Leonidas Gama. Jipu lililohamia mguuni kutoka kichwani

idoyo

JF-Expert Member
Jan 13, 2013
3,050
1,402
Kama mnakumbuka hapo nyuma, kambi rasmi ya upinzani katika bunge lililopita ilimtuhumu aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama, kuwa dalali wa ardhi iliyoibua mgogoro huko Holili. Alituhumiwa kuwa ni mmoja wa wanahisa wa Jun Tu Investment Company inayomiliki kiwanda cha sementi iliyomilikishwa ardhi hiyo. Baadaye alikana kila kitu kuhusu uhusika wake.

Leo hii, mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Amos Makalla amekuta kiwanda hicho kinatumia anuani ya ofisi ya mkuu wa mkoa kinyume na sheria. Kwa sasa huyo bwana ni mbunge huko Songea. Jipu limehamia mguuni, litumbuliwe!
 

Attachments

  • WP_20160220_007.jpg
    WP_20160220_007.jpg
    150.5 KB · Views: 59
Utetezi wake

“Historia ya Kiwanda hiki iko wazi, na nililipeleka hadi kwenye kikao cha ushauri wa mkoa (RCC), na naomba nieleweke kwamba, ni juhudi zangu na za mtoto wangu, nilitamka kwenye kikao kile na wala sikuficha, mtoto wangu ambaye ametajwa yeye ana rafiki yake wa kichina, wala si
kweli kwamba hii kampuni mimi nimekwenda kuichukua China kwa gharama za serikali” aliongeza Gama.

Alisema katika kikao hicho (RCC), Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini, Mbunge wa Vunjo, Dkt. Augustino Mrema na Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo, walishiriki katika kikao hicho na kwamba baada ya mvutano ndipo makubaliano yakawa kiwanda kijengwe wilaya ya Rombo .

“Toka siku ile mimi kama mkuu wa mkoa nikakabidhi madaraka wilaya ya Rombo,kwa hiyo shughuli zote za ujenzi ,shughli zote za kutafuta viwanja ziifanywa na halmashauri ya wilaya ya Rombo na sio Gama” alisema Gama.

“Nimeelezwa kweye tuhuma kuwa nimepewa milioni 500, hii ni hadithi ya kisiasa, sijapokea kiasi hicho cha fedha wala sikijui. Hata hizo hisa 20,000 nilizoambiwa ninazo kwa kweli sina. Kama ningekuwa nazo ni haki yangu kwa sabau sijavunja sharia lakini sina hata hisa moja.”alisema
Gama.

“Swala mtoto wangu kuwa na hisa si dhambi na ni haki yake kisheria, kwa
sababu yeye ndiye aliyewatafuta hao watu na ni rafiki zake, wala si
mimi niliyewaleta. Kama amenunua hisa huko ni hiari yake, mimi sina hisa
kama Gama. Sijapokea milioni 500 kama Gama. Mimi si dalali na kama ni
udalali wa ardhi hiyo itakuwa ni halmashauri ya wilaya ya Rombo na si Gama.” alisema Gama
 
Back
Top Bottom