Leo tupate somo kwa wale wasiojua historia ya kanisa huku wakijidanganya wanajua

Matola

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
40,099
2,000
Wapendwa waumini wakatoliki wenzetu Tumsifu Yesu Kristo. Asanteni sana kwa michango yenu kuhusu group letu na changamaoto mnazoziona. Leo kulikuwa na post ya mmoja ambaye ameeleza changamoto anazoziona kwa maadmins, kama kuchelewa kuachia posts za watu wanazotuma, kuachia posts ambazo zinaitwa za kichochezi, za madhehebu yanayokashifu ukatoliki, nk. Mmoja kasema labda group halikuanzishwa na wakatoliki bali wapinga Kristo. Ndugu zangu, mimi ni mmoja kati ya maadmins wa group na kati ya waanzilishi wa mwanzo wa group tukiongozwa padre Revocatus Paul. Mimi mwenyewe pia ni padre. Hivyo tuondokane na dhana ya kuwa group limeanzishwa na wapinga Kristo. La pili ni kuwa, ndugu zangu maadmins ni watu wenye kazi zao hivyo si rahisi muda wote wawe hewani. Padre Revocatus yuko parokiani, mimi ni mwalimu wa chuo kikuu, ndugu Prudens ni mwajiriwa wa serikali, dada Pollyne ni mwajiriwa wa benki, dada Antusa ni mwajiriwa, na wengine kama Ruta na wengine. Sasa kuna wakati posts zipo pending si sababu watu hawataki kuziruhusu, sababu hakuna aliye na nafasi wakati huo. Zamani meseji zilienda hewani moja kwa moja, waliokuwepo waliona baadhi walivyokuwa wakipost pornography. Sasa tumetengeza kuwa mmoja anajibu maswali kwanza, lakini sasa majibu ya maswali hayamfanyi mmoja awe mkristu au mkatoliki. Kuna mmoja atajibu na bado si mkatoliki. Lakini hata wale wasio wakristo au wakatoliki wakiingia kama wanataka kujifunza, sisi hatuna shida nao. Tuna mapadre wengi tu humu ndani, mmojawapo padre Tito ambaye nimeona ameandika kwenye post ile na ametukumbusha kuwa sisi hatuko kubishana na watu ila ni vyema kujua imani yetu ili tukiulizwa kwa nini tunafanya tunayofanya tuweze kufundisha.

Kanisa mwanzo lilikuwa moja na wengine walimeguka toka tulipo na kuanzisha madhehebu. Ni kama Chuo Kikuu cha Dar zamani kilijumuisha Sokoine, Ardhi na Muhimbili. Sasa baadaye hivi vimekuwa vyuo vinavyojitegemea lakini katika kuwa vyuo vinaondoka na baadhi ya vitengo tu na kuacha vingine, mfano Muhimbili wana medicine tu, Ardhi wana land tu, Sokoine wana agriculture tu, ukitaka vyote pamoja waweza kuvipata tu katika kilicho chuo kikuu cha Dar. Ni mfano ulio na madhaifu lakini nadhani unaweza kufundisha kidogo. Hivyo Sokoine kuuliza kwa nini chuo kikuu cha Dar wana kitengo cha sheria, jibu ni kuwa wewe umeachaje kutokuwa na sheria. Yaani wao wa madhehebu wangekuwa na mantiki kuuliza tunachofanya sisi kama tungekianzisha baada ya wao kuondoka, au tungekuwa tumeanza pamoja, lakini wao wameanza baadaye, miaka mingi baada ya mitume. Yaani madhehebu yote yaliyopo leo hakuna ambalo lilianzishwa wakati mitume wakiwa hai. Kanisa pekee waliloacha mitume ndilo tulilonalo sisi, na ndiyo maana ya Kanisa KATOLIKI (universal) na la MITUME. Kuwa lilianza na mitume na ndilo pekee waliloacha. Wengine wakajimega toka hapa na kuanzisha madhehebu, hivyo madhehebu yale hayakuanza na mitume, ila imani waliyonayo imeanza na mitume. Kanisa pekee lililoanzishwa na mitume ndilo hili tulilonalo. Madhehebu mengine yote ya ukristo yameanzia kwa imani ya mitume lakini hayakuanzishwa na mitume. Hii ndiyo tofauti yetu kubwa. Ndiyo maana huwezi kusema letu ni dhehebu, sababu hili likiwa dhehebu tunakosa dini iitwayo ukristo. Tutajiuliza sasa dini iitwayo ukristo ni ipi? Maana mpaka Yesu anakufa hakukuwa na ukristo. Ukristo umeanza na mitume. Na mitume na waliacha kanisa moja na siyo madhehebu. Sasa yule aliyeachwa na mitume na aliyemwachia na wakaachiana mpaka tulipo alibaki hakutoka kwenda kuanzisha dhehebu, ndiyo maana tunasema ule kila walichoacha kipo tulipo sisi na si huko nje.

