Ama hakika watanzania hawata sahau kile walichokifanya tarehe kama ya leo mwaka jana pale ambapo watanzania tulikwenda katika masanduku ya kufanyia maamuzi sehemu mbalimbali hapa nchini
ama eidha maamuzi tuliyofanya yalikua ni sahihi ama si sahihi ila kiukweli tarehe 25/10/2015 ni tarehe ambayo haitofutika kamwe vichwani mwa watanzania
kwa upande wangu naona ni tarehe ambayo tulifanya maamuzi ya kuisoma namba
kila uchwao matumaini yanapotea ukiuliza unaambiwa tunajenga mfumo, kwani nchi ilikua imetafunwa sana oooh mara tulichezewa sana, bila kuchukua hatua yoyote imebakia ni kupiga tantalila tu kila uchwao, pesa inaporomoka thamani,, sukari inazidi kupanda, mafuta ghali, ilihali soko la dunia ni bei ya kawaida, hospitali hakuna dawa, uwezeshaji kwa upande wa wanyonge hakuna, kiufupi ni kama tumekwama mahala, na tunaisoma namba bila shaka, japo namuomba mungu atufikishe salama tuendako, kwani hata mungu katika qur an anasema mwanzo ni mgumu, japo nchi yetu haikupata uhuru mwaka huu, tuna miaka zaidi ya 50 ya kujitawala yenyewe. na njaa inatunyemelea na hapo ndo tutaisoma sote sio serikali wala wananchi, nimealalamika sana niishie hapa na utu uzima wangu huu nisijeambiwa nimekosa adabu