Ambiele Kiviele
JF-Expert Member
- Dec 29, 2014
- 15,270
- 29,939
Asilimia kubwa watu wengi wenye vipaji hawana elimu na watu wenye elimu bora hawana vipaji,wakati kipaji kinapokupa utajiri ambao elimu haiwezi kukupa.
Tofauti kati ya Elimu na Kipaji ni kwamba Elimu ni hazina ya milele wakati kipaji huwa hakidumu milele.Kwa wale wapenzi na wafuatiliaji wa music watakuwa wanakumbuka mwanamuziki Stanley Kirk Burrel ,aliyekuwa anafahamika kwa jina la MC Hammer.
MC Hammer ,mwaka 1991 alikuwa na utajiri wa $33 million ambayo ni sawa na Billion 75,091,629,130.29 za kitanzania,kisha mwaka1996 alikuwa anadaiwa kiasi cha $13 million ni kipindi cha miaka mitano pekee.
Mc Hammer kipaji kilimpa pesa ila alikosa elimu na maarifa ya kuitunza pesa katika uwekezaji na njia stahiki za kuindeleza,baadaye alifilisika kabisa kwa muda wa miaka mitano pekee.
Pale nchini Ujerumani katika mji wa Dortmund, North Rhine-Westphalia ,kijana mwenye asili ya Uturuki anayefahamika kwa jina la Nuri Şahin ,tarehe 26 April alifanikiwa kupata admission ya kujiunga na chuo bora Duniani Harvard University Business School ,kusomea Degree ya Sports Management.
Kijana aliyezaliwa 5 September 1988 ,kwa sasa ana umri wa miaka 29 na utajiri wa $11 Million bado ana njaa ya kuwekeza kwenye maarifa kupitia elimu sababu hataki yamtokee yaliyo mtokea Emmanuel Eboué,MC Hammer na Mike Tyson.
Namuona Ngasa akihama timu kila uchwao wakati kipaji chake kimefika ukomo ila ubongo wake bado unahitaji elimu na bado ni kijana mdogo ambaye anaweza kujiendeleza kielimu wakati pale kipaji kinapofikia tamati.
Pale Harvard Business School kuna mwana mama anayeitwa Professor Anita Elberse, yeye ni kungwi au fundi wa kufundisha masomo ya Entertainment, Media pamoja na Sports sectors,Nuri Şahin atakuwa chini ya huyu mama akisoma huku account yake Bank inasoma $11 Million
Wakati sisi tunasomea mishahara wenzetu wanasomea utashi na maarifa yaani ana pesa kisha anasoma,Degree bora ni ile unayosomea maarifa na sio kusomea cheti.
Life is a school of living education.
You rise if you past the test.
You fall if you fail the test
[emoji407][emoji432][emoji388][emoji389][emoji460]️[emoji460]️#