Moabu , "Mbegu ya baba"; ni jina la kihistoria la eneo la milimani upande wa mashariki wa
Bahari ya Chumvi ndani ya nchi ya kisasa ya
Yordani. Ilikuwako kati ya
Edomu upande wa kusini na
Amoni upande wa kaskazini.
Zamani eneo hilo lilikuwa
ufalme wa
Wamoabu. Mji wake mkuu uliitwa
Diboni na maghofu yake yapo karibu na mji wa
Dhiban wa kisasa.
Sawa na Isreli Moabu ilikuja chini ya mamlaka kwanza ya
Ashuru na baadaye ya milki ya
Babeli. Mwaka 582 KK mfalme
Nebukadnezzar II wa Babeli alifanya Moabu kuwa sehemu ya milki yake; hivyo ilikuwa sehemu ya ufalme wa
Uajemi baadaye. Wakati wa utawala wa Kiajemi Moabu ilipotea kama taifa la pekee. Makabila ya Waarabu walianza kuingia na kukalia sehemu kubwa za nchi na wakazi waliacha lugha yao wakatumia Kiaramu badala ya lugha yao ya awali
Jiwe la Moabu
katika mwaka wa 1868 kule Diboni, Yordani Kulipatikana jiwe lifaamikalo kama MOABITE STONE lililogunduliwa na mwana akiolojia na mmishionari wa ujerumani
Klein,
Jiwe hili linathibitisha vita ya wa moabu dhidi ya Israeli kama ilivyoandikwa katika
2Fal 2 na 3.
Kati ya shuhuda za ki
akiolojia za kabila hili la wa moabu ni
Jiwe la Mesha, linaloeleza ushindi wao dhidi ya mwana wa mfalme
Omri wa
Israeli.
JIWE HILI LILIKUTWA LIMEANDIKWA MANENO HAYA
“Mimi ni Mesha […] mfalme wa moabub […] Omri alikuwa mfalme wa Israeli, na akawatesa moabu Moabu […]Nilichukua kutoka humo vyombo vya Yehova […] ilihali nyumba ya Daudi ilimiliki Horonaimu
Jiwe la moabu ni maelezo ya matukio yanayofanana na 2 Wafalme sura ya 3. Watu kadhaa wa bibilia na mahali hutajwa:
Jiwe la MOABU Lilikuwa na umri unaokaribia miaka 3,000. Ni kipande cha jiwe la basalti jeusi lililosuguliwa likiwa na upande wa juu ulioviringishwa vizuri, lilikuwa na kimo cha karibu meta 1.2 likipita kidogo tu upana wa meta 0.6, na likiwa na unene unaokaribia meta 0.6.