Lifahamu tatizo la Misophonia

Lifahamu tatizo la Misophonia

Huyu Mimi

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2019
Posts
2,575
Reaction score
2,122
MISOPHONIA

Hii ni neno la kitaalam likiwa na maana ile hali mtu anakasirika au anakerwa na vitu vidogo mfano mtu kutafuna kwa sautii , kupumua kwa sauti karibu na mtu, sauti ya mtu akisugua au kutafuna meno. Ishawahi kukukuta yaani mtu anapumua halafu wewe unajiisikia vibaya? Ama mtu anatafuna kwa sauti halafu ukakereka? Basi hii ndio wanaita misophonia.


• Mtu unakuta akisikia tu hivyo anapatwa na hasira sana na huwa anaboeka na kushindwa kuvumilia inadaiwa ikiendelea sana anaweza kumpiga mtu na chochote kile kilichokaribuu. Wengine hulia tuu na kujisikia vibaya na kupatwa hasira na kuachia yoweee za kutopendezwa na sautii hizoo.

• Ulishawahi kupatwa na hali hii??

Basii jua una tatizo hilo la misophonia

Kitaalam wanasema haina dawa yaani hata ukienda hospitali watakushaurii tuuh na kukupa mbinu mbalimbali za kujikinga na kuikabiri hali hii.

• Ila huwa kuna baadhi ya njia huwa wanashauri kutumia mfano kuepuka sehem zeny mrundikano wawatuu , kuepuka na kuondoka eneo la tukio, kuvaa ear phone ili kuepuka sauti hizo .

• Misophonia inatesa sana kama hujawahi kupata basii huwez jua kile anachokisikia mtu mweny tatizo hilo. Hapa ndo wanasemaga kitanda usicholalia hujui kunguni wake

Wajuvi Muongezee
 
Hili tatizo nafikiri ninalo

Kuna mmoja nilikutana nae hospital...alikuwa anakunywa soda sasa kila 'puff' analopiga lazima abeuwe!imagine inavyokera
Hatarii Saana Au Mtu anakula Mdomo uko wazi
 
Kama ugonjwa huu unaua basi na mimi nimo kwenye list ya wagonjwa sugu
 
Hahhah Sijajua kama Unaua Ila una athari zake Kisaikolojia mtu anakua hayupo sawa.
wale wotw wenye ghubu yaani kila kitu ni kulalamika tuu hata kidogo, yaani mtu anafanya kitu kidogo kwa bahati mbaya basi wewe ni kurudia rudia unalaumu tuu!!!! hawa nao ni wagonjwa sugu
 
wale wotw wenye ghubu yaani kila kitu ni kulalamika tuu hata kidogo, yaani mtu anafanya kitu kidogo kwa bahati mbaya basi wewe ni kurudia rudia unalaumu tuu!!!! hawa nao ni wagonjwa sugu
Hhahahhahha Kabisaa Yaaani
 
Harufu ya kinywa kinachotafuna karanga, sauti ya mtu anayekoroma usiku usipime, harufu ya kinywa kilichotafuna kitunguu swaum.
 
Back
Top Bottom