Leseni maeneo yasiyoendelezwa kufutwa

Leseni maeneo yasiyoendelezwa kufutwa

diana chumbikino

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
428
Reaction score
368
NAIBU Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amesema serikali inazipitia leseni zote zilizotolewa na wizara hiyo kwa ajili ya utati na wawekezaji na ambazo hazijaendelezwa zitafutwa. Nyongo ametoa kauli hiyo wakati anajibu swali la nyongeza la Mbunge wa Tunduru Kusini, Daimu Mpakate (CCM) aliyetaka kujua serikali ina mpango gani kwa watati waliopewa leseni na hadi sasa maeneo yao hawajayaendeleza ili yakabidhiwe kwa wachimbaji wadogo? Nyongo alisema wizara hiyo imekuwa katika kazi ya kupitia leseni zote za utati na kuangalia hali na utendaji wake na zile ambazo hazifanyiwi kazi na maeneo hayaendelezwi watazifuta.

"Serikali itazifuta leseni zote za watati ambazo wahusika walichukua maeneo ili kufanya utati na hadi sasa hawayajaendeleza," alisema. Akijibu swali la msingi la Mbunge Mpakate aliyetaka kujua ni lini serikali itajenga mtambo wa kuchenjua shaba katika kijiji cha Mbesa, wilayani Tunduru, Nyongo alisema Machi 3, mwaka juzi, serikali iliweka zuio la kusarisha nje ya nchi madini gha na kuelekeza madini yote yaongezwe thamani hapa nchini.

"Zuio hilo lilikuwa na nia njema ya kutaka shughuli zote za uongezaji thamani madini zifanyike hapa nchini ili kuongeza manufaa kwa wananchi na Taifa kwa ujumla kutokana na rasirimali za madini. "Kutokana na zuio hiyo, kwa GN namba 60 ya Januari 25, mwaka huu, serikali imetoa mwongozo wa kuhakiki uongezaji thamani madini na miamba nchini kabla ya madini hayo kupata kibali cha kusarisha kwenda nje ya nchi.” Alisema madini ya shaba yanapatikana katika maeneo mbalimbali nchini, hivyo kwa kuzingatia hilo, serikali imepokea maombi ya kampuni 11 zenye nia ya kujenga vinu vya kuyeyusha madini hayo baada ya kutangaza uwepo wa fursa hiyo.
 
Back
Top Bottom