi mbili mmoja atakua bingwa, bado zote ni pridictable ndio maana kuna kitu kinaitwa big four ndani ya EPL
Misimu kama mi4 iliyopita ligi ambayo ilikua ngumu kutabiri bingwa ilikua Bundasliga pekee, lakini saa hzi nayo kama La Liga na inakoelekea itakua kama ya Scotland
Nadhani kila ligi ina wababe wake, wawe wa3, wa2, it doesn't matter, ndio maana kila team inakuaga na target mwanzoni mwa ligi, huwezi kuwasikia Totenham au Everton au Liverpool (ya sasa) wameweka malengo ya Kuchukua Ubingwa wa ligi, hata kama watamfunga Man Utd goal 5
Ligi bora duniani ni EPL. Mie huwa naflip channels kuangalia mechi katika ligi zote ili kuamua nitulie wapi kwenye kandanda la uhakika na mara nyingi huamua kuangalia EPL. EPL haitoi mchezaji bora duniani, Timu ya Taifa ya UK si nzuri ukilinganisha na timu za mataifa mengine lakini hizo si sababu za msingi za kudai EPL si ligi bora duniani. Hata kwenye kuingiza mapato kupitia matangazo ya kibishara ya makampuni mbali mbali duniani, EPL inaziacha mbali ligi nyingine.
Ligi bora duniani ni EPL. Mie huwa naflip channels kuangalia mechi katika ligi zote ili kuamua nitulie wapi kwenye kandanda la uhakika na mara nyingi huamua kuangalia EPL. EPL haitoi mchezaji bora duniani, Timu ya Taifa ya UK si nzuri ukilinganisha na timu za mataifa mengine lakini hizo si sababu za msingi za kudai EPL si ligi bora duniani. Hata kwenye kuingiza mapato kupitia matangazo ya kibishara ya makampuni mbali mbali duniani, EPL inaziacha mbali ligi nyingine.
EPL ni 'the most watched' ligi duniani
but sio bora....
Ubora wa kitu huthibitika kwa demand ya kile kitu kuwa kubwa kuliko vitu vingine vinavyofanana na bidhaa ile. Hivyo hiyo ya kuangaliwa na watu wengi ni uthibitisho kwamba wapenzi wa soka duniani wanapenda kuiangalia ligi hiyo kuliko yoyote ile nyingine duniani. Kila mwaka mie hujaribu kuangalia michezo ya ligi yote lakini kama mpenzi wa soka ligi ya UK haina mpinzani duniani kutokana na ubora wa kandanda katika ligi hiyo.
Premier League to Remain Worlds Richest Soccer League After Auction Lands Record TV Deal | Chelsea FC | NESN.com
Ubora wa kitu huthibitika kwa demand ya kile kitu kuwa kubwa kuliko vitu vingine vinavyofanana na bidhaa ile. Hivyo hiyo ya kuangaliwa na watu wengi ni uthibitisho kwamba wapenzi wa soka duniani wanapenda kuiangalia ligi hiyo kuliko yoyote ile nyingine duniani. Kila mwaka mie hujaribu kuangalia michezo ya ligi yote lakini kama mpenzi wa soka ligi ya UK haina mpinzani duniani kutokana na ubora wa kandanda katika ligi hiyo.
Premier League to Remain World's Richest Soccer League After Auction Lands Record TV Deal | Chelsea FC | NESN.com
Inaweza kuwa inaangaliwa sana kwa sababu ya accessibility yake na sio demand, inaweza kuwa kwa sababu ya Promo nyingi na sio demand na bado wanaosema kuwa EPL ndio inawatazamaji wengi wanaweza kuwa ni watu wa promo tu.