Dr Matola PhD
JF-Expert Member
- Oct 18, 2010
- 56,608
- 93,384
Wapendwa waumini wakatoliki wenzetu Tumsifu Yesu Kristo. Asanteni sana kwa michango yenu kuhusu group letu na changamaoto mnazoziona. Leo kulikuwa na post ya mmoja ambaye ameeleza changamoto anazoziona kwa maadmins, kama kuchelewa kuachia posts za watu wanazotuma, kuachia posts ambazo zinaitwa za kichochezi, za madhehebu yanayokashifu ukatoliki, nk. Mmoja kasema labda group halikuanzishwa na wakatoliki bali wapinga Kristo. Ndugu zangu, mimi ni mmoja kati ya maadmins wa group na kati ya waanzilishi wa mwanzo wa group tukiongozwa padre Revocatus Paul. Mimi mwenyewe pia ni padre. Hivyo tuondokane na dhana ya kuwa group limeanzishwa na wapinga Kristo. La pili ni kuwa, ndugu zangu maadmins ni watu wenye kazi zao hivyo si rahisi muda wote wawe hewani. Padre Revocatus yuko parokiani, mimi ni mwalimu wa chuo kikuu, ndugu Prudens ni mwajiriwa wa serikali, dada Pollyne ni mwajiriwa wa benki, dada Antusa ni mwajiriwa, na wengine kama Ruta na wengine. Sasa kuna wakati posts zipo pending si sababu watu hawataki kuziruhusu, sababu hakuna aliye na nafasi wakati huo. Zamani meseji zilienda hewani moja kwa moja, waliokuwepo waliona baadhi walivyokuwa wakipost pornography. Sasa tumetengeza kuwa mmoja anajibu maswali kwanza, lakini sasa majibu ya maswali hayamfanyi mmoja awe mkristu au mkatoliki. Kuna mmoja atajibu na bado si mkatoliki. Lakini hata wale wasio wakristo au wakatoliki wakiingia kama wanataka kujifunza, sisi hatuna shida nao. Tuna mapadre wengi tu humu ndani, mmojawapo padre Tito ambaye nimeona ameandika kwenye post ile na ametukumbusha kuwa sisi hatuko kubishana na watu ila ni vyema kujua imani yetu ili tukiulizwa kwa nini tunafanya tunayofanya tuweze kufundisha.
Kanisa mwanzo lilikuwa moja na wengine walimeguka toka tulipo na kuanzisha madhehebu. Ni kama Chuo Kikuu cha Dar zamani kilijumuisha Sokoine, Ardhi na Muhimbili. Sasa baadaye hivi vimekuwa vyuo vinavyojitegemea lakini katika kuwa vyuo vinaondoka na baadhi ya vitengo tu na kuacha vingine, mfano Muhimbili wana medicine tu, Ardhi wana land tu, Sokoine wana agriculture tu, ukitaka vyote pamoja waweza kuvipata tu katika kilicho chuo kikuu cha Dar. Ni mfano ulio na madhaifu lakini nadhani unaweza kufundisha kidogo. Hivyo Sokoine kuuliza kwa nini chuo kikuu cha Dar wana kitengo cha sheria, jibu ni kuwa wewe umeachaje kutokuwa na sheria. Yaani wao wa madhehebu wangekuwa na mantiki kuuliza tunachofanya sisi kama tungekianzisha baada ya wao kuondoka, au tungekuwa tumeanza pamoja, lakini wao wameanza baadaye, miaka mingi baada ya mitume. Yaani madhehebu yote yaliyopo leo hakuna ambalo lilianzishwa wakati mitume wakiwa hai. Kanisa pekee waliloacha mitume ndilo tulilonalo sisi, na ndiyo maana ya Kanisa KATOLIKI (universal) na la MITUME. Kuwa lilianza na mitume na ndilo pekee waliloacha. Wengine wakajimega toka hapa na kuanzisha madhehebu, hivyo madhehebu yale hayakuanza na mitume, ila imani waliyonayo imeanza na mitume. Kanisa pekee lililoanzishwa na mitume ndilo hili tulilonalo. Madhehebu mengine yote ya ukristo yameanzia kwa imani ya mitume lakini hayakuanzishwa na mitume. Hii ndiyo tofauti yetu kubwa. Ndiyo maana huwezi kusema letu ni dhehebu, sababu hili likiwa dhehebu tunakosa dini iitwayo ukristo. Tutajiuliza sasa dini iitwayo ukristo ni ipi? Maana mpaka Yesu anakufa hakukuwa na ukristo. Ukristo umeanza na mitume. Na mitume na waliacha kanisa moja na siyo madhehebu. Sasa yule aliyeachwa na mitume na aliyemwachia na wakaachiana mpaka tulipo alibaki hakutoka kwenda kuanzisha dhehebu, ndiyo maana tunasema ule kila walichoacha kipo tulipo sisi na si huko nje.
