Leo tupate somo kwa wale wasiojua historia ya kanisa huku wakijidanganya wanajua

KUHUSU BABA MTAKATIFU PAPA FRANCIS

Kuna taarifa inasambazwa kwa kasi mitandaoni ikieleza kwamba baba mtakatifu Papa Francis amefuta rasmi Biblia na amependekeza kipatikane kitabu mbadala. Taarifa hiyo inaenda mbali na kueleza kuwa Papa kasema, "Biblia haifai tena kwa kuwa ni ya kizamani" na kwamba tayari mkutano mkuu wa kanisa umeitishwa kutekeleza agizo la Papa.

Napenda ujue...

1). Taarifa hii ilichapishwa kwa mara ya kwanza April, 2, 2018 na mtandao wa ThereIsNews.com (TIN). Huu ni mtandao maalumu wa habari za kutunga na vichekesho (fictional and humor) ambazo hazina uhalisia. Katika mtandao wao, kwenye eneo la tamko (disclaimer) wanaeleza wazi kuwa habari zote katika mtandao wao ni za kutunga ili kuchekesha (entertainment) na kwamba majina na maeneo vinavyotajwa katika habari yeyote havina uhalisia wowote na habari ama kichekesho wanachokua wametoa.

2). Katika kalenda na ratiba za Papa, hakuna tamko lolote kubwa kuhusu mabadiliko ya taratibu za kanisa hili lililotolewa muda huo uliotajwa na mtandao wa TIN.

Nini cha kuzingatia?

a). Habari hizi ni za uwaongo na kugushi zikilenga kuwatia hofu Wakatoliki na wasio Wakatoliki. Tukumbuke kuwa Shetani huwinda atuingizie hofu ili atushambulie kirahisi imani zetu. Ni vema tujifunze kuwa watafiti na wadadisi kila tunapopata taarifa za hofu. Mtindo wa kuzoa na kuamini kila taarifa unaweza kutumaliza.

b). Kanisa Katoliki ndio taasisi inayoongoza kutunza vyanzo vya kumbumumbu (bible historical sites) zilizopo ndani ya Biblia. Miaka nenda rudi wamekua wakitoa fedha, utaalamu na diplomasi, kuhakikisha miji ya Kibiblia na vitu vya Kibiblia vinalindwa. Kwa maana hiyo si hekima kuamini taarifa zinazoonesha kanisa katoliki halithamini Biblia hata kufika hatua ya kuifuta.

Ndani ya kanisa Katoliki kunaweza kuwepo madhaifu mengine ya kitaasisi (of which ni kawaida kwa kila taasisi), hata hivyo mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni.
 
nimeona majibu uliyowajibu baadhi ya members waliochangia mpaka nimepigwà na butwaa. we padri gani unakuwa na maneno ya shombo ka mwimba taarabu??

#DG

Mleta mada sio mwandishi....yeye amecopy kutoka kwenye group lao hukooooooo.
Huyu Ni mjumbe tuu hata padre aloandika hii hajui kama ishafika huku
 
Wapendwa waumini wakatoliki wenzetu Tumsifu Yesu Kristo. Asanteni sana kwa michango yenu kuhusu group letu na changamaoto mnazoziona. Leo kulikuwa na post ya mmoja ambaye ameeleza changamoto anazoziona kwa maadmins, kama kuchelewa kuachia posts za watu wanazotuma, kuachia posts ambazo zinaitwa za kichochezi, za madhehebu yanayokashifu ukatoliki, nk. Mmoja kasema labda group halikuanzishwa na wakatoliki bali wapinga Kristo. Ndugu zangu, mimi ni mmoja kati ya maadmins wa group na kati ya waanzilishi wa mwanzo wa group tukiongozwa padre Revocatus Paul. Mimi mwenyewe pia ni padre. Hivyo tuondokane na dhana ya kuwa group limeanzishwa na wapinga Kristo. La pili ni kuwa, ndugu zangu maadmins ni watu wenye kazi zao hivyo si rahisi muda wote wawe hewani. Padre Revocatus yuko parokiani, mimi ni mwalimu wa chuo kikuu, ndugu Prudens ni mwajiriwa wa serikali, dada Pollyne ni mwajiriwa wa benki, dada Antusa ni mwajiriwa, na wengine kama Ruta na wengine. Sasa kuna wakati posts zipo pending si sababu watu hawataki kuziruhusu, sababu hakuna aliye na nafasi wakati huo. Zamani meseji zilienda hewani moja kwa moja, waliokuwepo waliona baadhi walivyokuwa wakipost pornography. Sasa tumetengeza kuwa mmoja anajibu maswali kwanza, lakini sasa majibu ya maswali hayamfanyi mmoja awe mkristu au mkatoliki. Kuna mmoja atajibu na bado si mkatoliki. Lakini hata wale wasio wakristo au wakatoliki wakiingia kama wanataka kujifunza, sisi hatuna shida nao. Tuna mapadre wengi tu humu ndani, mmojawapo padre Tito ambaye nimeona ameandika kwenye post ile na ametukumbusha kuwa sisi hatuko kubishana na watu ila ni vyema kujua imani yetu ili tukiulizwa kwa nini tunafanya tunayofanya tuweze kufundisha.

