LHRC ni Non-Gorvernmental Organization au Anti-Governmental Organization?

LHRC ni Non-Gorvernmental Organization au Anti-Governmental Organization?

Mkuu, wala haina haja ya kumpeleka the Hague. huyu ni kumnyima tu ya kusema. kila kitu kitaenda shwari na wale vibaraka wake watabanwa kila kona wasiwe na mambo ya kuongea. tuone kama ndoa yao itadumu

wanaoachika kwa waume huwa ni wanawake wenye matatizo sana.
 
Siyo LHRC tu, tunahitaji sauti nyingi zaidi zenye kutoa kauli mbadala, ili tuachane na baggage hii ya "amani na utulivu" wa kijinga ambayo tumeirithi kutoka siasa ya Ujamaa. Ujamaa ulikuwa na mazuri yake mengi sana, lakini tatizo moja ni kuwa na ule "UMOJA KATIKA UJINGA" na "AMANI KATIKA UMASKINI". tunahitaji watu wengi zaidi waseme HAPANA! natiwa moyo sana jinsi ambavyo hilo limekuwa likijitokeza katika jamii ya watanzania, achilia mbali katika vyama vya upinzani na taasisi kama LHRC. Sasa hivi ni kawaida kuona katika TV au kusikia katika vyombo vya habari, wananchi wamefunga barabara kwa kupinga hiki au kile.

Kwa vyama vya upinzani, tunahitaji zaidi na zaidi watu wanaoweza kusema HAPANA kwa maamuzi ya kipuuzi kama yale ya Ndugai. yaani siku nyingine akitaka kufanya uamuzi wa aina hiyo ajiulize mara mbili...sasa inatakiwa hiyo iende mpaka kwa mama kule kijijini ambaye anapata taarifa kwamba binti yake kabakwa na mbakaji anatamba mtaani, watu wamshushie kisago cha mbwa mwizi, ahame kijiji!! maana kwa sasa mama maskini hata akienda Polisi ataambiwa atoe kitu kidogo ndio mtuhumiwa akamatwe. wakimkamata watataka kitu kidogo kutoka kwa mtuhumiwa ili aachiwe, na pia watadai kitu kidogo kutoka kwa mshtaki ili mshtakiwa aendelee kuwekwa chini ya ulinzi. lakini kwa utaratibu mpya wa mahakama za wananchi, thubutu yake...

Kwa hiyo LHRC wanafanya vizuri sana na wanatoa mfano mzuri na mwema kwa vyama vingine kama hivyo, wasiogope makunyanzi ya Wasira (btw yuko nchini huyu jamaa?). kwamba LHRC iko very active ni dalili tosha kwamba hali ya haki za binadamu na utawala wa sheria nchini kwetu ni mbaya sana. na nina uhakika maandishi ya watu kama Mapunda wa Tazama Tanzania hayatawarudisha nyuma akina Sungusia - mmoja wa wanasheria matata sana niliopata kuwaona-sana sana nadhani yatawachochea waongeze nguvu zaidi. kwamba kitendo cha gazeti kama Tazama Tanzania kuwashambulia namna hiyo, ni dalili tosha kwamba kazi yao inaonekana na hivyo waongeze nguvu. Hao ni wapambanaji wanaotumia elimu yao kupambana na uovu, ukandamizaji na uonevu, uje kwa sura yoyote ile wao wanapiga tu. Sio kama wasomi wengi ambao tunatumia usomi wetu kuendeleza sera za ubabe na ukandamizaji...BRAVO LHRC!!!
 
Back
Top Bottom