barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,870
Hii nimeiona kwa Mbunge mmoja wa UKAWA....na hii inaleta picha kuwa hata huko UKAWA kuna watu washakula chao hivyo CCM wamepelea kura moja ambayo ndio wanataka kulazimisha itimie.Maana kura nyingine wanajuaa watazipata ndani ya UKAWA,maana hongo inamwagwa ni balaa toka juzi.Masterminded ni yule jamaa aliyekuwa Meya wa Jiji maana anajuwa atafungwa saa mbili asubuhi tu endapo Umeyor utabebwa na mtu mwingine.
Nimetoka kwenye kikao muda huu na viongozi wa CUF na CCM cha Mkurugenzi wa manispaa ya ILALA.
Agenda yake ilikuwa ni kuongeza jina la Mbunge wa viti maalum 1 anayeitwa Stella Ikupa.
Mwanasheria kaja na vielelezo juu ya mchakato wa mbunge uyu kuwa ulianzia ILALA/DSM.
Tumeweka msimamo kuwa hakuna mjumbe yeyote ataweza kuongezwa kwa wakati huu.
CCM wamesema uyo mjumbe wao yupo na atafika kwenye kikao cha uchaguzi kwa sababu ni mjumbe halali.
Wameenda mbele zaidi kumtuhumu mwanasheria wa Halmashauri kupindisha sheria kwa lengo la kuwanyima haki,bila aibu wamekana makubaliano yetu ya awali juu ya kuwaruhusu wabunge Anatropia na Sophia Simba kama wajumbe,
Wanadai mkurugenzi hakuwa na mamlaka hayo.
Mkurugenzi amelazimika kususpend kikao kwa sababu ya hao mabwana,wameonesha uelewa mdogo na ukada uliowapitiliza kiasi cha kushindwa kuelewa hata maelezo yaliyokuwa wazi.
My take.
Tujipange vizuri kupambana na hawa jamaa inaonekana bado hawajakata tamaa.
Ilala tumewagomea khali ikoje uko temeke?inaonekana wanashawishi wakurugenzi ku ingiza list mpya ya wapiga kura.