Kanisa mwanzo lilikuwa moja na wengine walimeguka toka tulipo na kuanzisha madhehebu. Ni kama Chuo Kikuu cha Dar zamani kilijumuisha Sokoine, Ardhi na Muhimbili. Sasa baadaye hivi vimekuwa vyuo vinavyojitegemea lakini katika kuwa vyuo vinaondoka na baadhi ya vitengo tu na kuacha vingine, mfano Muhimbili wana medicine tu, Ardhi wana land tu, Sokoine wana agriculture tu, ukitaka vyote pamoja waweza kuvipata tu katika kilicho chuo kikuu cha Dar. Ni mfano ulio na madhaifu lakini nadhani unaweza kufundisha kidogo. Hivyo Sokoine kuuliza kwa nini chuo kikuu cha Dar wana kitengo cha sheria, jibu ni kuwa wewe umeachaje kutokuwa na sheria. Yaani wao wa madhehebu wangekuwa na mantiki kuuliza tunachofanya sisi kama tungekianzisha baada ya wao kuondoka, au tungekuwa tumeanza pamoja, lakini wao wameanza baadaye, miaka mingi baada ya mitume. Yaani madhehebu yote yaliyopo leo hakuna ambalo lilianzishwa wakati mitume wakiwa hai. Kanisa pekee waliloacha mitume ndilo tulilonalo sisi, na ndiyo maana ya Kanisa KATOLIKI (universal) na la MITUME. Kuwa lilianza na mitume na ndilo pekee waliloacha. Wengine wakajimega toka hapa na kuanzisha madhehebu, hivyo madhehebu yale hayakuanza na mitume, ila imani waliyonayo imeanza na mitume. Kanisa pekee lililoanzishwa na mitume ndilo hili tulilonalo. Madhehebu mengine yote ya ukristo yameanzia kwa imani ya mitume lakini hayakuanzishwa na mitume. Hii ndiyo tofauti yetu kubwa. Ndiyo maana huwezi kusema letu ni dhehebu, sababu hili likiwa dhehebu tunakosa dini iitwayo ukristo. Tutajiuliza sasa dini iitwayo ukristo ni ipi? Maana mpaka Yesu anakufa hakukuwa na ukristo. Ukristo umeanza na mitume. Na mitume na waliacha kanisa moja na siyo madhehebu. Sasa yule aliyeachwa na mitume na aliyemwachia na wakaachiana mpaka tulipo alibaki hakutoka kwenda kuanzisha dhehebu, ndiyo maana tunasema ule kila walichoacha kipo tulipo sisi na si huko nje.

