Jackwillpower
JF-Expert Member
- Oct 4, 2017
- 2,539
- 3,860
Jiwe la Moabu
katika mwaka wa 1868 kule Diboni, Yordani kulipatikana jiwe lifaamikalo kama Moabite Stone, lililogunduliwa na mwana Akiolojia na Mmishionari wa Ujerumani Klein. Jiwe hili linathibitisha vita ya wa Moabu dhidi ya Israeli kama ilivyoandikwa katika 2Fal 2 na 3.
Kati ya shuhuda za kiakiolojia za kabila hili la wa Moabu ni Jiwe la Mesha, linaloeleza ushindi wao dhidi ya mwana wa Mfalme Omri wa Israeli.
Jiwe hili lilikutwa limeandikwa maneno haya;
“Mimi ni Mesha […] Mfalme wa Moabub […] Omri alikuwa Mfalme wa Israeli, na akawatesa Moabu Moabu […]Nilichukua kutoka humo vyombo vya Yehova […] ilihali nyumba ya Daudi ilimiliki Horonaimu."
Jiwe la Moabu ni maelezo ya matukio yanayofanana na 2 Wafalme sura ya 3. Watu kadhaa wa Biblia na mahali hutajwa:
Jiwe la Moabu lilikuwa na umri unaokaribia miaka 3,000. Ni kipande cha jiwe la basalti jeusi lililosuguliwa likiwa na upande wa juu ulioviringishwa vizuri, lilikuwa na kimo cha karibu mita 1.2 likipita kidogo tu upana wa meta 0.6, na likiwa na unene unaokaribia meta 0.6.
Sent using Jamii Forums mobile app