TAKUKURU Kilimanjaro yamfikisha Mahakamani aliyekuwa Mkurugenzi Rombo

Fred Mwakitundu

JF-Expert Member
Dec 31, 2018
227
383
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro,Judethadeus Mboya na aliyekuwa Mwanasheria wa Halmashauri hiyo,Andrew Gregory ,wamefikishwa mahakamani mjini Moshi wakikabiliwa na mashitaka ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia hasara Halmashauri hiyo ya shilingi Milioni 226.689,700 .

Shauri hilo la uhujumu uchumi namba 1/2019 limefikishwa leo mahamani katika mahakama ya hakimu mkazi ambako washitakiwa hao walisomewa mashitaka yao na mwendesha mashitaka kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru),Suzan Kimaro.

Kwa mujibu wa hati ya mashitaka washitakiwa hao kwa pamoja wanashitakiwa kwa kosa la kutumia mamlaka yao vibaya kwa kuingia mkataba usio na tija kwa Halmashauri hiyo wa kuipangisha Ardhi Kampuni ya Jun Yu Investment International kinyume na kifungu cha 31 cha sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007.

katika shitaka la pili,Mboya akiwa Mkurungenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Rombo na na Gregory akiwa Mwanasheria wa Halmashauri hiyo kwa pamoja waliisababishia hasara kwa makusudi Halmashauri hiyo ya shilingi Milioni 226,689,700.

Washitakiwa baada ya kusomewa mashitaka yao hawakutakiwa kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kusikiliza mashauri ya uhujumu uchumi hadi mahakama maalumu ya makosa ya ufisadi na hivyo wakapelekwa mahabusu katika Gereza Kuu la Mkoa la Karanga,

Uchunguzi wa Takukuru unaonyesha kwamba washitakiwa hao walitumia fedha za Halmashauri shilingi Milioni 226,689,700 kuwalipa fidia wamiliki wa ardhi yenye ukubwa wa Ekari 25 katika mji mdogo wa Holili wilaya ya Rombo badala ya fedha hizo kutolewa ama kulipwa na Kampuni ya Jun Yu Investment International .

Kwa mujibu wa uchunguzi wa Takukuru,baada ya eneo hilo kupatiikana,washitakiwa hao kwa niaba ya Halmashauri waliingia mkataba na Kampuni hiyo inayomilikiwa kwa ubia na watu watatu akiwamo mtoto wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas Gama aitwaye Muyanga Leonidas Gama kwa ajili ya ujenzi wa Kiwanda cha Saruji.

Wabia wengine katika Kampuni hiyo ni raia wawili wa Kichina ambao ni Wang Zhigang na Feng Hu.

"Aidha uchunguzi wetu unaonyesha kuwa mkataba huo wa miaka 99 haukuwa na tija kwa Halmashauri ya wilaya ya Rombo",inasema taarifa ya Takukuru iliyotolewa leo na Mkuu wa Takukuru mkoa wa Kilimanjaro(RBC),Holle Makungu.

Takukuru imetoa wito kwa watumishi wa umma kutojiingiza kwenye shughuli zenye mgongano wa maslahi na majukumu waliyopewa na kusisitiza pale maslahi binafsi yanapokinzana na maslahi ya umma katika utekelezaji wa majukumu ya umma,kipaumbele kiwe maslahi ya umma.

Taasisi hiyo imeonya kuwa,kwa wale watumishi ambao wataendelea kukaidi na kuweka mbele maslahi binafsi watashitakiwa kwa matumizi mabaya ya ofisi kinyume na kifungu cha 31 cha sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya Mwaka 2007.
 
Washitakiwa baada ya kusomewa mashitaka yao hawakutakiwa kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kusikiliza mashauri ya uhujumu uchumi hadi mahakama maalumu ya makosa ya ufisadi na hivyo wakapelekwa mahabusu katika Gereza Kuu la Mkoa la Karanga,


Sasa walipelekwa hapo kutafuta nini kama tangu mwanzo walijua mahakama hiyo haina uwezo wa kuisikiliza kesi hiyo!
 
Back
Top Bottom