Maana yake ni kuwa ukitaka tafsiri ya uhakika ya maandiko kadiri walivyoelezwa mitume na Yesu huwezi kuipata nje, maana wenye hiyo tafsiri kama ilivyoelezwa na mitume na waandishi wa maandiko hawakutoka, walibaki na kufundisha walio ndani. Nje waliacha kutafuta tafsiri kadiri walivyoelewa wao na siyo kadiri ya maelezo ya mitume. Kuna tofauti kubwa kati ya kujisomea kitabu cha sayansi kilichoandikwa na Copleston, na kufundishwa sayansi na Copleston, aliyeandika kitabu cha sayansi. Bila shaka aliyefundishwa ataelewa zaidi kuliko asiye na mwalimu anayetegemea tu kujua kwake kusoma. Nimetoa mfano huu mara kadhaa, kuwa kujua kusoma haitakufanya ujue kuwa H2O ni alama ya maji, kama huna mwalimu wa kukuelekeza. Kujua kusoma kutakufanya useme Hechi Two Ooh badala ya water. Na shida hii tunaipata kwa mfano kwa waitwao YEHOVA WITNESS. Wanasema jina la Mungu ni Yehova, lakini ukweli ni kuwa walishindwa kujua kuwa Wayahudi waliandika jina la Mungu kama YHWH bila silabi kwa sababu ilikuwa marufuku kutamka jina la Mungu, hivyo kwa kuandika hivyo iliwasaidia hata waliosoma wasiweze kutamka. lakini neno halisi ya YHWH ni YAHWEH. Wao sababu hawana elimu hiyo wakasoma kama Yehova na kwa vile W ya Wayahudi ilikaa kama V ndo ikawa kabisa wamehalalisha. Ndugu zangu, Yesu alikaa na wanafunzi miaka mitatu akiwafundisha. Paulo alikaa na mitume kwa muda mrefu tu kabla hajaanza kuhubiri. Hii inatuambia nini? Inatufundisha nini? Inatufundisha kuwa Roho Mtakatifu hufanya kazi baada ya watu kujifunza na siyo kabla. Yesu hakushindwa kuwapa mitume Roho Mtakatifu na wawe na elimu yote, lakini aliwapa Roho Mtakatifu baada ya kuwafundisha kwa miaka mitatu. Nasi basi tujifunze kwanza, ndipo tumuite Roho Mtakatifu. Kinyume cha hapo huyo si Roho Mtakatifu. Ili mwalimu akufundishe formula ile ya H2O yabidi uwe kwanza na basics za syllaby, consonants, na numbers. Ndivyo Roho Mtakatifu anavyofanya kazi. Ama sivyo tuache hata kujifunza kusoma na kuandika tukae nyumbani tumuombe Roho Mtakatifu atupulizie kujua kusoma na kuandika. Roho Mtakatifu hafanyi kazi kwa namna hiyo. Na zaidi tukumbuke kuwa Roho Mtakatifu hufanya kazi kupitia wengine pia. Roho Mtakatifu anaweza mtumia jirani yako pia kukufundisha wewe anachotaka ukijue. Miujiza ya kazi za Roho Mtakatifu hutokea kila siku katika maisha yetu, hata katika mambo yale tuyaonayo kuwa ni ya kawaida sana kwetu. Yatubidi tu kufungua macho yetu ya imani kuyaona.
Mimi naomba mniadd hilo group kama
au nitumie link Pm kama mkatoliki pure ni join
 
Nikumbushe tu kuwa wakati wa kusulubiwa kwa Yesu Kristo ni Warumi ndio walikuwa wanatawala hata Israel ilikuwa chini yake ( Hiyo ndio ilikuwa roman empire) walikuwa ni watawala tu wa kisiasa, hawakuwa na dini, walikuwa wapagani. Rumi ya kipagani. Baada ya sarakasi za hapa na pale wakaingilia ukirsto, mila zao na miungu yao ikaingizwa kwenye ibada ya kikristo kinguvu ,aliyepinga ,akuawa. Inakadiriwa watu Zaidi ya milioni 100 waliuawa katika mchakato wa kuondoa upinzani. Historia kama hii wengi hawaijui. Kwa hiyo wakiambia hili ni kanisa lililoanzishwa na Mtume petro wanaamini.
 
Tupe source ya hii taarifa yako.
 
Nini kuzimia hata kufa kabisaa.

Lete source baba maneno mengi ya nini?
Naendelea kufundisha kwa wasijua historia
Maana na asili ya jina Papa
Wikipedia inasema, “Papa ( neno la mkopo kutoka Kilatini lakini lenye asili ya Kigiriki, πάππας, pappas, [1] jina ambalo mtoto anamuitia baba yake) [2] ni cheo cha kiongozi mkuu wa Kanisa Katoliki duniani kote.” -(Wikipedia kamsi elezo huru, “Papa“).

