LESENI ZA UDEREVA TRA NI WAZEMBE.

Kwani ukienda kurenew unaacha ile leseni ya zamani? Mi nimeenda kurenew kama mwezi sasa umepita nikapewa hiyo risiti na nikaondoka na leseni yangu ya zamani, wakaniambia watanitumia sms leseni mpya ikiwa tayari, ingawa mpaka sasa ni kimya. Ila leseni yangu ilikuwa na miezi 11 tangu ilivyoexpire.
 
Hauachi lakini sababu imepita muda wake unaweza iacha nyumbani na kama emergency basi utembee na copy yake!.
 
Waliwahi nikamata na hiyo risiti na hawakuelewa
Ulikuwa na wenge wakajua wamekupata!.. Ukikaza hawana ujanja hata Mkuu wa Trafiki Tz alilitolea ufafanuzi hawatakiwi kukukamata!!..
 
Usitake tuvunje sheria, tueleze kifungu cha sheria kinachoruhusu karatasi ya malipo kuwa mbadala wa leseni ili nasi tukitumie.
Neno langu sio sheria lakini fuatiria Kamanda wa kikosi cha Usalama barabarani alisemaje kuhusu hili!..
 
Kama una magari matatu inakulazimu kutoa copy 3. Dah!
 
Mkuu mpaka leo hii huna ID ya Kupiga kura au ya NIDA?.. Mbona vyote hivi matumizi yake ni aina moja tu!.
Ingawa kwa madereva waomba ajira kweli ni changamoto ila kwa watu wengine card ya Leseni ya Udereva haina maana sana!.
Poleni lakini!.
Kwani NIDA wanatoa vitambulisho? Mimi sijapewa kwa zaidi ya miezi 18!
 
Wewe komaa na risiti ya malipo tuu, hiyo ni leseni tosha. mimi mwezi wa nane sasa natumia risiti na leseni iliyo expire.
 
Hivyo ndio nilivyofanya baada ya kuona walio renew kabla yangu usumbufu wanaopata.Nililipia mwezi wa 7 mwaka Jana nikapata leseni mwz wa 12 mwishoni KBS tena baada ya wao kunipigia simu kuwa iko tayari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…