Jana nilisikia kupitia Radio one kuwa Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani linaangalia uwezekano wa kutumia kanuni inayotaka kila mwenye leseni ya udereva kufanya mafunzo ya siku 5 hadi 7 ili kujikumbusha sheria za usalama barabarani wakati anapokwenda kuhuisha (Renew) leseni yake.
Hili linaweza kuwa wazo zuri; lakini utekelezaji wake unawezekana bila kuleta kero kwa wahusika?
Haya mafunzo yataendeshwa na kikosi cha usalama barabarani au shule na vyuo vya udereva? Kutakuwa na gharama au hakutakuwa na gharama?
Najiuliza kuhusu mafanikio ya huu utaratibu kwa kuwa hata ukaguzi wa magari wiki ya Nenda kwa usalama haufanyiki kikamilifu; Kinachoonekana kutiliwa mkazo ni uuzaji wa stika za kubandika kwenye magari!