Libermann School, Mnawanyanyasa watoto

Wiyelelee

JF-Expert Member
Nov 9, 2012
1,071
347
Karibu wiki nzima hii, nimekuwa namsindikiza mtoto wangu Shule ya Libermann iliyoko Mbezi Beach. Nitaandika kwa kifupi maana nawahi Mkutano. Nimeshuhudia watoto wanaodaiwa ada kuzuiwa nje ya gate, huku wenye gate pass wakipita tu. Nadhani Libermann wangekua wanatoa barua kwa wazazi kuliko kuzuia watoto wanapofika shule maana inawatesa watoto kiakili (Psychological torture). Sioni sababu ya kuwaruhusu wanafunzi kutumia usafiri wa shule halafu wakifika eti unawazuia getini na kubaki nje hadi wenzao wanatoka ndo warudi nyumbani.
Ni muhimu sisi wenye watoto Libermann tuje kulijadili hili kwenye kikao cha wazazi na Uongozi wa Shule

Short but clear for now.
 
Kazi ya dereva ni kuakikisha anachukua watoto wote aliokabidhiwa ktk vituo au maeneo yao na ktk uhalisia sio kazi yake kumdai mtoto au kumuuliza km anadaiwa sch fees.
2.Jukumu la mzazi ni kuakikisha unamlipia ada mwanao kwa wakati na hayo matatzo mzazi anahusika kwa more than 75percent.kama una matatizo kidogo(mzazi)ni jukumu lako kuwasiliana na uongozi wa shule na kuacha kufanya hvyo ni KUTOKUWAJIBIKA KAMA BABA,MAMA AU MLEZI.
NB.MIMI SIO MSEMAJI WA HYO SHULE.
 
Ukiona hivi fahamu ya kwamba mawasiliano kati ya wazazi na Uongozi wa shule si ya kuridhisha. Nina mtoto pale (japo hajarudishwa). Naona kuna tatizo la kimawasiliano.

Tutaushauri uongozi wa shule kuelewa kuwa mawasiliano na wazazi/walezi ni muhimu sana kuliko wanachokifanya.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom