Leo siku ya tatu simuongeleshi mpenzi wangu. Ungekua ni wewe ungechukua uamuzi gani?

vugwe

Senior Member
Dec 18, 2020
113
296
Wakuu habari zenu, niende moja kwa moja kwenye topic

Mimi kwa sasa ninaishi mkoa tofauti na mpenzi wangu, sasa siku ya tarehe 26 huyu dada aliniambia anaenda Dar kufata mzigo wa viatu na pia anaenda kumtembelea rafiki yake aliyesoma nae ili aule na mwaka mpya hukohuko!

Sasa kizaa zaa kikaanza alipofika huko Dar kwanza siku anafika alifika na hakupatikana siku nzima kesho yake mida ya saa saba mchana akanipigia simu kwa namba ngeni nikamuuliza vipi kulikoni akasema eti usiku alioingia Dar aliibiwa simu kwahiyo hiyo aliyonayo ameiazima ili anijulishe na akaniambia hiyo namba amepewa laini na huyo mtu awe anatumia,

Alipokata simu nikaangalia hiyo namba kwenye Mpesa nikakuta imesajiliwa kwa jina lake, nikamuuliza kwa meseji mbona hiyo namba ina jina lako akaanza kunijibu eti alikua amesahau ameisajili

Sasa tukachati hapo kama dakika kumi tukaagana lakini akaniambia nisiwe namtafuta yeye ndio atakua ananitafuta maana hiyo simu ameazima kwahiyo atakua anamrudishia mwenye nayo! Tena alinizuia katukatu kutuma sms usiku maana hiyo simu inakua iko kwa mwenyewe.

Mimi nikamwambia kwanini usichukue hata elfu ishirini ukanunua simu ndogo ukawa unatumia kuliko kuomba omba watu simu, akagoma akasema yeye hataki kununua atanunuagaa tu hata sku nyingine,

Baada ya hayo maelezo mi nilikausha nikawa kweli nasubiri yeye ndo anitafute, akawa ananitafuta mchana tu usiku hanitafuti lakini nikimtumia sms usiku inadeliver ila yeye ndio hajibu, siku nyingine ilikua inapita siku nzima hajanitafuta.

Sasa juzi tarehe mbili akanipigia simu mida ya saa tisa alasiri akaniambia yuko safarini anarudi home kwao, nikamuuliza sasa simu umeitoa wapi umenunua njiani au? Akasema eti nilikua nakutania sikupotezaga simu nilikua nayo, nilikua nataka kukupima tu kama wewe ni mume mwema, nikamuuliza hivi inawezekanaje eti umpime mtu kwa kumwambia umepoteza simu asikutafute wewe ndo utamtafuta, unapima nini sasa? Akaniambia alikua anapima kama mimi ni mvumilivu, nikamwambia au ulikua kwa mwanaume akanijibu eti 'inawezekana'

Kwakweli mimi sikuhitaji kabisa kuendeleza majibizano nae nilikata simu na sikutaka tena mawasiliano naye, niliwaza kabisa huyu alikuwa kwa mwanaume ndio maana alikua hataki tuwasiliane usiku wala hakutaka mimi ndio niwe naanza kumtafuta.

Sasa nikachukua uamuzi wa kukaa kimya kukata mawasiliano nae tangu juzi ananitumia tu sms mimi sitaki kumjibu nimeshapata mawazo ya kumuacha kabisa,

Naombeni ushauri wakuu hata kama ungekua ni wewe ungefanyeje? Je, huu uamuzi niliochukua si ni sahihi maana hapa naona kabisa huyu dada alienda Dar kuliwa kabisa.
 
Umeshachukua maamuzi tena tukupe ushauri wanini sasa au huo uamuzi ulionao umechacha!!
Anyway ningalikuwa Mimi ningalimuambia ana mbinu za kitoto sana hivyo akachezee watoto wenzake na huo ndio ungekuwa mwisho wa mahusiano changamano.
 
Nilipoona ni wale wadada wanaofuata mizigo Dar sikuona hata haja ya kuendelea kusoma post yako bro.

Hao wadada ni wauzaji tu kama wauzaji wengine Ila tofauti ni kuwa kajificha kwenye hicho kichaka cha biashara.

Epuka sana mdada anayejifanya anakuja Dar kufuata mzigo wa viatu au nguo.

Narudia Tena "EPUKA SANA".
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom