Leo tunawakumbuka mashujaa wetu

Sungurampole

JF-Expert Member
Nov 17, 2007
984
205

Leo ni mwezi mmoja tangu mashujaa wapenzi wetu wameuwawa huku Arusha na jeshi LETU la polisi. Tunaomboleza kwa uchungu zaidi kwa sababu Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Tanzania ambaye ndiye mwenye dhamana ya kulinda maisha ya kila mtanzania hajaona hata umuhimu wa kutueleza ni nini kilichotokea na tutarajie nini kwake yeye na majeshi anayoyasimamia.

Ni kebehi na dharau kwa watanzania kumsikia akiwaambia mabalozi wan je kuwa ilikuwa Bahati mbaya na haitaruduiwa tena…Tunajiuliza hivi rais wetu anawajibika kwetu au kwa mabalozi?

Sijui nini tatizo, je hii inakubalika popote pale? Je, hii haoni kama huu ukimya juu ya jambo ziti kama la kupoteza ‘kondoo aliokabidhiwa’ kuwalinda unatia doa kubwa katika uhalali wake kuendelea kuwa rais wetu?

Hivi hajui kwa kuwa rais amekabidhiwa maisha ya kila mtanzania na yoyote akipoteza uhai anabidi atoe akaunti? Huku si ndiyo kuwajibika ambako ni sehemu ya Utawala Bora anasema anausimamia? Je, tuliobaki nani kakabidhiwa maisha yetu? Au siku hizi tunajilinda wenyewe?

Wakati tunaomboleza tuendelee kutafakari!!:msela:

MUNGU TUPE PA KUKIMBILIA WATU WAKO WA TANZANIA
 
Mashujaa wenu wameuliwa na jeshi lenu ...! Nionavyo hapo patakuwa na tatizo ,mimi nilitarajia CDM ambayo inahusika mojakwa moja na mkasa huo ndio wawe wenye kuweka kumbukumbu ,kama tuonavyo kwa CUF wao huikumbuka siku kama hiyo ambayo iliwatokea kwa upande wao ,ila upande wa CUF hawasemi jeshi letu la polisi , kwani sidhani kama kuna Chama kina jeshi.
 
Umepotika! Nasema umepotoka kwanza kwa vile waliuwawa ni watanzania, kuwa walikuwa wana CDM haiwaondolei haki yao ynznaia ndiyo maana historia waliyoandika ni ya historia ya Tanzania siyo ya CDM. Pili kuhusu jeshi husika nasema LETU kwani hili ni la jeshi la Tanzania ambalo kimsingi wahanga hawa walitakiwa kulindwa nalo.
 
Back
Top Bottom