Maana yake ni kuwa ukitaka tafsiri ya uhakika ya maandiko kadiri walivyoelezwa mitume na Yesu huwezi kuipata nje, maana wenye hiyo tafsiri kama ilivyoelezwa na mitume na waandishi wa maandiko hawakutoka, walibaki na kufundisha walio ndani. Nje waliacha kutafuta tafsiri kadiri walivyoelewa wao na siyo kadiri ya maelezo ya mitume. Kuna tofauti kubwa kati ya kujisomea kitabu cha sayansi kilichoandikwa na Copleston, na kufundishwa sayansi na Copleston, aliyeandika kitabu cha sayansi. Bila shaka aliyefundishwa ataelewa zaidi kuliko asiye na mwalimu anayetegemea tu kujua kwake kusoma. Nimetoa mfano huu mara kadhaa, kuwa kujua kusoma haitakufanya ujue kuwa H2O ni alama ya maji, kama huna mwalimu wa kukuelekeza. Kujua kusoma kutakufanya useme Hechi Two Ooh badala ya water. Na shida hii tunaipata kwa mfano kwa waitwao YEHOVA WITNESS. Wanasema jina la Mungu ni Yehova, lakini ukweli ni kuwa walishindwa kujua kuwa Wayahudi waliandika jina la Mungu kama YHWH bila silabi kwa sababu ilikuwa marufuku kutamka jina la Mungu, hivyo kwa kuandika hivyo iliwasaidia hata waliosoma wasiweze kutamka. lakini neno halisi ya YHWH ni YAHWEH. Wao sababu hawana elimu hiyo wakasoma kama Yehova na kwa vile W ya Wayahudi ilikaa kama V ndo ikawa kabisa wamehalalisha. Ndugu zangu, Yesu alikaa na wanafunzi miaka mitatu akiwafundisha. Paulo alikaa na mitume kwa muda mrefu tu kabla hajaanza kuhubiri. Hii inatuambia nini? Inatufundisha nini? Inatufundisha kuwa Roho Mtakatifu hufanya kazi baada ya watu kujifunza na siyo kabla. Yesu hakushindwa kuwapa mitume Roho Mtakatifu na wawe na elimu yote, lakini aliwapa Roho Mtakatifu baada ya kuwafundisha kwa miaka mitatu. Nasi basi tujifunze kwanza, ndipo tumuite Roho Mtakatifu. Kinyume cha hapo huyo si Roho Mtakatifu. Ili mwalimu akufundishe formula ile ya H2O yabidi uwe kwanza na basics za syllaby, consonants, na numbers. Ndivyo Roho Mtakatifu anavyofanya kazi. Ama sivyo tuache hata kujifunza kusoma na kuandika tukae nyumbani tumuombe Roho Mtakatifu atupulizie kujua kusoma na kuandika. Roho Mtakatifu hafanyi kazi kwa namna hiyo. Na zaidi tukumbuke kuwa Roho Mtakatifu hufanya kazi kupitia wengine pia. Roho Mtakatifu anaweza mtumia jirani yako pia kukufundisha wewe anachotaka ukijue. Miujiza ya kazi za Roho Mtakatifu hutokea kila siku katika maisha yetu, hata katika mambo yale tuyaonayo kuwa ni ya kawaida sana kwetu. Yatubidi tu kufungua macho yetu ya imani kuyaona.
 
Matola

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
40,099
2,000
Leo nimeona mmoja aliniandikia meseji ambayo ilikuwa filtered kwenye inbox yangu, miaka ya 2014. Huyu alisema kuwa RC tunadanganya watu na hawawi critical sababu hawasomi Biblia Jumapili kama kanisa la kwanza. Na kuwa ananiombea nibadilike maana.naye alikuwa mbishi kama mimi ila akabadilika baada ya kusoma Biblia. Hiki ndicho nilichomjibu:
Milele amina. Sikukumbuki na ndiyo kwanza naona meseji zako za malalamiko kuhusu RC. Ni rahisi sana kusoma Biblia lakini ni ngumu kuielewa. Biblia siyo gazeti la kila siku na wala haikuandikwa Tanzania. Hivyo kudhani sababu naweza kusoma basi najua Biblia ni kujidanganya. Tofauti na unavyodhani RC wanadanganywa, wewe unajidanganya. Kanisa la kwanza halikusoma Biblia, lilisoma masomo kama RC wafanyavyo maana walirithi desturi za wayahudi ambayo inaelezwa katika Injili siku ile Yesu alipokwenda sinagogi kusali na wakampa kitabu/gombo la chuo na akasoma sehemu ya kitabu cha Isaya sehemu iliyosema "Roho wa Mungu yu juu yangu..." Na alipomaliza alikaa lakini wote wakamkazia macho ahubiri kadiri ya desturi yao. Haya yote ndiyo ambayo RC wanaendelea hadi leo. Sasa tofauti na kuwa RC wanawadanganya watu, wanaodhani RC wanadanganya watu ndiyo wanaojidanganya. Hata Yesu alipochagua wanafunzi hawawaambia tu nawapa Roho mkahubiri, alikaa nao miaka mitatu akiwafundisha. Baada ya miaka mitatu ya kujifunza kwa Yesu ndiyo wakaanza kuhubiri baada ya kufufuka kwa Yesu. Sasa wewe unayedhani waweza amka tu asubuhi sababu wajua kusoma Biblia basi umekuwa mtaalamu wa maandiko, unajidanganya. Haijawahi kutokea na haitatokea, hata kati ya wayahudi wakati wa Yesu hakukuwa na walimu wa sheria waliokuwa walimu tu kwa kujua kusoma na kuandika bila kujifunza sheria toka kwa walimu waliokuwepo. Yesu alikuwa na wanafunzi ndiyo wale wafuasi, hakuwafundisha kusoma bali aliwafundisha Neno la mungu. Aliwafundisha kwanza na Roho Mtakatifu aliyekuja baadaye aliwaambia atawakumbusha yale aliyowafundisha. Wadhani Yesu alishindwa kuwapa tu Roho Mtakatifu na wawe na ufahamu wote? Kwanini alichagua kuwafundisha miaka mitatu ndipo akawapa Roho Mtakatifu? Sasa wewe unapojifanya unafahamu Biblia kwa kujua tu kusoma na kuandika tunashangaa. Tutakuuliza kuwa je umejifunza Biblia chini ya mwalimu nani? Wale mitume walijifunza chini ya Yesu kwa miaka mitatu. Wewe umejifunza chini ya nani mpaka leo uwe mwalimu? Hivyo si RC wanaodanganywa, ni wewe ndiye unayejidanganya.
 
Mmenyakunde

Member
Aug 18, 2018
97
125

@Matola
 
Northman

JF-Expert Member
Dec 22, 2016
1,146
2,000
Ni rahisi sana kusoma Biblia lakini ni ngumu kuielewa. Biblia siyo gazeti la kila siku na wala haikuandikwa Tanzania. Hivyo kudhani sababu naweza kusoma basi najua Biblia ni kujidanganya.
Biblia inasomwaje?
 
Matola

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
40,099
2,000
Ni kujidanganya kudhani kanisa katoliki limetokana na mitume. Mitume hawakuwahi kuacha kitu kinaitwa RC maana mafundisho yake tu ni kinyume na yale ya RC
Unapopinga kwamba Nairobi siyo mji mkuu wa Tanzania unapaswa kueleza Nairobi ni mji mkuu wa Kenya.

Kwahiyo unapopinga kanisa katoliki si la mitume tueleze wewe historia ya kanisa na biblia tunayosoma leo iliandaliwana na kina nani?

Otherwise shut up.
 
3 Angels message

JF-Expert Member
Aug 3, 2017
2,483
2,000
Unapopinga kwamba Nairobi siyo mji mkuu wa Tanzania unapaswa kueleza Nairobi ni mji mkuu wa Kenya.

Kwahiyo unapopinga kanisa katoliki si la mitume tueleze wewe historia ya kanisa na biblia tunayosoma leo iliandaliwana na kina nani?

Otherwise shut up.
Twende taratibu tu mtumishi huna haja ya kutumia nguvu sana kwenye mambo ya kiroho

Ngoja tuanze na hoja moja baada ya nyingine na tuanzie mbali kidogo. Miaka kadhaa ya nyuma kanisa katoliki lilikuwa likiuza hati za misamaha ya dhambi kwa wale waliokuwa wakitenda dhambi

Sasa hebu tuambie ni mtume gani aliwahi kuuza hati ya msamaha wa dhambi?
 
Joseph lebai

JF-Expert Member
Jul 19, 2017
3,750
2,000
Mliojiita mapadri , mlisoma falsafa japo sijui ni kiwango gani certificate , diploma au degree ! Baada ya falsafa na kuitafakari je ulichoandika kina ukweli kiasi gani ? Kaukweli kapo ila kiasi gani ? Huenda theology imekumeza zaidi ! Je Yesu aliponwambia Petro ni mwamba na juu ya mwamba atajenga kanisa ina maana ni ukatoliki ??
 
Kyalow

JF-Expert Member
Mar 6, 2011
3,100
2,000
Twende taratibu tu mtumishi huna haja ya kutumia nguvu sana kwenye mambo ya kiroho

Ngoja tuanze na hoja moja baada ya nyingine na tuanzie mbali kidogo. Miaka kadhaa ya nyuma kanisa katoliki lilikuwa likiuza hati za misamaha ya dhambi kwa wale waliokuwa wakitenda dhambi

Sasa hebu tuambie ni mtume gani aliwahi kuuza hati ya msamaha wa dhambi?
Hana jibu zaidi ya mipasho
 
Nadu

JF-Expert Member
Jul 19, 2018
261
250
Unapopinga kwamba Nairobi siyo mji mkuu wa Tanzania unapaswa kueleza Nairobi ni mji mkuu wa Kenya.

Kwahiyo unapopinga kanisa katoliki si la mitume tueleze wewe historia ya kanisa na biblia tunayosoma leo iliandaliwana na kina nani?

Otherwise shut up.
Kanisa la RC sio kanisa la Mitume. Katika historia halijawahi kuwako na kanisa linaloitwa la Mitume lilikuwa linaitwa Kanisa la mahali fulani (kutegemea eneo husika). Mfano kanisa la Yerusalem, Antiokia, Efeso au Rumi nk.