Maana yake ni kuwa ukitaka tafsiri ya uhakika ya maandiko kadiri walivyoelezwa mitume na Yesu huwezi kuipata nje, maana wenye hiyo tafsiri kama ilivyoelezwa na mitume na waandishi wa maandiko hawakutoka, walibaki na kufundisha walio ndani. Nje waliacha kutafuta tafsiri kadiri walivyoelewa wao na siyo kadiri ya maelezo ya mitume. Kuna tofauti kubwa kati ya kujisomea kitabu cha sayansi kilichoandikwa na Copleston, na kufundishwa sayansi na Copleston, aliyeandika kitabu cha sayansi. Bila shaka aliyefundishwa ataelewa zaidi kuliko asiye na mwalimu anayetegemea tu kujua kwake kusoma. Nimetoa mfano huu mara kadhaa, kuwa kujua kusoma haitakufanya ujue kuwa H2O ni alama ya maji, kama huna mwalimu wa kukuelekeza. Kujua kusoma kutakufanya useme Hechi Two Ooh badala ya water. Na shida hii tunaipata kwa mfano kwa waitwao YEHOVA WITNESS. Wanasema jina la Mungu ni Yehova, lakini ukweli ni kuwa walishindwa kujua kuwa Wayahudi waliandika jina la Mungu kama YHWH bila silabi kwa sababu ilikuwa marufuku kutamka jina la Mungu, hivyo kwa kuandika hivyo iliwasaidia hata waliosoma wasiweze kutamka. lakini neno halisi ya YHWH ni YAHWEH. Wao sababu hawana elimu hiyo wakasoma kama Yehova na kwa vile W ya Wayahudi ilikaa kama V ndo ikawa kabisa wamehalalisha. Ndugu zangu, Yesu alikaa na wanafunzi miaka mitatu akiwafundisha. Paulo alikaa na mitume kwa muda mrefu tu kabla hajaanza kuhubiri. Hii inatuambia nini? Inatufundisha nini? Inatufundisha kuwa Roho Mtakatifu hufanya kazi baada ya watu kujifunza na siyo kabla. Yesu hakushindwa kuwapa mitume Roho Mtakatifu na wawe na elimu yote, lakini aliwapa Roho Mtakatifu baada ya kuwafundisha kwa miaka mitatu. Nasi basi tujifunze kwanza, ndipo tumuite Roho Mtakatifu. Kinyume cha hapo huyo si Roho Mtakatifu. Ili mwalimu akufundishe formula ile ya H2O yabidi uwe kwanza na basics za syllaby, consonants, na numbers. Ndivyo Roho Mtakatifu anavyofanya kazi. Ama sivyo tuache hata kujifunza kusoma na kuandika tukae nyumbani tumuombe Roho Mtakatifu atupulizie kujua kusoma na kuandika. Roho Mtakatifu hafanyi kazi kwa namna hiyo. Na zaidi tukumbuke kuwa Roho Mtakatifu hufanya kazi kupitia wengine pia. Roho Mtakatifu anaweza mtumia jirani yako pia kukufundisha wewe anachotaka ukijue. Miujiza ya kazi za Roho Mtakatifu hutokea kila siku katika maisha yetu, hata katika mambo yale tuyaonayo kuwa ni ya kawaida sana kwetu. Yatubidi tu kufungua macho yetu ya imani kuyaona.