“Papa” ni jina la kilatini linalomaanisha “baba” ambalo watoto hulitumia kuwaita baba zao. Hivyo Wakatoliki wanapoita “papa” wanamaanisha kwamba wao ni watoto na baba yao ni papa. Jina hili linapotamkwa kwa kiswahili sahihi Wakatoliki hutumia neno “Baba” pamoja na kivumishi “Mtakatifu” yaan, “Baba Mtakatifu”! Ni makufuru makubwa kumwita mwanadamu “Baba Mtakatifu”, kwani hakuna hata mwanadamu mmoja katika Biblia ambaye amewahi kuitwa jina hili, Inashangaza kwamba hata Yesu Mwenyewe hajawahi kuitwa “Baba Mtakatifu”, lakini Yesu katika Yohana 17 alipokuwa anasali, alilitumia jina la “Baba Mtakatifu” kumwita Mungu Baba wa mbinguni.

Papa kwa kuunda mfumo wa Upapa; yaani Ubaba, na kuitwa “Baba Mtakatifu” yeye ndiye “mtu wa kuasi”, “mwana wa uharibifu”, “mpingamizi” au “mpingaKristo”, “ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu.” II Wathesaloke 2:4. Huyu kazi zake ni “mfano wa kutenda kwake Shetani, kwa uwezo wote, na ishara na ajabu za uongo; 10 na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa. 11 Kwa hiyo Mungu awaletea nguvu ya upotevu, wauamini uongo; 12 ili wahukumiwe wote ambao hawakuiamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu.” II Wathesalonike 2:9:12.

Mfumo huu wa Upapa kwa madogima yake na mapokeo yake, umewaongoza mamilioni ya Wakristo kuamini uongo; “ibaada ya jumapili” ilianzishwa na Upapa, “fundisho la utatu mtakatifu” lilianzishwa na Upapa, tena ndilo lilikuwa msaada mkubwa uliosababisha Upapa kuwaua wapinga utatu, na kupata mamlaka kamili ya kanisa na serikali. Kuamini uongo huo ni “kujifrahisha katika udhalimu”, tena ni “ibaada ya bure” (Marko 7:1-10). Na kwa sababu hiyo Bwana Yesu atauangamiza mfumo wa Upapa “kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake; II Wathesalonike 2:8

Wakatoliki hudai kwamba Papa alirithi kiti cha Petro, hakuna hata kumbukumbu moja katika Biblia ambapo Petro ameitwa “Papa” au “Baba Mtakatifu”, jina “papa” lenyewe halipo kwenye Biblia, ila ni jina lililoingizwa na mwanadamu baada ya mitume wote kufariki. Yesu aliwaambia mitume kwamba, “Wala msimwite mtu baba duniani; maana Baba yenu ni mmoja, aliye wa mbinguni.” Mathayo 23:9. Hapa Yesu alimaanisha kuwa katika kanisa asiwepo mtu mwenye cheo cha kuitwa “baba”; Yesu alijua kabisa kuwa mpingaKristo angekuja kwa kujiita “baba”, na akatuonya mapema. Kumwita mwanadamu “Papa” au “Baba Mtakatifu” si tu kwamba ni kudharau amri ya Yesu inayokataza kumwita mwanadamu baba, bali ni kumwabudu mwanadamu pia. Kama mtu akiwa na cheo cha “baba” kanisani, je Mungu Mwenyewe atakuwa na cheo gani? Hii ni wazi kwamba papa ndiye mungu na baba wa kanisa Katoliki!

Jina jingine linalotumika kwa Papa ni “Pontifex Maximus” jina hili ni la kilatini na linamaanisha “askofu mkuu” (greatest pontiff), au “mjenzi mkuu wa daraja” (greatest bridge-builder). Kabla ya papa kulitumia jina hili, zamani lilitumiwa na mkuu wa makuhani katika dini ya Rumi ya kipagani. Papa analitumia jina hili kuashiria kwamba yeye ndiye mkuu wa makuhani wote wa Katoliki, lakini kiukweli jina hili la kipagani linaonyesha wazi kuwa papa alirithi kiti cha upagani wa Rumi na wala sio Petro.