Kati ya karne ya 3 na 4 AD kulikuwa na Maaskofu katika mijii mitano yenye nguvu: Jerusalem, Alexandria, Constantinople, Rumi na Antioch. Kila Askofu alikuwa anaongoza eneo lake wakiwa co equals.

Kwa sababu ya kuingia mafundisho potofu wakati ule, na dola la Rumi kuanguka karne ya nne, kukatokea ombwe la uongozi. Askofu wa Rumi polepole akaanza kujijengea umaarufu na kukubalika. Kwanza kwa sababu Rumi ilikuwa na nguvu kiuchumi na ni mji Mkuu ktk iliyokuwa dola la Rumi.

Askofu huyo na wote waliofuata wakaanza kudai kuwa yeye ndiye kiongozi wa wenzake (universal bishop) wa wale wa Antioch, Jerusalem, Constantinople na Alexandria. Ili kujengea ushahidi jambo hilo kukaanzishwa dhana kuwa Petro ndiye aliyekuwa kiongozi wa kanisa la Rumi na ndiye aliachiwa madaraka na Yesu na ndiye anayewaachia maasokofu wa Rumi Uaskofu huo. Pamoja na fundisho hill lisilo la kibiblia kanisa hilo Likaingiza mafundisho mengine mengi ambayo yalikuwa mageni mfano, ibada za wafu, vyeti vya msamaha wa dhambi nk.

Jina la "Roman Catholic Church " lilianzia katika mktadha huo. Nikumbushe tu kuwa wakati huo wote wale Maaskofu wengine 4 hawakuwa na furaha na jinsi kanisa lilivyokuwa linaendeshwa. Mfano ni kanisa la Constantinople ambalo mpaka mwaka 1054 lilijitenga officially na kanisa la mgharibi yaani Rumi.

Kwa hiyo kanisa lenyewe la Roman Catholic ndio lililoacha imani ya Mitume ama kanisa la Mitume kama linavyojinasibu na likakataliwa na kanisa la mashariki (Constantinople). Wakati wote kanisa la Yesu ama liwe RC ama vinginevyo nilazima lijikite katika mafundisho ya kibiblia. Sote RC na wengine turudi katika ukristo wa Agano jipya.
 
Kyalow

JF-Expert Member
Mar 6, 2011
3,100
2,000
Twende taratibu tu mtumishi huna haja ya kutumia nguvu sana kwenye mambo ya kiroho

Ngoja tuanze na hoja moja baada ya nyingine na tuanzie mbali kidogo. Miaka kadhaa ya nyuma kanisa katoliki lilikuwa likiuza hati za misamaha ya dhambi kwa wale waliokuwa wakitenda dhambi

Sasa hebu tuambie ni mtume gani aliwahi kuuza hati ya msamaha wa dhambi?
Matola copy hii peleka kwenye group, najua majibu hauna
 
Kiwete

JF-Expert Member
Dec 18, 2010
706
1,000
Wapendwa waumini wakatoliki wenzetu Tumsifu Yesu Kristo. Asanteni sana kwa michango yenu kuhusu group letu na changamaoto mnazoziona. Leo kulikuwa na post ya mmoja ambaye ameeleza changamoto anazoziona kwa maadmins, kama kuchelewa kuachia posts za watu wanazotuma, kuachia posts ambazo zinaitwa za kichochezi, za madhehebu yanayokashifu ukatoliki, nk. Mmoja kasema labda group halikuanzishwa na wakatoliki bali wapinga Kristo. Ndugu zangu, mimi ni mmoja kati ya maadmins wa group na kati ya waanzilishi wa mwanzo wa group tukiongozwa padre Revocatus Paul. Mimi mwenyewe pia ni padre. Hivyo tuondokane na dhana ya kuwa group limeanzishwa na wapinga Kristo. La pili ni kuwa, ndugu zangu maadmins ni watu wenye kazi zao hivyo si rahisi muda wote wawe hewani. Padre Revocatus yuko parokiani, mimi ni mwalimu wa chuo kikuu, ndugu Prudens ni mwajiriwa wa serikali, dada Pollyne ni mwajiriwa wa benki, dada Antusa ni mwajiriwa, na wengine kama Ruta na wengine. Sasa kuna wakati posts zipo pending si sababu watu hawataki kuziruhusu, sababu hakuna aliye na nafasi wakati huo. Zamani meseji zilienda hewani moja kwa moja, waliokuwepo waliona baadhi walivyokuwa wakipost pornography. Sasa tumetengeza kuwa mmoja anajibu maswali kwanza, lakini sasa majibu ya maswali hayamfanyi mmoja awe mkristu au mkatoliki. Kuna mmoja atajibu na bado si mkatoliki. Lakini hata wale wasio wakristo au wakatoliki wakiingia kama wanataka kujifunza, sisi hatuna shida nao. Tuna mapadre wengi tu humu ndani, mmojawapo padre Tito ambaye nimeona ameandika kwenye post ile na ametukumbusha kuwa sisi hatuko kubishana na watu ila ni vyema kujua imani yetu ili tukiulizwa kwa nini tunafanya tunayofanya tuweze kufundisha.

Kanisa mwanzo lilikuwa moja na wengine walimeguka toka tulipo na kuanzisha madhehebu. Ni kama Chuo Kikuu cha Dar zamani kilijumuisha Sokoine, Ardhi na Muhimbili. Sasa baadaye hivi vimekuwa vyuo vinavyojitegemea lakini katika kuwa vyuo vinaondoka na baadhi ya vitengo tu na kuacha vingine, mfano Muhimbili wana medicine tu, Ardhi wana land tu, Sokoine wana agriculture tu, ukitaka vyote pamoja waweza kuvipata tu katika kilicho chuo kikuu cha Dar. Ni mfano ulio na madhaifu lakini nadhani unaweza kufundisha kidogo. Hivyo Sokoine kuuliza kwa nini chuo kikuu cha Dar wana kitengo cha sheria, jibu ni kuwa wewe umeachaje kutokuwa na sheria. Yaani wao wa madhehebu wangekuwa na mantiki kuuliza tunachofanya sisi kama tungekianzisha baada ya wao kuondoka, au tungekuwa tumeanza pamoja, lakini wao wameanza baadaye, miaka mingi baada ya mitume. Yaani madhehebu yote yaliyopo leo hakuna ambalo lilianzishwa wakati mitume wakiwa hai. Kanisa pekee waliloacha mitume ndilo tulilonalo sisi, na ndiyo maana ya Kanisa KATOLIKI (universal) na la MITUME. Kuwa lilianza na mitume na ndilo pekee waliloacha. Wengine wakajimega toka hapa na kuanzisha madhehebu, hivyo madhehebu yale hayakuanza na mitume, ila imani waliyonayo imeanza na mitume. Kanisa pekee lililoanzishwa na mitume ndilo hili tulilonalo. Madhehebu mengine yote ya ukristo yameanzia kwa imani ya mitume lakini hayakuanzishwa na mitume. Hii ndiyo tofauti yetu kubwa. Ndiyo maana huwezi kusema letu ni dhehebu, sababu hili likiwa dhehebu tunakosa dini iitwayo ukristo. Tutajiuliza sasa dini iitwayo ukristo ni ipi? Maana mpaka Yesu anakufa hakukuwa na ukristo. Ukristo umeanza na mitume. Na mitume na waliacha kanisa moja na siyo madhehebu. Sasa yule aliyeachwa na mitume na aliyemwachia na wakaachiana mpaka tulipo alibaki hakutoka kwenda kuanzisha dhehebu, ndiyo maana tunasema ule kila walichoacha kipo tulipo sisi na si huko nje.

Maana yake ni kuwa ukitaka tafsiri ya uhakika ya maandiko kadiri walivyoelezwa mitume na Yesu huwezi kuipata nje, maana wenye hiyo tafsiri kama ilivyoelezwa na mitume na waandishi wa maandiko hawakutoka, walibaki na kufundisha walio ndani. Nje waliacha kutafuta tafsiri kadiri walivyoelewa wao na siyo kadiri ya maelezo ya mitume. Kuna tofauti kubwa kati ya kujisomea kitabu cha sayansi kilichoandikwa na Copleston, na kufundishwa sayansi na Copleston, aliyeandika kitabu cha sayansi. Bila shaka aliyefundishwa ataelewa zaidi kuliko asiye na mwalimu anayetegemea tu kujua kwake kusoma. Nimetoa mfano huu mara kadhaa, kuwa kujua kusoma haitakufanya ujue kuwa H2O ni alama ya maji, kama huna mwalimu wa kukuelekeza. Kujua kusoma kutakufanya useme Hechi Two Ooh badala ya water. Na shida hii tunaipata kwa mfano kwa waitwao YEHOVA WITNESS. Wanasema jina la Mungu ni Yehova, lakini ukweli ni kuwa walishindwa kujua kuwa Wayahudi waliandika jina la Mungu kama YHWH bila silabi kwa sababu ilikuwa marufuku kutamka jina la Mungu, hivyo kwa kuandika hivyo iliwasaidia hata waliosoma wasiweze kutamka. lakini neno halisi ya YHWH ni YAHWEH. Wao sababu hawana elimu hiyo wakasoma kama Yehova na kwa vile W ya Wayahudi ilikaa kama V ndo ikawa kabisa wamehalalisha. Ndugu zangu, Yesu alikaa na wanafunzi miaka mitatu akiwafundisha. Paulo alikaa na mitume kwa muda mrefu tu kabla hajaanza kuhubiri. Hii inatuambia nini? Inatufundisha nini? Inatufundisha kuwa Roho Mtakatifu hufanya kazi baada ya watu kujifunza na siyo kabla. Yesu hakushindwa kuwapa mitume Roho Mtakatifu na wawe na elimu yote, lakini aliwapa Roho Mtakatifu baada ya kuwafundisha kwa miaka mitatu. Nasi basi tujifunze kwanza, ndipo tumuite Roho Mtakatifu. Kinyume cha hapo huyo si Roho Mtakatifu. Ili mwalimu akufundishe formula ile ya H2O yabidi uwe kwanza na basics za syllaby, consonants, na numbers. Ndivyo Roho Mtakatifu anavyofanya kazi. Ama sivyo tuache hata kujifunza kusoma na kuandika tukae nyumbani tumuombe Roho Mtakatifu atupulizie kujua kusoma na kuandika. Roho Mtakatifu hafanyi kazi kwa namna hiyo. Na zaidi tukumbuke kuwa Roho Mtakatifu hufanya kazi kupitia wengine pia. Roho Mtakatifu anaweza mtumia jirani yako pia kukufundisha wewe anachotaka ukijue. Miujiza ya kazi za Roho Mtakatifu hutokea kila siku katika maisha yetu, hata katika mambo yale tuyaonayo kuwa ni ya kawaida sana kwetu. Yatubidi tu kufungua macho yetu ya imani kuyaona.
Even a cursory reading of the New Testament will reveal that the Catholic Church does not have its origin in the teachings of Jesus or His apostles. In the New Testament, there is no mention of the papacy, worship/adoration of Mary (or the immaculate conception of Mary, the perpetual virginity of Mary, the assumption of Mary, or Mary as co-redemptrix and mediatrix), petitioning saints in heaven for their prayers, apostolic succession, the ordinances of the church functioning as sacraments, infant baptism, confession of sin to a priest, purgatory, indulgences, or the equal authority of church tradition and Scripture. So, if the origin of the Catholic Church is not in the teachings of Jesus and His apostles, as recorded in the New Testament, what is the true origin of the Catholic Church?

For the first 280 years of Christian history, Christianity was banned by the Roman Empire, and Christians were terribly persecuted. This changed after the “conversion” of the Roman Emperor Constantine. Constantine provided religious toleration with the Edict of Milan in AD 313, effectively lifting the ban on Christianity. Later, in AD 325, Constantine called the Council of Niceain an attempt to unify Christianity. Constantine envisioned Christianity as a religion that could unite the Roman Empire, which at that time was beginning to fragment and divide. While this may have seemed to be a positive development for the Christian church, the results were anything but positive. Just as Constantine refused to fully embrace the Christian faith but continued many of his pagan beliefs and practices, so the Christian church that Constantine and his successors promoted progressively became a mixture of true Christianity and Roman paganism.

Following are a few examples:

Most Roman Catholic beliefs and practices regarding Mary are completely absent from the Bible. Where did those beliefs come from? The Roman Catholic view of Mary has far more in common with the Isis mother-goddess religion of Egypt than it does with anything taught in the New Testament. Interestingly, the first hints of Catholic Mariology occur in the writings of Origen, who lived in Alexandria, Egypt, which happened to be the focal point of Isis worship.

The Lord’s Supper being a consumption of the literal body and blood of Jesus is not taught in the Bible. The idea that bread and wine are miraculously transformed into the literal body and blood of Jesus (transubstantiation) is not biblical. However, several ancient pagan religions, including Mithraism, which was very popular in the Roman Empire, had some form of “theophagy” (the eating of one’s god) as a ritualistic practice.

Roman Catholicism has “saints” one can pray to in order to gain a particular blessing. For example, Saint Gianna Beretta Molla is the patron saint of fertility. Francis of Assisi is the patron saint of animals. There are multiple patron saints of healing and comfort. Nowhere is even a hint of this taught in Scripture. Just as the Roman pantheon of gods had a god of love, a god of peace, a god of war, a god of strength, a god of wisdom, etc., so the Catholic Church has a saint who is “in charge” over each of these and many other categories. Many Roman cities had a god specific to the city, and the Catholic Church provided “patron saints” for cities as well.

The idea that the Roman bishop is the vicar of Christ, the supreme leader of the Christian Church, is utterly foreign to the Word of God. The supremacy of the Roman bishop (the papacy) was created with the support of the Roman emperors. While most other bishops (and Christians) resisted the idea of the Roman bishop being supreme, the Roman bishop eventually rose to supremacy, again, due to the power and influence of the Roman emperors. After the western half of the Roman Empire collapsed, the popes took on the title that had previously belonged to the Roman emperors—Pontifex Maximus.

Many more examples could be given. These four should suffice in demonstrating the origin of the Catholic Church. Of course, the Roman Catholic Church denies the pagan origin of its beliefs and practices. The Catholic Church disguises its pagan beliefs under layers of complicated theology and church tradition. Recognizing that many of its beliefs and practices are utterly foreign to Scripture, the Catholic Church is forced to deny the authority and sufficiency of Scripture.

The origin of the Catholic Church is the tragic compromise of Christianity with the pagan religions that surrounded it. Instead of proclaiming the gospel and converting the pagans, the Catholic Church “Christianized” the pagan religions and “paganized” Christianity. By blurring the differences and erasing the distinctions, the Catholic Church made itself attractive to the idolatrous people of the Roman Empire. One result was the Catholic Church becoming the supreme religion in the Roman world for centuries. However, another result was the most dominant form of Christianity apostatizing from the true gospel of Jesus Christ and the true proclamation of God’s Word.

Second Timothy 4:3–4 declares, “For the time will come when men will not put up with sound doctrine. Instead, to suit their own desires, they will gather around them a great number of teachers to say what their itching ears want to hear. They will turn their ears away from the truth and turn aside to myths.”
 
Top Bottom