Petro hakuwa mkuu juu ya watu wengine, Yesu aliwaambia mitume kwamba, “Mwajua ya kuwa wakuu wa Mataifa huwatawala kwa nguvu, na wakubwa wao huwatumikisha. Lakini haitakuwa hivyo kwenu; bali mtu ye yote anayetaka kuwa mkubwa kwenu, na awe mtumishi wenu;” Mathayo 20:25-26. Miaka hamsini baada ya kupaa kwa Yesu, katika mwaka 49 B.K., kulitokea malumbano miongoni mwa Wakristo kuhusu kutahiriwa na kutokutahiriwa, ikabidi mitume, wazee wa kanisa, na ndugu wengine wakusanyike Yerusalemu ili kulitatua tatizo hilo (Matendo 15). Kama Petro angekuwa ni mkuu, kichwa cha kanisa, mchungaji mkuu, au papa, hapa yeye angekuwa sauti ya mwisho, na watu wote wangemtegemea yeye na kutii uamuzi wake. Lakini siyo hivyo; kwani baada ya Petro, Paulo, Barnaba n.k, kutoa maoni yao kuhusu Mungu alivyofanya kazi kwa watu wa mataifa. Aliyekuja kutoa uamzi wa mwisho alikuwa ni Yakobo na wala sio Petro, Yakobo akasema, “mimi naamua hivi; Tusiwatabishe wale waliomgeukia Mungu katika Mataifa;” (Matendo 15:19), kisha watu wote wakapendezwa na uamuzi wa Yakobo wakakubaliana naye (Matendo 15:22).

Katika Wagalatia 2 tunaona Paulo alishindana na Petro huko Antiokia, kwa sababu Petro alikuwa akila na watu wa mataifa, lakini Wayahudi walipokuja akajitenga yeye pamoja na Barnaba na wayahudi wengine kadhaa, huku akiwaogopa waliotahiriwa. Paulo akawakemea na kusema kwamba walikuwa wamefanya jambo la unafiki. Paulo alijua kabisa kwamba kichwa cha kanisa ni Yesu pekee, Petro ni ndugu kama watu wengine. Angalia pia Je Petro alikuwa papa wa kwanza?
 
Tatizo la wasabato mnadhani biblia inasomwa kama gazeti la Shigongo?

Inakuwaje sasa Biblia hiyohiyo inasema Mungu anapendezwa na watakatifu waliopo duniani?

Huna hoja mpuuzi kabisa wewe, hata Fellah anaitwa mkubwa na wanawe na hajawazaa.

Sina muda wa kubishana na machizi mimi.
 
Nilifikiri tunafundishana kila mtu na anachokijua kumbe na matusi yamo. Sasa neno la Mungu na matusi kweli. Unaonekana umekasirika ngoja nikuache rafiki
 
Hapa na mimi huwa naachwa njia panda kwamba kusoma Bible ni lazima uwe umesomea au una roho mtakatifu? Au IQ ya mtu?

Padre naomba nielekezwe unitoe ujinga nilionao, Bible inasomwaje?
Biblia iliandikwa na watu waiovuviwa roho mtakatifu. Hivyo kuielewa inahitaji uwezo wako + uwezo wa roho mtakatifu. Hivyo omba kwa Mungu kabla ya kuanza kusoma. Na kama maarifa yoyote yalivyo upate mtu mjuzi akupe msaada.Ndivyo ninavyojua
 
Matola katika Ukristo nilipokuwa nasoma historia ya kanisa kwanza tulikuwa na 2 Historia Ya Kanisa I&II
kwa kila kitabu si chini ya page 1500 na bado marejo yalikuwepo mengine mengi tu
zaidi ya yote nilisoma na maandiko ya waandishi mbalimbali kama sehemu ya kupata hoja na ufahamu wa ziada ili nielewe vizuri.
Sasa sijajua wewe hapo ni historia ya kanisa lenu au kanisa lini mkuu?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom